Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Ndio haya ninayosema. Ndugu wa mume hawana huruma saa nyingine
 
Ndoa za siku hizi zimejaa migogoro sababu wanachagua wenza wasiofanana nao/hawana misingi inayofanana. Kama wa kwako 50 50 sawa, sisi wengine tuachie waume zetu wanaotuhudumia 100 na 50 zetu tunazo. Siku ya siku hata yeye akikwama (kwa sababu zisizozuilika), hausiti kumpiga tafu babe sababu unajua mlipotoka.
 
Ndiyo ndoa yenye maelewano mbona unafanya tu palipo pungua, bila shida yeyote
 
๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†
 
Kama mwanamke lazima achangie kifedha ili ndoa ifanye kazi, basi mume naye lazima ashiriki sawa kwenye majukumu ya nyumbani na malezi. Ndoa siyo biashara ya kugawana gharama, ni kushirikiana katika maisha kwa kila hali.
Sasa mtoke wote asubuhi muende kazini na mrudi wote jioni huku kazi za nyumbani pamoja na kuangalia watoto zinafanywa na dada wa kazi. Wewe mwanamke unakua na mchango gani kwenye iyo ndoa? Kipato chako unapeleka wapi?
 
Lakini kabla ya kulipia ada watoto wa dada ni lazima kwanza nihakikishe watoto wangu wameshatimiziwa mahitaji yote, nitakuwa kichaa eti niwalipie ada watoto wa dada yangu hali yakuwa watoto wangu wamekaa nyumbani.

Sasa inashangaza kuona ww mwanamke watoto wana mahitaji fulani mwanaume ana kuambia sina pesa ebu na ww yatatue una kataa eti hilo siyo jukumu lako ila unaenda kutua matatizo ya watoto wa dada yako ambao nao wana baba yao mwenye jukumu la kutatua matatizo hayo.

Kabla ya kutoa msaada nje ni lazima uhakikishe kuwa ndani ya familia hakuna pengo lolote sio unaacha pengo kwenye familia yako unaenda kuziba mapengo kwenye familia za wenzako.
 
Wanawake wengi wanaofanya kazi mara nyingi ni kwaajili ya uhuru wa kipato na kuwekeza kwaajili ya kipindi cha kiangazi. (Mume kufariki, kuugua, kukimbilia michepuko) kwaajili yake, wanaomtegemea na watoto wake
Kwamba hapa unachomaanisha hasa ni kwamba pesa ya mwanamke huwa inaanza kutumika ndani ya familia pale mwanaume anapofika ukomo wa kuhudumia familia sio? Ila siku nyingine zote ambazo mwanaume huyo anawajibika ipasavyo pesa ya mwanamke yenyewe haitumiki kabisa na kama ataitumia basi ni kuwasaidia ndugu zake huko kwao sio?

Kwa hii parasitic mindset ndio maana huwa nasema nyie wanawake wasomi na wafanya kazi huwa ni hasara kubwa sana kwa mwanaume , yaani nyie huwa ni liability kwenye ndoa..!!

Binafsi huwa nawahurumia sana vijana wanaowaoa nyie wanawake wa kisasa kwa kuangalia kazi na elimu zenu.
 
Kwanini iwe hiyari ww kuipiga tafu familia pale inapo kwama kwani hiyo familia na hao watoto ni wa mwanaume peke yake?
Ya kwamba ww mwanamke kumlipia ada mtoto, kumnunulia nguo, kumnunulia chakula ni hisani na sio jukumu lako?
Ya kwamba hao watoto wakija kukua na kufanikiwa watakuwa wa mwanaume peke yake ww hutofaidi mafanikio yao?
Tena nyinyi wana wake ndo wafaidika wakubwa wa watoto pale wanapo fanikiwa.
Mimi nitahudumia familia kwa asilimia 100 iwapo mwanamke atakuwa amekaa nyumbani analea watoto, lakini ukijitia kwenda kutafuta hela hizo hela zitakuwa chini ya mamlaka ya kifamilia na zitatumika kwenye maendeleo ya familia tofauti na hapo ni big no.
 
Vipi kazi za nyumbani naye mwanaume atafanya kama mkewe anavyofanya?
Sio mnarudi wote jioni mke anaanza majukumu y nyumbani mwanaume anashika remote yeye na TV, mke achangie kwa hiari sio lazima.
Ukiniletea hii mentality mimi mbona utafurahi, yaani hata kukuachia hela ya matumizi ndani itakuwa ni hiari yangu sio lazima, ukipatwa na changamoto binafsi kama kufiwa,kuugua kukusaidia kwangu kutakuwa ni kwa hiari sio lazima. Kiufupi tu vitu vingi sana nitavifanya kwa hiari na sio kama wajibu... maana unajifanya mbinafsi hivyo mimi nitakuonesha ubinafsi uko vipi na unafanywaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ