Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kula mzigo tu kwa wakati wako. Usiweke matarajio kwake.Kwa hiyo nifanye nini bro?
Kama kuandika hujui utaweza ndoa?
Sasa una miaka 22 umenza kujitwisha mizigo yote hiyo, utazeeka vibaya mkuu.
Wenzio tuna 30 years na hatuna mambo mengi hivyo.
Endelea ku "ongeya" nae.
Vinausiana vip sasa kwan kabla ya kuletewa elimu ya kuandika watu walikuwa hawaoani?Kama kuandika hujui utaweza ndoa?
Ni kweli aisee,iyo miaka 22 kweli uteseke ivo,Hivi watoto mbona mnakimbilia sana izo ndoa.Sasa una miaka 22 umenza kujitwisha mizigo yote hiyo, utazeeka vibaya mkuu.
Wenzio tuna 30 years na hatuna mambo mengi hivyo.
Huu mwandiko unaumiza macho
[emoji1787]Sasa una miaka 22 umenza kujitwisha mizigo yote hiyo, utazeeka vibaya mkuu.
Wenzio tuna 30 years na hatuna mambo mengi hivyo.
Pole,nadhani pia umri na kiwango cha elimu vinaweza kuwa ndiyo shida,wala siyo yeyeJambo ndugu zangu,
Nahitaji msaada wenu.
Mimi ni kijana nina miaka 22 niko kwenye mausiano na dada fulani ambaye tuna tarajia kuoana. Sasa kuna vitu ambavyo vina ni tatizaga na jiulizaga sipatagi majibu.
Na vitu hivyo ni kuhusiana na tabia ya huyo binti. Mara nyingi huyu mtoto wa kike huwa hanisikilizi. Kila nikimwambia sitaki kitu fulani nikione kwako utakuta tunabebana, kama atakubali yaani ni kwa mbinde kabisa na tena baada ya siku fulani kupita utakuta tena ulicho mkataza ndicho anachokifanya.
Na mara nyingine utakuta anaongea na mimi kwa sauti kubwa; hata ukimwambia mwanaume hafokewi yeye huwa hajali hata kidogo. Na ukizidisha kumwambia kuhusiana na kuongeya kwako uta kuta ana ni jibu ndo maana sipendagi kuongea na wewe.
Yeye ndo rafiki wa wanaume utakuta mwanaume akimwambia njoo twende huku anakubali, anapokuwa yeye ndipo wanaume walipo kuwa na matani nao ya kugusana gusana. Hata nikimwambia aache tabia hiyo utakuta najibiwa "jiamini"
Yeye ndo mtu wa kupost picha na video za kijinga kwenye status za Messenger na WhatsApp utakuta amepost picha mara anapiga kiss mara anatoa ulimi nje mara anaimba, mara anabinuwa matako yake.
Nikimshauri naambiwa mimi ndo nina wivu.
Mwanaume akimsimamisha hata kama yuko na mimi utakuta anasimama na akiombwa namba anatoa bila tatizo.
Sasa huyo mtoto wa kike nimeshafunga naye ndoa. Kulingana na mila zetu sisi hufunga kwanza ndoa halafu mke utaenda kuchukua siku ya kwenda kuweka mali.
- Ni muongo sana
- Anapenda mauzo sana
- Ana dharau watu wengine mpaka na mimi
- Ana kiburi
- Hujiona mrembo na mara nyingi husema hawezi kosa soko yeye ni mrembo
Sasa hapo ndipo nina maswali. Je, mwanamke wa hivi kweli anaweza badirika katika ndoa au pesa zangu niziwekeze kwenye mambo mengine?