Vhagar
JF-Expert Member
- Jun 8, 2015
- 20,550
- 39,949
yaah kujua kusimamia mipaka kati ya familia yenu na yako.Wala! Inategemea na Akili ya mume.
Mume akiwa Smart mbona mnaishi tuu.
Mume awe na uwezo WA kumuambia Mama ukweli.
"Mama wewe sio mke wangu, mke wangu ni to yeye. Hii ni familia yangu. Mimi ndio mume na Mwanaume pekee humu ndani. Wote mtafuata Oda zangu. Baki kwenye nafasi yako kama Mama"
"to yeye wewe sio Mama yangu, wewe ni mke wangu. Wewe ndiye mama wa familia hii. Kabla sijakuoa nilikufundisha Kupenda Haki na uadilifu. Na nilikuoa baada ya kuthibitisha kuwa unaweza kutenda haki na sio vinginevyo. Mtendee haki Yeyote aliyekuwa humu ndani Kwa nafasi yake. Pia usikubali kuonewa na kunyamazia mambo ikiwa unaona hayaendi sawa"
Waambie kabisa nyumbani kuwa mtu yeyote ambaye hatatenda haki ATAONDOKA bila kujali nafasi yake.
Atakayeweza kufuata haki na sheria za hapo nyumbani atadumu Kwa Raha mustarehe.
Kuwa Mama hakukufanyi usifuate sheria na. Kutotenda haki katika nyumba yangu.
Kuwa Mke hakukufanyi usifuata niliyoyaagiza.
Huyu ni Mama yangu
Wewe ni mke wangu na Mama wa watoto wangu.
Kila mtu ananafasi kubwa katika maisha yangu. Lakini haimaanishi nafasi hiyo ndio mniletee ushetani katika nyumba yangu.
Waambie huwezi ishi na Shetani nyumba moja.
Be a Man, not like a man
Ukichemka hapa ndio shida huanzia. Na ukikuta mama kichefu chefu basi ndoa itapata shida sana.