Je, ni kitu gani ambacho hakina kasoro kabisa duniani?

Wewe hata hujuinunataka kusema nini.

Unanilazimisha kwamba nitaandika unavyotaka wewe?

Nitaandika lini? Weka tarehe na saa hapa turejee.
Ukilazimishwa si utatapika.
Jua tu kuwa utaandika si kwa kulazimishwa bali kwa kulazimika.
Hayo mambo ya kuweeka tarehe na saa ni kama ule utoto wa kusema tupinge.
 
Hivi jua lilianza wakati wa "big bang?" Maadamu hakuna anaejua huenda hiyo miaka bilioni 5 uliyosema imeshapita na bado jua linapeta tu. Kuna wakati nafikiria huenda ndio Mungu mwenyewe. Angalia mimea na vitu vyote vyenye uhai vinavyopiga magoti kwa jua! Angalia ukijani wa mimea unavyopendeza! "I love you sun".
 
Kifo kina kasoro ndiyo maana kimeshindwa kuua watu wote kwa pamoja.

Kinavizia mmoja mmoja.

Kimeshindwa kufanya kazi yake kinyambisi.
Una uhakika gani kuwa kinamvizia mmoja mmoja, ikiwa aliyekiratibu ndivyo alivyoona kinampasa kutenda hivyo we ni nani hadi ukikatalie hakina ukamilifu?
 

Kimsingi hivyo vyote ulivyovitaja vinasimamiwa na binadamu na binadamu wote tuna mapungufu au kasoro kama nne hivi.
1. Hatuna hisia sahihi
2. Tunatenda makosa kwa kukusudia au kutokukusudia
3. Tunasema uongo
4. Tunaambiwa uongo
 
Kuna chombo chochote kilichotumwa kwenye jua,au ni nadharia tu ulizoamua kuzibugia Kama dawa!?
Kwani wewe ulipo kuna chombo chochote umekituma hapa nilipo ili ujue nipo?

Au unanijibu kwa nadharia tu?

Ushawahi kusikia Hubbke Telescope, James Webb Telescope, Spitzer Telescope, SOHO, STEREO, SDO?

Au hayo majina ni "mashikolo mageni" ndiyo unayasikia leo?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…