China kwa chip bado wako nyuma kidogo lakini they are coming maana kilichotokea kama week mbili zilizopita na HUAWEI kimewaacha mabeberu na kizunguzungu, wanachotaka solve kikubwa ni machine za kuzalisha hizo chip kama zile za mdachi ASML ambazo kapigwa ban, they working day and night najua watazipata tuu maana nasikia research stage wameshavuka wanamalizia puzzles zilizobaki, Historia haiko upande wa mabeberu walishafnay huu upuuzi ili kumrudisha nyuma China lakini walipigwa na kitu kizito sana, mfano China alipigwa ban na kunyimwa kabisa technology ya GPS waliingia kazini wakaja na BeiDou kitu superior kuliko GPS, vile vile walipigwa ban space station walichofanya wakaja na ya kwao ambayo ni very modern na superior kuliko ya mabeberu, nuclear walifanya the same miaka ya 60 maana walijua bila nuclear wangeteseka tuu na kupewa order, sasa hivi wana hypersonic ambayo beberu hana na inawafanya Pentagon wasipate usingizi maana unaweza kushtukia iko mlangoni , wachina achana nao ni watu wanjua kuweka focus sana kwenye kitu wanachotaka, nimesoma nao na kule nyumbani ni kama wale washikaji wana akili sana na wanasoma usiku kucha bado, faculty zote za vyuo vikuu vya maana US kama Havard, Princeton, Yale etc kwenye masomo ya science, medicine,Engineering etc wamejaa wachina vibaya sana, hawa watu itakuwa ngumu sana kushindana nao, ila ninachoogopa ni ule ukomunisti wao maana naona kuna siku tutalazimishwa kuongea kichina dunia nzima
Wengi hawajui, wachina wana long term thinking, aina hii ya kupanga na kufikiria ni sehemu ya tamaduni yao kwa mda mrefu kiasi kwamba huwa wanafikiria hivyo by default
So hakuna wasichoweza kamilisha wakiamua kuweka jitihada, huwa nawashangaa watu wanaoyoifananisha Marekani na China.
Ukisoma Historia yao, kwa Maelfu na maelfu ya miaka Wachina walikua vinara kwenye biashara, teknolojia na uvumbuzi, ni karne ya 20 tu ndipo China ilipoanguka kwa kushindwa ku industrialized, hii tunachokiona sasa hivi ni China kurudi kwenye nafasi yake...
U.S ina miaka 200 tu na inaelekea ku collapse
China ni underrated sana, miaka ya 60 tu hapo, ilikua haina tofauti na nchi nyingi za Africa.
Kuhusu "hofu" yako, China sio imperial nation kama U.S na nchi nyingi za ulaya Magharibi, in fact ni nchi tu za Ulaya Magharibi na U.S zenye itikadi hii, Uchumi wao na standard of living ime base kwenye hio Mindset
China ina miaka zaidi ya 5000 kama taifa, sidhani kama iliwahi ku invade taifa jingine, mara nyingi huwa ni watu wa kujifungia
Wakati wazungu wapo kwenye dark age, Mchina kashagundua karatasi, gun powder, dira pamoja na meli kubwa
Anasafiri kufanya biashara, wazungu walikuja kutumia hivyo hivyo vitu baadae na vi meli vyao vidogo wakafanya uovu dunia nzima
Pia u communism ni aina ya ku organize working places, kinyume cha capitalism, sio aina ya ukoloni