Je, ni kitu gani ambacho hakina kasoro kabisa duniani?

Je, ni kitu gani ambacho hakina kasoro kabisa duniani?

Alikuwa binadamu kweli na Mungu kweli.
100% UBINADAMU
100% UUNGU.

UBINADAMU WA YESU.
- kuzaliwa.
-Njaa.
-Matusi.
-Vurugu Hekaluni.
-Kupotea Katika ukuaji.
-Kupitiwa na usingizi wakati chombo kikizama.
- kupigwa kufa nk.....

UUNGU WA YESU.
-Kupata mimba kwa uwezo wa Roho mtakatifu
- kufufua wafu.
-Miujiza mingi vipofu chakula nk.
  • Kutembea Juu ya Maji.
  • Kujibadirisha Mlimani.
  • Kufufuka Katika wafu.
  • Dunia Nzima kulikiri jina lake kama ni Mokozi wa Ulimwengu.
  • mwana falsafa no 1 Duniani.
NENO
-
Hivi haya yanahusiana vp na maada husika
 
Kuna Wabongo wengi hawajui kupingana kwa hoja, ukimpinga hoja yake anaona kama umemshambulia yeye binafsi.

Kibaya zaidi, anaacha kukujibu kwa kupinga hoja zako, anakushambulia wewe kama mtu (ad hominem attack). Hii ni daliki ya kukosa hoja.

Mimi siogopi kuambiwa mbishi. Hakuna maendeleo ya fikra bila ubishi.

Watu waliotengeneza computers, internet na email walifanya ubishi kubishia barua za kawaida na typewriters.

Wengine wakafanya ubishi wakaweka internet kwenye cellphone.

Usiseme Kiranga mbishi, onesha ubishi wake una kasoro gani? Hoja zake zina mantiki au hazina mantiki?

Kwa sababu, mtu anaweza kuwa anakukubalia kila kitu tu, hana ubishi, halafu hana mantiki. Mnakubaliana ujinga tu.

Halafu anayekuletea ubishi ndiye anayeleta mantiki nzuri.

Tusikubali kwamba ubishi kama ubishi tu ni kitu kibaya.

Hata Galileo alipoiambia dunia kwamba dunia inazunguka jua, jua halizunguki dunia, alionekana mbishi.

Leo watu wamekubali, mpaka kanisa lililompinga limeomba msamaha na kusema yule tulimuona mbishi, lakini alikuwa na akiki kubwa iliyokuwa mbali sana kiasi miaka ile hatukumuelewa.

Sasa hapa pia inawezekana naonekana mbishi kwa sababu watu hawaelewi vitu vingi tu kama unavyosema.

Vitu vyenyewe basic tu, basi tu watu wetu wengi wako nyuma sana.
Hapo kwenye kusimamia hoja ndio tatizo kubwa lilipo.

Mara nyingi unaandika vitu vikubwa sana mkuu sasa kwa mtu ambae anaandika ela badala ya hela au ludi badala ya rudi watakaokuja kukuelewa labda kizazi chake ila sio yeye.

Hata hivyo napenda vile unajitahidi kuitoa jamii gizani.
 
Natafuta kitu ambacho hakina kasoro hapa duniani, kitu kikamilifu kwa 100% kitu ambacho huwezi kukuta mawaa ndani yake.

Nimeangalia kama dini, zote zinamapungufu ndani yake.

Kama ni elimu zote zina mapungufu ndani yake, zimekosa majibu mengi.

Kama ni sera za vyama, sera za vuama vyote vimejaa mapungufu

Kama ni kazi za sanaa, zote zina kasoro.
Space
 
Oh kipimo cha kupima efficiency ya kitu kuwa ni 100% je na chenyewe kinapimwa au hakipimwi?
Yaani kinapimwa efficiency yake ya kupima kama ni 100%?
Kinapimwa, lakini kwa kasoro pia, hapo juu nimesema hakuna kisicho na kasoro.

Yani ni kwamba hata kitendo cha kupima kasoro kinaleta kasoro, kusoma ujue kuna kasoro au hakuna kasoro uta disturb unachopima at some level, na kipimo chako kitaleta kasoro.

Kisicho na kasoro ni nothingness, ambayo haipo, kwa sababu ikiwepo tu inakuwa si nothingness tena.

Kwa hivyo hakuna kisicho na kasoro.
 
Kinapimwa, lakini kwa kasoro pia, hapo juu nimesema hakuna kisicho na kasoro.

Kisicho na kasoro ni nothingness, ambayo haipo, kwa sababu ikiwepo tu inakuwa si nothingness tena.

Kwa hivyo hakuna kisicho na kasoro.
Kama kasoro ni nothingness maana yake kasoro imetungwa na kundi fulani? Kusema kuwa hakuna kitu ambacho hakina kasoro na huku unasema kuwa kasoro ni nothingness huoni kuwa unajichanganya?
 
Natafuta kitu ambacho hakina kasoro hapa duniani, kitu kikamilifu kwa 100% kitu ambacho huwezi kukuta mawaa ndani yake.

Nimeangalia kama dini, zote zinamapungufu ndani yake.

Kama ni elimu zote zina mapungufu ndani yake, zimekosa majibu mengi.

Kama ni sera za vyama, sera za vuama vyote vimejaa mapungufu

Kama ni kazi za sanaa, zote zina kasoro.
Kila unachokijua we basi akijakamilika

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mwanadamu pia ana kasoro hivyo baadhi ya vitu vipo katika ukamilifu wake lkn kutokana na udhaifu wa mwanadamu hatouona ukamilifu wake

[emoji124][emoji124][emoji124]
 
Mwanadamu pia ana kasoro hivyo baadhi ya vitu vipo katika ukamilifu wake lkn kutokana na udhaifu wa mwanadamu hatouona ukamilifu wake

[emoji124][emoji124][emoji124]
Basi hivyo vitu upungufu wake ni kutoonekana ukamilifu wake.
 
Kama kasoro ni nothingness maana yake kasoro imetungwa na kundi fulani? Kusema kuwa hakuna kitu ambacho hakina kasoro na huku unasema kuwa kasoro ni nothingness huoni kuwa unajichanganya?
Sijasema kasoro ni nothingness.

Ninasema kitu pekee kinachoweza kuwa hakina kasoro, katika dhana (maana hakipo katika uhalisia) ni nothingness.

Nothingness haina kasoro.

Kwa sababu, ili iwe na kasoro, inabidi iwepo.

Na yenyewe haipo.

Hivyo haiwezi kuwa na kasoro.

Halafu katika fizikia, nothingness has the lowest possible entropy. Katika fizikia kasoro inaendana na kuongezeka kwa entropy (second law of thermodynamics).

Hivyo lowest possible entropy = nothingness = perfection.
 
Back
Top Bottom