Nina ushuhuda. Mtoto wa Shangazi yangu alibakwa na watu zaidi ya 10, miaka ya tisini akapata maambukizi ya ugonjwa wa zinaa. Kwakuwa alikuwa mdogo wa umri (14yrs by the time) likashughulikiwa swala la yeye kubakwa, watuhumiwa walikamatwa na wakaadhibiwa vifungo virtually gerezani.
Lakini yule binamu alipata infection, kizazi kikaoza na hakukuwa na namna nyingine isipokuwa kukitoa.
Alifanyiwa upasuaji na akatolewa na kuambiwa hatozaa tena. Baada ya miaka mingi akapata jamaa, auntie akamjulisha kabisa jamaa kuwa atafute mtu mwingine maana yeye hana kabisa uwezo wa kuzaa. Jamaa akakomaa naye wakaoana.
Walipooana wakawa watu wa maombi sana, aiseee, binamu alipigwa maombi hadi kizazi kikaota, sasa ana watoto wanne