Je, Mwanamke mvuta Bangi anafaa Kuolewa?

Huku Arusha mwanamke kuvuta bangi ni kama huko kwenu Dar mwanamke kula popcorn ๐Ÿฟ
 
Aseeee hilo lipo kwa wachache kuna single MMA anapuriza bangi uyo lkn analeola vizur tu
 
Mbona tunaoa walevi why bangi, oyaa kama unataka kuzaa Yesu fresh piga chini tafta mlokole
 
Wanajeshi wengi wanavuta bangi lakini wanaendesha maisha vizuri tu. Hata mwanamke akivuta bangi, bado ana uwezo wa kutunza na kuilinda familia yake.

Usiwanyanyapae wavuta bangi.
 
Wanajeshi wengi wanavuta bangi lakini wanaendesha maisha vizuri tu. Hata mwanamke akivuta bangi, bado ana uwezo wa kutunza na kuilinda familia yake.

Usiwanyanyapae wavuta bangi.
 
Kupungua kwa idadi ya wanawake wenye maadili na discipline isikufanye kushusha vigezo vya asili vya mke. Mwanamke kuvuta bangi ilikuwa ni maamuzi yake binafsi sio maagizo ya MUNGU, why sasa unataka kumuingiza katika maagizo ya MUNGU ili awe mke wa ndoa?

Ni bora uwe malaya ila kuliko kula kiapo cha kujenga uzao na mwanamke kahaba, mzaa watoto nje ya ndoa, muongo, mdangaji, mtoa ujauzito, mpenda pesa/mali, mwenye tamaa za mambo makubwa kushinda uhalisia wake, etc.

Kataa mwanamke yoyote ambaye hafit profile ya mke mwema kwasababu haimgharimu chochote binti kujitunza na kufuata muongozo wa vitabu vya imani na kuishi kwa njia za kujitunza.

Mtu anavuta bangi tafsiri yake huyo hajitambui na hajielewi yeye ni nani na majukumu yake ya kike. Ni vema kuishi kwa mipaka na kujiheshimu.

Mwanamke anayevuta bangi si ajabu ameshawahi fanya mambo ya ajabu na huwa wanakuwa na company ya wahuni. Je unajua wamefanya mambo mangapi katika uhuni wao?
 
Kwann kwa mwanamke picha ya ajabu kwa mwanaume isiwe picha ya ajabu
Unalinganisha kiwembe na panga kisa vyote vina makali unasahau kazi zake?

Mwanaume anaweza kuwa anavuta bangi ila sio mlezi mkubwa wa watoto. Wewe unaweza acha watoto wako walelewe na mwanamke au mama mvuta bangi?

Unajua bangi inafanya nini katika mwili kwa maana ya kuufanya urelax hadi unakuwa haupo sensitive na vitu vingine kama watoto na kadhalika.

Mtu mwenye uraibu wa bange ni likely atakuwa kwenye mazingira ya kutumia na madawa ya kulevya, wewe unataka mtu wa namna hiyo mjenge familia ya aina gani?

Hebu muwe mnauliza maswali kwa akili sio ushindani
 
Mawazo potofu na hayana uhalisia, woiiiiiih
 
Mbona sikutanagi na hao warembo wanao vuta ๐Ÿ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ