Je, ni halali kumpiga makofi mama mkwe anayekukera kila siku?

Je, ni halali kumpiga makofi mama mkwe anayekukera kila siku?

Wala! Inategemea na Akili ya mume.
Mume akiwa Smart mbona mnaishi tuu.
Mume awe na uwezo WA kumuambia Mama ukweli.
"Mama wewe sio mke wangu, mke wangu ni to yeye. Hii ni familia yangu. Mimi ndio mume na Mwanaume pekee humu ndani. Wote mtafuata Oda zangu. Baki kwenye nafasi yako kama Mama"

"to yeye wewe sio Mama yangu, wewe ni mke wangu. Wewe ndiye mama wa familia hii. Kabla sijakuoa nilikufundisha Kupenda Haki na uadilifu. Na nilikuoa baada ya kuthibitisha kuwa unaweza kutenda haki na sio vinginevyo. Mtendee haki Yeyote aliyekuwa humu ndani Kwa nafasi yake. Pia usikubali kuonewa na kunyamazia mambo ikiwa unaona hayaendi sawa"

Waambie kabisa nyumbani kuwa mtu yeyote ambaye hatatenda haki ATAONDOKA bila kujali nafasi yake.
Atakayeweza kufuata haki na sheria za hapo nyumbani atadumu Kwa Raha mustarehe.

Kuwa Mama hakukufanyi usifuate sheria na. Kutotenda haki katika nyumba yangu.
Kuwa Mke hakukufanyi usifuata niliyoyaagiza.

Huyu ni Mama yangu
Wewe ni mke wangu na Mama wa watoto wangu.
Kila mtu ananafasi kubwa katika maisha yangu. Lakini haimaanishi nafasi hiyo ndio mniletee ushetani katika nyumba yangu.
Waambie huwezi ishi na Shetani nyumba moja.

Be a Man, not like a man
yaah kujua kusimamia mipaka kati ya familia yenu na yako.
Ukichemka hapa ndio shida huanzia. Na ukikuta mama kichefu chefu basi ndoa itapata shida sana.
 
yaah kujua kusimamia mipaka kati ya familia yenu na yako.
Ukichemka hapa ndio shida huanzia. Na ukikuta mama kichefu chefu basi ndoa itapata shida sana.
Na Ndoa ikishaingiliwa ivyo kudumu ni ngumu
 
Yani wewe Umesikia tu unampiga makofi... Kuna sister alikuwa anapigiwa simu kabisaa anaambiwa ni mgumbaaa ila Sema alikuja kujifunguaaa
❤️Umeona,subra yavuta kheri
 
ah mie sina utani aisee nilimwambia mke wangu toka mwanzo kuwa fanya yote mabaya lakini mama usimguse. atakae ondoka ni wewe na sio huyu mama maana bila yeye wewe usingenitaka. so respect her.
mke naweza badilisha anytime, ila mama siwezi.
Lini umeoa [emoji23]
 
Alafu analalamikia mwanamke ukute mwanaume ndio ana shida sijui ataweka wapi uso wake. Wakwe wengi ni vichomi na hasira zangu hizi Mungu anisaidie kwakweli.
Wanawake ampendani kesho nawe utakuwa mama mkwe,ndo utajua mtoto akui.
 
Wanawake ampendani kesho nawe utakuwa mama mkwe,ndo utajua mtoto akui.
Aah wanawake sisi Mungu atusaidie tu. Ila upuuzi wa kusumbua mtu eti kisa hazai huo ndio siwezi kumfanyia mtoto wa mtu sababu kuzaa ni majaaliwa. Vipi kama mwanae ndio angekua wa kike angeshauri aachike? Upuuzi tu wa huyo mama.
 
Ni tukio limetokea jana jioni hapa uyole. Ndoa ina miaka mitatu mke hajabahatika kushika ujauzito. Sasa mama mtu alikuwa anapiga kelele juu ya hilo. Nataka mjukuu nataka mjukuu, mnataka nife sijaona wajukuu na kadhalika.

Ni mama mkwe hivo binti akawa hana la kusema zaidi ya tutapata mama na mume kumwambia mama yake kuwa na subra. Nadhani huyu mama aliona kelele za mbali hazifanyi kazi, akamwomba mwanae amtumie nauli aje awasalimie hivo akasafiri na tangu mwezi wa 6 yupo pale nadhani alikuwa anataka ashuhudie tumbo likinyanyuka akiwa pale pale.

Sasa kisa cha ugomvi ni nini? Unaambiwa tangu afike ni kelele hizohizo, sasa jana binti kamfuma mama anamwambia mwanae "Au uoe mke mwingine mwanangu?" Binti hakutaka kupepesa akamrukia mama na kumpa mabanzi ya mashavu ya maana. Mama kizunguzungu chali.

Mwenye mama kaghadhibika kamrukia mke. Kwanini unanipigia mama yangu wakati mimi nakuvumilia na maneno mengi mengi. Ndio hivo ugomvi ukawa ugomvi mpaka majirani kwenda kuamria.
Una miaka kumi na ngapi?
 
Aah wanawake sisi Mungu atusaidie tu. Ila upuuzi wa kusumbua mtu eti kisa hazai huo ndio siwezi kumfanyia mtoto wa mtu sababu kuzaa ni majaaliwa. Vipi kama mwanae ndio angekua wa kike angeshauri aachike? Upuuzi tu wa huyo mama.
Si ndo hapo.
 
Back
Top Bottom