Je, Mungu analo Jina? Jina lake ni lipi?

Je, Mungu analo Jina? Jina lake ni lipi?

DINI hazijadiliwi hapa.

Litaje Jina la Mungu ikiwa unalijua.
Akili huna wewe ngedere

Kila dini ina Mungu wake .

images.jpeg
 
Akili huna wewe ngedere

Kila dini ina Mungu wake .

View attachment 2901341
Anayetwafutwa kujulikana hapa ni yule mwenye mamlaka kuu kuliko zote Mbinguni na duniani.

Ukisema Kila dini na muungu wake, wahindi watasema anaitwa ng'ombe!!

Jina ni Moja,

Taja Moja tu, Jina lipitalo Majina yote, liwwezalo kuokoa!!
 
Kutoka (Exo) 3:14
Mungu akamwambia Musa, {MIMI NIKO AMBAYE NIKO}; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu.

Yohana (Joh) 8:58
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, {MIMI NIKO}

Mwenye masikio amesikia.
 
Kwa sisi waislamu Mungu ana majina 100.

Majina yanayojulikana na wengi ni majina 99 hilo moja wanalijua mitumie na wale watu wacha Mungu sana.

Ukilijua hilo jina chochote utakachokiomba ni rahisi kukubaliwa ndani ya muda mfupi sana.
Hizo ni sifa na sio Majina
Mungu wa Waislamu anaitwa Allah.
 
Kutoka (Exo) 3:14
Mungu akamwambia Musa, {MIMI NIKO AMBAYE NIKO}; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu.

Yohana (Joh) 8:58
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, {MIMI NIKO}

Mwenye masikio amesikia.
Unamaanisha Yesu ndiye MIMI NIKO?
 
Anayetwafutwa kujulikana hapa ni yule mwenye mamlaka kuu kuliko zote Mbinguni na duniani.

Ukisema Kila dini na muungu wake, wahindi watasema anaitwa ng'ombe!!

Jina ni Moja,

Taja Moja tu, Jina lipitalo Majina yote, liwwezalo kuokoa!!
Wewe ngedere shida yako upate replies au?

Umetaka majina nimekuorodheshea .
 
Kazi kuu tatu za Mungu wa Mbinguni.

1. Kwenye uumbaji anajulikana kwa sifa ya Baba.
Baba ndiye mzalishaji wa viumbe.

Mathayo (Mat) 6:9
Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,

2. Kwenye Ulinzi wa Wanadamu na Nguvu za Kimungu anajulikana kama Roho Mtakatifu.

Mathayo (Mat) 1:18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

3. Kwenye Ukombozi wa Wanadamu anajulikana kama Yesu Kristo Mwana wa Mungu.

Mathayo (Mat) 16:15
Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
Mungu ni mmoja tu

"Sema" alijidhihirisha kwetu kwa namna tatu alizopenda yeye.

Hili ni somo la Hekima ya Mbinguni.

Ona hapa Mungu anajigeuza kama ni Binadamu ili aongee na Nabii wake Ibrahim.

Hii ni kwamba akijidhirisha ktk Utukufu wake.
Mwanadamu akimtokea atakufa kwa ile nguvu yake ya Utukufu.
Ni kwamba Mwanadamu hawezi kuhimili kumwona Mungu katika umbo la Mwili wa Nyama.


Mwanzo 18
1 Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari.

2 Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi,

3 akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako.

4 Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu.

5 Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema.

6 Basi Ibrahimu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate.

7 Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng'ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa.

8 Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala.

9 Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani.

10 Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.

11 Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake.

12 Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee?

13 Bwana akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee?

14 Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume.

15 Akakana Sara, akisema, Sikucheka, maana aliogopa. Naye akasema, Sivyo, umecheka.

16 Kisha watu hao wakaondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Ibrahimu akaenda pamoja nao awasindikize.

17 Bwana akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo,

18 akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa?

19 Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu, ili kwamba Bwana naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake.

20 Bwana akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana,

21 basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua.

22 Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana.

23 Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu?

24 Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo?

25 Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki?

26 Bwana akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.

27 Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu.

28 Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano.

29 Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini.

30 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini.

31 Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini.

32 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi.

33 Basi Bwana alipokwisha kuzungumza na Ibrahimu, akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi mahali pake.
 
Back
Top Bottom