Je, ni kitu gani ambacho hakina kasoro kabisa duniani?

Je, ni kitu gani ambacho hakina kasoro kabisa duniani?

Natafuta kitu ambacho hakina kasoro hapa duniani, kitu kikamilifu kwa 100% kitu ambacho huwezi kukuta mawaa ndani yake.

Nimeangalia kama dini, zote zinamapungufu ndani yake.

Kama ni elimu zote zina mapungufu ndani yake, zimekosa majibu mengi.

Kama ni sera za vyama, sera za vuama vyote vimejaa mapungufu

Kama ni kazi za sanaa, zote zina kasoro.
Ni Mungu peke yake tu
 
Yesu ana kasoro.

Aliwachia nguruwe wasio na kosa waangukie ziwani na kufa.

Angekuwa anaishi leo watu wa PETA (People for the Ethical Treatment of Animals) wangemshitaki kwa ukatili wake dhidi ya wanyama.
Huamini uwepo wa Mungu lakini unaamini uwepo wa Yesu, yani huli nyama ilihali unakunywa mchuzi au supu ya nyama.

Duniani wajinga hawawezi kuisha kamwe [emoji38]
 
uran imejaa contradictions zinazoonesha mapungufu ya Uislam.
Tangu Jana nimekwambia weka contradictions,hujaweka imebaki kuimba pambio la contradictions
 
Jua halina kasoro, ni chanzo cha maisha duniani.
Jua linateketea kama kuni inayochoma moto, katika mchakato wa nuclear fusion.

Na katika miaka bilionin 5 ijayo litaanza kufa, na kabla ya miaka bilionin10 ijayo litazimika nankufa na kutoka nje ya Milky Way Galaxy.

Pia lina sunspots, lina mawaa, halipo perfect, lina kasoro kibao sehemu nyingine zina joto zaidi ya nyingine.
 
Hebu tueleze Quran inaelezea nini kuhusu kuzama kwa jua.
Hilo limeelezwa Sana labda Kama si mfuatiliaji,na halina uhusiano na contradictions...labda Kama hujui maana ya contradictions
 
Hilo limeelezwa Sana labda Kama si mfuatiliaji,na halina uhusiano na contradictions...labda Kama hujui maana ya contradictions
Hebu nipe summary. Maana hapa tunaongelea kasoro. Wewe umesema Quran haina kasoro.
 
Je, mapungufu yana upungufu katika upungufu wake? Kwa sababu mapungufu hayajakamilika?

Hivyo, je, kwa kuwa hayajakamilika katika kukamilika, yamekamilika katika upungufu wake?

Au, hayajakamilika hata kwenye upungufu, kwa kuwa yangekamilika kwenye upungufu yasingekuwapo na yasingejulikana kuwa ni mapungufu?

Ukifikiria sana utaona, kitu ambacho hakina mapungufu hakipo. Kipo, lakini, kuwapo kwake kuna maana hakipo.

Kitu hicho ni nothingness, nothingness ni kutokuwepo chochote, hata vacuum in space si nothingness, kwa sababu ina space. Nothingness yenyewe hata space haina. Haina space, haipo kwenye time. Haipo. Inafikirika tu.

Hiyo nothingness haipo. Kwa kuwa kuwapo kwake ni kutokuwapo.Ikiweza kuwapo nje ya hapo tu, inakuwa si nothingness tena.

Hiyo dhana ya nothingness, kinadharia, ndiyo haina makosa. Kwa sababu ina lowet entropy, hauwezi kupunguza entropy hapo. Huwezi kuharibu, ili uharibu, inabidi uitoe kwenye nothingness.

Hiyo nothingness ndiyo haina mapungufu.

Kitabu cha kusoma ni "Why Does The World Exist: An Existential Detective Story" cha Jim Holt.
Ungesema kwa kifupi kwamba upungufu na ukamilifu havipo isipokua mahitaji ndiyo huviumba kungekua na shida gani?
 
Jua linateketea kama kuni inayochoma moto, katika mchakato wa nuclear fusion.

Na katika miaka bilionin 5 ijayo litaanza kufa, na kabla ya miaka bilionin10 ijayo litazimika nankufa na kutoka nje ya Milky Way Galaxy.

Pia lina sunspots, lina mawaa, halipo perfect, lina kasoro kibao sehemu nyingine zina joto zaidi ya nyingine.
Kuna chombo chochote kilichotumwa kwenye jua,au ni nadharia tu ulizoamua kuzibugia Kama dawa!?
 
Huamini uwepo wa Mungu lakini unaamini uwepo wa Yesu, yani huli nyama ilihali unakunywa mchuzi au supu ya nyama.

Duniani wajinga hawawezi kuisha kamwe [emoji38]
Mkuu,

Kwani watu wote wanaokubali Yesu alikuwepo wanakubali alikuwa Mungu?

Mbona Wayahudi wenyewe ambao wamemuona Yesu tangu anazaliwa hawakubali kwamba ni Mungu?

Mbona Waislamu hawakubali kwamba Yesu ni Mungu?

Mbona Mrumi Tacitus kamuandika Yesu katika historia, lakini hakuamini kwamba Yesu ni Mungu?

Ushawahi kumsoma Tacitus?

Hoja yako haina mantiki, umefanya kama vile kukubali Yesu alikuwepo ni lazima ukubali Yesu ni Mungu.

Logical non sequitur.
 
Hebu nipe summary. Maana hapa tunaongelea kasoro. Wewe umesema Quran haina kasoro.
Ukiwa pwani ya Cameroon jua huzama baharini,ukiwa coco beach jua huchomoza baharini,ukiwa kwenye huo mji wenye ziwa la tope aliofika huyo msafiri,jua huzama kwenye ziwa la tope
 
Ukiwa pwani ya Cameroon jua huzama baharini,ukiwa coco beach jua huchomoza baharini,ukiwa kwenye huo mji wenye ziwa la tope aliofika huyo msafiri,jua huzama kwenye ziwa la tope
Ndio Quran inasema hivyo? Huoni hiyo ndiyo kasoro?
 
Ungesema kwa kifupi kwamba upungufu na ukamilifu havipo isipokua mahitaji ndiyo huviumba kungekua na shida gani?
Sikutaka kusema hilo, wala hata hujaelewa nilichoandika.

Unanilazimisha niandike unavyotaka wewe, wakati umeandika kitu tofauti na nilichoandika mimi.

Usinilazimishe kuandika unavyotaka wewe.

Hususan kama hata hujaelewa nilichoandika.
 
Utaandika tu utake usitake
 
Ndiyo maana nilisema limeshaelezwa Sana,ukataka summary...unaleta mdahalo,tafuta wa kufanya nae mdahalo
Hapa tupo kwenye kuongelea kasoro. Huoni hayo uliyoyaeleza kuhusu Quran tukufu ni kasoro zinapingana na uhalisia?
 
Back
Top Bottom