Waamini wa Quran wanaamini kwamba Quran ndio kitabu cha mwisho cha mwenyezi Mungu kwa watu hapa Duniani, kwamba Quran ni updated version ya Biblia.
Naam, Qur'an ni kitabu cha mwisho katika vitabu walivyopewa Mitume wa Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake wa mwisho Muhammad (swala na salaam ziwe juu yake.)
Lakini Qur'an sio updated version ya Biblia. Na fahamu pia hakuna kitabu kinaitwa Biblia kilichoshushwa kwa Mtume yeyote.
Kama unakusudia kitabu alichopewa Yesu kama muongozo kwa watu wake basi kitabu chake kinaitwa Injili. Na cha Nabii Mussa kinaitwa Taurat.
Kwa msingi huo tukifuata mtiririko wa Vitabu vya Mungu, kuna agano la kale, agano jipya na Quran.
Miongoni mwa vitabu vilivyoshushwa kwa Mitume kama miongozo kwa watu ni pamoja na Zaburi kwa Nabii Daud, Taurat kwa Nabii Mussa, Injili kwa Nabii Isa (ninyi mnamwita Yesu), Qur'an kwa Mtume Muhammad.
Hakuna kitabu kilichoshushwa kwa mtume yeyote kinachoitwa Agano jipya au Agano la zamani.
Ukisoma Agano la kale, hakuna concrete promise ambayo mungu aliitoa kwa watu watakaokufa na kwenda mbinguni,
Hakuna kitabu kilicholetwa kwa mitume ambacho hakijatoa maelezo kwa watu kwamba nini kitatokea ikiwa wataasi uongozo au nini kitatokea ikiwa wanafanyia kazi miongozo.
maelekezo mengi yalikua centred kwa waisraeli na makabila yake, ni ahadi za mungu exclusively kwa waisraeli. Ahadi nyingine ilikua ni ujio wa masia.
Naam, mitume wote akiwemo Mussa, Yesu na wengineo kabla yao walitumwa kwa watu maalum.
Isipokuwa Mtume Muhammad ambaye ndio mwisho wa Mitume amatumwa kwa wanadamu wote. Na hiyo ni miongoni mwa tofauti iliyopo kati ya Muhammad na mitume wengine waliopita kabla yake.
Pia kwenye agano la kale mungu alikua mkatili sana, mwenye hasira na asie na huruma, uki mess up umekwisha. No mercy.
Mwenyezi Mungu ni mpole na mwenye huruma kwa waja wema na ni mkali wa kuadhibu kwa wenye kuasi baada ya kubainikiwa na uongofu yaani kuonywa na Mitume kupitia vitabu walivyopewa.
Hataadhibiwa kiumbe isipokuwa mpaka Mwenyezi Mungu atume muonyaji yaani Mtume.
Agano jipya akaja Bwana Yesu, yeye mafundisho yake 99.9% yalikua centred kwenye upendo, kupendana, kuhurumiana na pia ahadi ya waumini wake kwenda Mbinguni kumuona Mungu. Kuonyesha mungu anatupenda watu wake, anatujali, tutubu, tuombe toba, nk.
Vipi kama mtu ataamua kupitia hilo uliitalo Agano jipya la Yesu asitubu, asiombe toba mwisho wake mbinguni utakiwaje?
Hapana shaka hatafanana na wale wenye kuomba toba.
Agano hili lilionyesha mungu kama aleijaa upendo, huruma na msamaha.
Daima Mwenyezi Mungu ni mwingi wa huruma na mwingi wa kusamehe kwa kila mwenye kurejea kwake kwa kuomba toba.
Mafundisho mengi kuhusu Mbinguni aliyatoa Bwana Paulo kwenye agano jipya na ahadi nyingi za mbinguni zinaongelea kuimba na kucheza na kufurahi na kufutwa machozi ya kupumzishwa na adha na madhira ya Duniani.
Kwa kifupi maelezo yako haya ni sawa na kusema ni kustarehe kama malipo ya kufuata miongozo ya Mwenyezi Mungu.
Ukija kwenye Quran, ama updated version ya Agano jipya unakutana na vituko kidogo, kwanza Mungu anaonekana yuko so frasturated, amechanganyikiwa, amevurugwa, hana huruma, hacheki na mtu na mambo kama hayo.
Hizo ni sifa za uongo unamzushia Mwenyezi Mungu. Hebu toa ushahidi katika dai lako kuwa yuko frastuated, amechanganyikiwa, hana huruma, amevurugwa.
Mbaya zaidi this time akatoa ahadi ya ngono na ulevi wa kupindukia huko mbinguni. Kwamba mbingu itakua imejaa madanguro na mito ya pombe, ni ulevi na kupigana miti tu.
Miongoni mwa starehe kubwa kabisa kwa viumbe wanadamu, wanyama hata wadudu ni tendo la ngono.
Unaona ajabu kusikia kuwa huko Peponi miongoni mwa starehe ni wanaume kuozeshwa wanawake wazuri wazuri, lakini huoni ajabu kwamba hilo tendo la ngono ni starehe kubwa hapa duniani?
Je, mungu kubadilika badilika kuhusu ahadi zake kwa binadamu ni kutokana na binadamu kutokumuelewa kwenye maagano ya zamani ama amegundua kua wanadamu wanapenda sana ngono hivyo kwenye last version yake ndio akawaahidi kua wakimtii watapewa hiyo zawadi?
Hakuna mabadiliko ya ahadi. Hata wewe ukifuata muongozo sahihi na ukawa ni wa Peponi huko utastarehe kwa kila aina ya starehe ambazo jicho halijapata kuona, sikio halijapata kusikia na moyo haujapata kuwaza namna uzuri ulivyo.