Je, mwanamke uko tayari kumpa pesa mchumba wako akakulipie mahari kwenu?

Dada yangu watu walioa kwa kondoo tu,tena dingi alikuwa anataka Bible tu!!shemeji hakuwa na kitu kabisa ila ndo hivyo dada yangu alikuwa ameoza amekufa kabisa!!ndo ilifungwa vizuri tu!! Ila baada ya ndoa
1.shemeji pesa ilikuja kama mvua dili zake zilikubali sana.
2.dada yangu hakuna rangi aliacha kuona kwa maana jamaa aliona kama vild sisters hata kwao kama vile hawa mthamini vile kisa tu mahari alilipa kidogo!!
3.kidume wa kweli hawezi pokea pesa ya mwanamke kwenda kulipa mahari kwa sababu hiyo inaondoa dhana ya kutoa shukrani mahari ni kama asante kwa wazazi wa yule binti unayetaka kumuoa ,so hata kitenge na kanzu tu inatosha.kwa maana huna uwezo wakuwalipa gharama walizotumia wazazi kwa binti yao!!
 
Ila mimi naijua familia moja ambayo baba yule hana hata mia ,lakini mwisho wa mwezi mama anakabidhi kibunda chote na baba ndo anapanga matumizi,mama yuko barrick pesa ipo ni boss mkubwa sana.
Maendeleo kwao usipime mijumba mikali,ya wapangaji ,watoto wamesoma international schools wote.ila baba hana kazi yeye akaimka kwenda kunywa supu kununua gazeti basi
Na wanapendana sana huwezi kujua kama yule baba hana kazi labda uambiwe na majirani kwa hiyo maisha ya mapenzi hayana formula!!
 
Iliwahi chambuliwa kibiblia kuwa mwanamke kujitolea mahari wewe mwenyewe siyo sahihi hata kidogo !

Tena ndoa za hivyo wengi wameishia majuto !

Mwanaume anakuwa tegemezi hakununulii hata chup.

Mwanamke hata kama unafanyakazi nzuri unaingiza hela nyingi lakini hela ya mume nayo inautamu wake!
Kwa kweli hela ya mume ni tamu sana na zawadi za mume ni nzuri
 
Ngoja waje kukupa muongozo...

Ila zama hizi wapo wanawake wengi tuu, wanafanya hivyo...

Cc: mahondaw
 
Natamani wanaume wote msome hapa.
@Emery, @Extrovert

Back
Top Bottom