Dodoma bado ina safari ndefu kufikia mwanza, dodoma itakuwa ni mji uliopangwa vizuri, dodoma itaipita mbeya na Tanga ila kwa Arusha na Mwanza bado sana.
Ukiondoa miradi ya ujenzi wa wizara miradi iliyobaki karibu yote ipo mza tena mingine ni mikubwa kuliko ya Dom.
Soko la mwanza litakuwa kubwa karibu mara 3 ya soko la Ndugai.
Ukiacha hilo mwanza ina masoko mengine makubwa kama soko la samaki kirumba, kirumba pia kutajengwa soko jingine, mkuyuni kutakuwa na soko pia, buzuruga ilipo stendi ya mabasi kutajengwa buzuruga complex.
Mwanza ina stendi 2 za mabasi.
Barabara naona serikali imeanza kuona aibu, city centre to usagara upembuzi tayari hii itakuwa 25km dual carriageway.
City Centre kisesa upembuzi unaendelea almost 20+km njia 4.
Barabara ndogondogo zinajengwa nyingi tu.
Airport, serikali inataka kujenga jengo kubwa sawa na terminal 2 ya Dar hapa mwanza.
SGR inakuja mwanza pia, jengo la stesheni ya mwanza linaweza kuwa kubwa na zuri kwa sababu ya location.
Kwa hoteli Dom bado sana.
Karibu kila chuo Tz kimeshika eneo kubwa mza,
Kwa Leo inatosha