Je, Mungu kaumba baadhi ya wanadamu kwa upendeleo wa akili na maarifa?

Unamaanisha tuzirud elimu zetu za asili na tuache elimu ya kimagharibi et??
I try to imagine hyo elimu itakuwaje[emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Kuna kaukweli humu
 
Kuna mambo mengi sana yamejificha nyuma ya pazia mpaka tupo hivi tulivyo...

Chochote utakachogundua au kuvumbua kama mwaAfrica, nchi zilizoendelea zishajiwekea utaratibu (System) kwamba ili viwe vya kimataifa vipitie katika mfumo ambao wameuunda wao... Kama kimetoka Africa hakiwezi pitishwa hata siku moja...

Mfano vumbua kitu kizuri kama mwaAfirica nchi zilizoendelea hawatokipitisha... Ila badilisha uraia mathalani kua mmarekani na kitu hicho hicho, kitapitishwa kua cha kimataifa...

Akili tunazo, uthubutu tunao na uwezo tunao, ila system ndiyo tatizo...


Cc: mahondaw
 
Unamaanisha tuzirud elimu zetu za asili na tuache elimu ya kimagharibi et??
I try to imagine hyo elimu itakuwaje[emoji13] [emoji13] [emoji13]

Wachina na wahindi wanachukua maarifa na kuyanufaisha mataifa yao

Sisi tunachukua umagharibi kama ulivyo na kuukana utaifa wetu

Wachina kwa kuchukua tu maarifa wameweza kubadilisha mfumo mzima wa elimu kuwa kwenye lugha Yao kwa maslahi yao.....

Ndio maana ni rahisi kumkuta mchina mwenye maarifa mengi lakini hajui kingereza.....

Watanzania bila ya kujinasibisha na mzungu bado haoni kama usomi wake umekamilika.....
 
Daah.... N kweli ....yaan n Africa ambako tunauana cc kwa cc...ukiandalia Global peace index(GPI)utaona idadi kubwa ya nvhi zisizo na aman n za Africa,kitu cha ajab n kwamba tunauana cc kwa cc na kwa maliasili zetymu wenyewe...hii roho mbaya cjui tumetoa wapi
 
Mbona north Korea wako strict kulko hapa ila wanateknolojia kubwa,nuclear ,rockets,na sayansi mbalimbali mkuu....sisi labda kuna kasoro nyngne
Huwezi kufananisha akili kubwa za North Korea na hawa mazuzu yenu.

Things are strict there, yeah, i know..... Lakini atleast vitu wanavyovifanya vina some sort of sense..... Sio hawa zero brain wenu wanaokimbizana na wavaa milegezo!

Unakimbizana na milegezo wakati mezani kwako kumejaa maji machafu ya visima.
 
Duuuh..kaz ipo kweli
 
Mungu alimuitaga mzungu na mwafrica ili awape akili.akawaambia wawai saa kumi na mbili asubuhi.mzungu kaja mda wa saa kumi na mbili asubuhi,mwafrica kaja saa nne asubuhi.nafkiri jibu umelipata
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hapa mkuu Nina walakini na mawazo yako...

Ukiangalia suala LA uchafuz wa mazingira hata cc licha ya kuwa hatuna viwanda tunachangia kwa kiasi kikubwa..mfano vtu kama kilimo kinachangia sana uharibifu wa mazngira na mwisho tumebaki na majangwa tu.

Kihusu matibabu sikatai yanatoka kwenye mimea ila shida inakuja kwenye kujua n mmea UPI na kiwango kipi kinamfaa magonjwa hapo panahitaji ugunduz ambao cc weusi hatijafikia...hebu angalia magonjwa kama malaria,kichaa cha mbwa,surua n.k je kwa kutumia mitishamba ambayo huna uhakika NAyo kuna kupona kweli mkuu??

Unavosema uhitaj wa mineral extraction hatuna hapo huoni ndio kuonyesha how mbumbumbu we are?? We stay on natural wealth without utilizing them!! Is that not foolishness of highest rank ndugu yangu??

Try to imagine ur current life how it would have been if u font have cell phone,no transport yaan ukitaka kuna dar kutoka kigoma inakubid utembee HV is that normal life??

Bado hujanishawishi ndugu....
 
Mkuu umeibua hoja nzuri sana. Nataka nikufahamishe tu kuwa kama tukitazama kwa hoja yako hiyo ya Upendeleo basi Mungu alitupendelea maarifa sisi waafrika ila tu hatuna juhudi hasa kizazo hiki cha sasahivi.
Mwandishi Walter Roodney aliwahi kuandika kitabu cha HOW EUROPE UNDERDEVELOPED AFRICA. Katika kitabu hiko ameelezea namna gani Afrika ilikua na maendeleo zaidi ya wazungu.
Ukisema kwamba waafrika hatuna maarifa ya kugundua kitu unakua unakosea sana. Kwanza tambua kwamba uhusiano wa Mzungu na mwafrika ulianza mnamo karne ya 15. Hapo tunazungumzia miaka ya 1400.
Wazungu walipokuja Afrika kwa mara ya kwanza, walikuta tayari tumeendelea kuzidi wao wenyewe kiasi kwamba wakaiga sehemu kubwa ya teknolojia yetu na kwenda kuziendeleza kwao. Najua utabisha katika hili, lakini nitakudhibitishia kwa nadharia za kihistoria na kisayansi kupitia nyanja zifuatazo.

ELIMU
(Hesabu na maandishi)
Hesabu nyingi unazoziona hivi leo zilianzia MISRI (Egypt). Njia hii tunayotumia leo kuhesabu ilianza zaidi ya miaka 35000 iliyopita kutoka Africa. Wamisri walianza kuandika vitabu kuhusu hesabu za kugawanya kuzidisha, hesabu za sehemu na Geometry.
Mfumo wa kuandika herufi tunazozitumia leo, ulianza Misri pia mnamo miaka ya 3100 KB (Kabla ya kristo).
Kalenda inayoipa dunia siku 365 na robo , ilitengenezwa na wamisri. Kugwanywa kwa masaa 24 kwa siku kulianza misri zamani sana na enzi hizo walitumia misimu hasa ya maji kutambua masaa.

DAWA

Katika hoja yako umesema kwamba wazungu wamegundua dawa. Sio kweli!! kuna tofauti kati ya kugundua na kuendeleza. (invent and develop)
Dawa zinazotumiwa leo ziligunduliwa Africa zamani sana huko Misri, Nigeria na Afrika kusini enzi hizo kabla nchi hizo hazijapewa hayo majina. Walitumia mizizi na mimea kutibu magonjwa mbalimbali. kwamfano Salicylic acid kwaajili ya kupunguza maumivu ambayo leo hii wazungu wameindeleza tunaitambua kama Aspirin. Kaolin Acid kwaajili ya ugonjwa wa kuhara ambayo leo hii dawa inaitwa Kaopectate. Utafiti umeendelea kueleza kua, waafrika walikua na uwezo wa kufanya upasuaji (under antiseptic conditions) wakati huo ujuzi huo ndo ulikua unaanza kuibuka barani ulaya.

ENGINEERING
Moja ya kidhibiti hai cha utafiti kwamba Africa ilikua na maengineer na maachitecture wake hata kabla ya wazungu ni Pyramid of Giza (Cairo) ambayo ipo kwenye maajabu saba ya dunia. Utafiti unaonyesha Pyramid hyo ilijegwa mnamo Miaka ya 2580 KB (Kabla ya kristo) kipindi ambacho hta mzungu hakuwa na jengo lolote la ajabu kama hilo. Kinachofanya pyramid hii iwe ya ajabu ni ufundi uliotumika.
Waliosimamisha pyramid ile walibeba tani milioni sita na nusu za mawe ambapo kila jiwe lilikuwa na tani zisizopungua 9. Kwa kipindi hiko ambapo hakukua na mawinch wala minyororo wala cement waliwezaje kupandisha haya mawe? Ni wazi kabisa mwafrika alikua na teknolojia ya kipekee kabla ya mzungu.

Nina mifano mingi natamani kukushirikisha ila kwa leo naishia hapo. Waafrika tuna akili na kama ni upendeleo basi Mungu alitupendelea sisi. Ila tu waafrika sisi ni wavivu kujituma na kufikiri. Mzungu hana akili kama tunavyodhani, ila tu kapewa juhudi na kiu ya kujifunza. Sisi tumelala sana na kwa mantiki hiyo Mzungu anaokana ana akili kuliko sisi.
ASANTENI!!
 
Nadhani una miss pointi ndugu.

Nimeeleza vizuri hapo juu kwa kuhoji "je tunahitaji kila kinachotokana na teknolojia?"

Sidhani kama athari za kilimo zina ukubwa sawa na uharibifu unaosaabishwa na viwanda na uvunaji holela wa miti, ni asilimia ngapi ya mashamba yapo kando ya mito, na je kama hali ya kunyesha mvua ingebaki ileile tangu awali ni wanagapi wangeenda kulima kando ya mito? je ni kweli jamii zetu hazikuwa na mila/makatazo ya uharibifu wa mazingira?
nakumbuka hotuba moja ya Mwalimu alisema kwao Wazee wao waliaminishwa kuwa kukata miti ni kukaribisha mikosi/mashetani...sasa je huoni jamii zetu zilikuwa na njia za kutunza mazingira ila ni taarifa sahihi tu hazipatikani kuhakiki ni kwa jinsi gani kila jamii ilikuwa na mbinu zake...sasa kwa nini nisiamini kuwa pia enzi hizo jamii ziliweka marufuku kulima kando ya mto?

Kuhusu tiba sidhani kama kuna haja ya kuzusha mabishano, hebu jiulize ni jamii ngapi unazifahamu ambazo mpaka sasa wanaamini kwenye tiba ya baadhi ya mimea? na mimea sio lazima ilenge mimea ya porini...hata mboga na matunda tunayotumia kila siku...hivi kama kuna virutubisho unahitaji kutoka kwenye Parachichi unahitaji kipimo gani mahsusi ili ufikie uhitaji? wewe kula parachichi tu basi halitokudhuru, hiyo malaria unayoitaja nayo kumbuka imekuzwa sana na uwepo mabadiliko ya tabia nchi, yaliyosababishwa na teknolojia..sehemu kama Lushoto haikuwa na Malaria awali, sasa wao wangehitaji dawa ya nini?

Hizo simu za mikononi, Ndege za kukupeleka Kigoma unaposema, kwa nini unanilazimisha nidhani kwamba nisingeishi salama bila uwepo wake? kwani ni lazima niende Kigoma? ndio maana nimehoji tulihitaji kula kilicholetwa na teknolojia?
 
HAPA NAONA BORA TUKACHUNGUZE HISTORIA KABLA YA GERMAN EAST AFRICA, YAANI KABLA YA "TANGA-NYIKA" ILIYO UNDWA NA MJERUMANI.
TANGA = BAHARI .. SAIL
NYIKA = MBUGA .. WILDERNESS

TULIKUA NA WATU WENYE ELIMU ZA HALI YA JUU.
WATU WENYE UJASIRI WAKUMONDOA MJERUMANI VITA VYA MAJI MAJI..
KABLA YA HAPO TULIKUA AKINA NANI SISI?!?! [emoji362] [emoji353] HISTORY WHERE FROM TO DATE. TUTAPATA MAJIBU YA KWANINI TUMEBAKI KUZUBA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…