Kama una akili ya biashara, fanya biashara kwanza.
Kwa mtaji wako wa milioni tatu unaweza ukanunua bodaboda zilizotelekezwa Polisi, unazikarabati kidogo halafu unauza kwa bei ya faida. Polisi unaweza ukapata bodaboda hadi kwa Tshs. 300,000/- ukaja kuiuza kwa 700,000/- hadi 900,000/- (ukarabati 100,000/-). Lenga sana bodaboda ambazo ukiuza kwa bei ya mwisho milioni moja unapata faida. Hapo kwenye chini ya milioni moja ndo utapata wateja wengi sana.
Au ukanunua amana zilizotelekezwa kwenye taasisi za mikopo midogomidogo (Microfinance Institutions) kwa bei chee ukaziuza kwa bei ya faida. Kwenye microfinance utapata amana kama vile simu, laptops, flat screen na bodaboda pia.
Ila kama akili ya biashara unaona huna, basi ni bora ukajenga. Chukua ramani ya kimaskini ya Kituo Kidogo cha Polisi utapata chumba cha kulala na sebule unaanza mdogo mdogo. Hapo sasa itabidi ufunge ndoa na kazi. Yaani jitahidi uwe mfanyakazi bora unayemfurahisha bosi wako ili mkataba ukiisha akupe mwingine. Na wakati huohuo ukiwa unajituma kutafuta ajira sehemu zingine kwa sababu mara nyingi sana ukibadilisha mwajiri ndo mshahara huwa unapanda. Mwajiri uliyenaye ni ngumu sana kukupa nyongeza yoyote ya maana ya mshahara.
Hakikisha pia unafungua akaunti Linked-In na kufanya networking kupitia mtandao huo. Ukifunga ndoa na ajira mitandao kama Facebook na Insta haina maana tena kwako. Mtandao wako ni Linked-in.