Adverse Effect
JF-Expert Member
- Oct 8, 2017
- 2,049
- 5,449
Usichokijua ni kama usiku wa giza, hapo kuna sarakasi na sintofahamu.Nina ushuhuda. Mtoto wa Shangazi yangu alibakwa na watu zaidi ya 10, miaka ya tisini akapata maambukizi ya ugonjwa wa zinaa. Kwakuwa alikuwa mdogo wa umri (14yrs by the time) likashughulikiwa swala la yeye kubakwa, watuhumiwa walikamatwa na wakaadhibiwa vifungo virtually gerezani.
Lakini yule binamu alipata infection, kizazi kikaoza na hakukuwa na namna nyingine isipokuwa kukitoa.
Alifanyiwa upasuaji na akatolewa na kuambiwa hatozaa tena. Baada ya miaka mingi akapata jamaa, auntie akamjulisha kabisa jamaa kuwa atafute mtu mwingine maana yeye hana kabisa uwezo wa kuzaa. Jamaa akakomaa naye wakaoana.
Walipooana wakawa watu wa maombi sana, aiseee, binamu alipigwa maombi hadi kizazi kikaota, sasa ana watoto wanne
Kwanza tujiulize ni kweli huyo binti alitolewa kizazi?
Kizazi ni nini? Kwa mwanamke/msichana tunaongelea kuhusu uterus mfuko/kiungo ambacho unajumuisha ovari, mirija, neva, mishipa ya damu na sehemu ya uuke( k au vagina), hadi matiti hapo ni kwa kifupi tu nimejaribu kueleza.
Kutolewa kizazi chote kitaalamu kwa kufanyiwa upasuaji ni total hysterectomy( yaani kizazi chote hutolewa na viungo vingine vinavyosapoti mfuko wa uzazi), hapa mwanamke/msichana hawezi na hataweza kushika mimba/ujauzito.
Kutegemea na kiwango, aina ya maambukizi na complications alizopata pia kuna uwezekano hakutolewa kizazi chote bali walitoa pengine upande mmoja wa mirija wakaacha upande mwingine, baadhi ya magonjwa ya zinaa husababisha madhara katika kizazi kupelekea mirija kuziba kabisa, kwa hiyo kitaalamu mimi na wewe hatujui na hatuna uhakika wa hili isipokuwa daktari na timu waliyofanya upasuaji.
Maandiko yanasema "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa".