Tuambie chanzo cha uhai na maisha apa duniani
Ama binadamu alianzia wap.
Na vitu vyote kukaa kwenye mpangilio viliwekwa na nani?
Unajidanganya na kujipumbaza
Na kama mpaka leo hujaonana na mungu mtafute kwa bidii sana
Point ya muhimu kabisa kuelewa ni hii. Tunaweza kujua jibu fulani si sahihi, hata kama hatujui jibu sahihi ni lipi.
Halafu, kuanzia hapo, tunaweza kutafuta jibu sahihi kwa kufuatisha elimination method itakayotuondoa kwenye majibu yasiyo sahihi na kutupeleka kwenye majibu yaliyo sahihi.
Mtu kutokujua chanzo cha uhai haimaanishi chanzo ni Mungu.
Mtu kutokujua jibu la swali, haimaanishi kwamba hawezi kujua jibu fulani si sahihi.
Nitakupa mifano miwili.
Ukijua square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, halafu mtu akakuambia square root ya 2 ni 10, unaweza kujua hili jibu la 10 si sahihi, bila hata kujua square root ya 2 ni nini. Kwa sababu ushajua square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2. Na 10 ukii sqiare unapata 100, si 2.
Hapo utakuwa ushajua kwamba 10 si square root ya 2, bila hata kujua square root ya 2 ni nini. Katika kutafuta square root ya 2, utazitoa namba zote kubwa kuliko 2, by elimination method.
Mfano mwingine.
Kukiwa na mwanamme Juma mwenye umri wa miaka 30 leo, na binti mchanga Jeni mwenye umri wa miezi 6 leo, halafu tukaambiwa huyu binti Jeni mwenye umri wa miezi 6 leo ndiye mama mzazi wa kibaiolojia wa huyu mwanamme Juma mwenye miaka 30 leo, tutajua habari hii ina uongo, si sahihi.
Tutajuaje? Tutajua hivyo kwa sababu mantiki ya timeline hairuhusu mtoto mchanga mwenye miezi 6 leo kuwa mama mzazi wa kibaiolojia wa mwanamme mwenye umri wa miaka 30 leo.
Kwa hivyo, tunaweza kujua huyu binti mchanga Jeni mwenye miezi 6 leo hawezi kuwa mama mzazi wa huyu mwanamme Juma mwenye miaka 30 leo, kwa kutumia mantiki tu, bila hata ya kujua mama yake mzazi halisi Juma ni nani.
Sasa, unachofanya hapa ni hiki.
Mimi nakwambia hovii, Jane mwenye umri wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama yake mzazi wa kibaiolojia Juma mwenye umri wa miaka 30 leo. Kwa sababu mantiki hairuhusu kitu hiki.
Wewe unapinga, unasema lazima binti Jane mwenye umri wa miezi 6 leo ndiye mama mzazi wa kibaiolojia wa Juma mwenye miaka 30 leo, kama napinga, nikuoneshe mama yake Juma ni nani.
Hukubali kwamba, bila hata kumjua mama yake Juma ni nani, tunaweza kujua kuwa, Juma, mwanamme mwenye miaka 30 leo, mama yake hawezi kuwa Jane, binti mwenye umri wa miezi 6 leo.
Nakwambia hivi, 10 haiwezi kuwa square root ya 2. Naweza kukuambia hilo hata bila ya kujua square root ya 2 ni ipi, kwa sababu najua square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2.
Wewe unanijibu, sqiare root ya 2 ni lazima iwe 10, kama si 10, square root ya 2 ni ipi?
Hujaelewa kwamba tunaweza kujua jibu fulani si sahihi hata kabla hatujajua jibu sahihi ni lipi.
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo, watu wanaoelewa mambo wameshamtoa kwa elimination method.
Wamebakia watu wanaolazimisha awepo tu, ambao, ukiwautaka wathibitishe Mungu yupo, hawawezi.
Wanakupa hoja za logical non sequitur fallacy tu kama "uwepo wako ni uthibitisho Mungu yupo".
Au wanakupa hoja inayothibitisha M7ngu hayupo, huku wakifikiri wanakupa hoja inayotetea uwepo wa Mungu.
Mtu anasema kama Mungu hayupo, hii complexity ya ulimwengu imetokeaje?
Akiwa hajui kwamba, ikiwa kweli complexity haiwezi kutokea bila kuumbwa, hata huyo Mungu mwenyewe naye atahitaji muumba wake, na muumba wake atahitaji muumba wake, ad infinitum, ad nauseam.
Katika ulimwengu ambao hauna Mungu.
Hoja hii kwa juu juu inaonesha mtu anatetea uwepo wa Mungu, lak8ni, ukiipima kwa kina, ni hoja inayoonesha Mungu muumba vyote hawezi kuwepo.
Lakini, sitegemei kila mtu aelewe ninachoandika.
Kwa sababu watu wana uwezo tofauti kufikiri, historia tofauti, umri tofauti, upeo tofauti, elimu tofauti, etc.
Ningependq zaidi kujibizana na watu ambao angalau wanaelewa hoja zangu na wanaweza kuzijibu.
Sio wale wa "Mungu yupo, uwepo wako unathibitisha hilo". Au wale wa "Kama Mungu hayupo, haya mambo ya ulimwengu yote yanajiendeshaje yenyewe. Yamejiumbabyenyewe? Lazima yameumbwa na Mungu"