Je, Mungu wa walokole hasikii hadi apigiwe makelele Makubwa?

Acha kabisa kabisa 🀣 πŸ˜‚ πŸ˜† 🀣 πŸ˜…
 
Halafu wale wavaao mashati ya vitenge ndio wale waendao kitafuta mademu kanisani.
Hapana. Hawa wanaovaa mashati ya kitenge ni mandondocha. Kila asemacho mkewe yeye huitikia ndio.

Hata mke wake alisema leo naenda kulala kwa nabii, jamaa huitika sawa mama, nakutakia usingizi mwema wenye upako
 
Imani yetu "sisi" wapiga mayowe ni kwamba,Mungu yupo mbali mnoo.Hivyo inabidi tupaze sauti zetu ili zifike mbingu ya Saba.Ameeen?
Nyie mnaona mbingu ya saba ni karibu hivyo?!
Mkiwa hapo Dar es salaam Ubungo kelele zenu hata Kimara hazifiki, zitafika mbingu ya saba?!
 
MamaSamia2025 kajenga msikiti Coco Beach kwenye eneo la umma. Jengo ni la kudumu
Kuna msikiti coco Beach β›±πŸ˜πŸ˜ itakuwa mashekh mudi boy wanataka kuitwa beach boy vipi mashekh watake msikiti kwenye maeneo kama hayo?
 
Hivi makanisa ya kikatoliki hayana spika za nje kweli?!
 
Kelele. Soma hiyo tafsiri ya Kingereza hujaona neno noises?
Shangwe ya mungu ni ya rohoni ...soma mariam anasema roho yangh yamshangiria bwana pia hizo shangwe za makelele mbona aziendani na matunda ya rohoni upendo wema uchamungu uhadilifu upole unyenyekevu nk tunaona kinyume chake wezi mataperi vibaka wahuni washenzi wanafiki nk
 
Kwa njia yake yeye pamoja naye na ndani yake wewe Mungu baba Mwenyezi katika umoja wa Roho Mtakatifu unavifanya vitu vyote kuwa sifa na heshima yako, milele na milele
 
Kwanza ukiacha ukiziwi ni DJ bila mziki sala haitimii,Na usipomwabudu kikichaa kichaa hupati baraka.Mungu wa walokole anaweza kumponya muumini mpya kanisani mwenye magongo lakini akashindwa kumponya muumini wa zamani kanisani aliyepinda miguu na atambaaye.
 
Zaburi 68:3 Bali wenye haki hufurahi, Na kuushangilia uso wa Mungu, Naam, hupiga kelele kwa furaha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…