passion_amo1
JF-Expert Member
- Dec 3, 2023
- 1,828
- 3,922
Mohamed,Any way mi hoja yangu ni NI MAGAIDI WENYEWE WANAJIFUNGAMANISHA, NI WAISLAM WENYEWE WANAJIFUNGANISHA NA UGAIDI KUWA KWAO NI IBADA NA UISLAM AU WAANDISHI WA HABARI NDIO WANAOFUNGAMANISHA UISLAM NA UGAIDI
hoja yako ni nzuri. Ila Mimi ninapenda uislamu jinsi unavyokemea vitu, kama vile masuala ya ushoga, kutania haswa vinavyohusu masuala ya dini yao.
Huenda waandishi wanawafunganisha waislamu na magaidi au uislamu unajifunganisha na ugaidi.
Mwaka 2006 gazeti la jyllands posten nchini Denmark, lilichapisha katuni zenye michoro 12. Maimamu wawili waliopewa Makazi nchini humo kwa kukimbia nchi zao, wakiongozwa na Imam Ahmed akkari walianza kuzunguka nchi za kiislamu wakiomba kuungwa mkono na kuonyesha kile kilichochorwa katika gazeti huku vingine vikiwa vimeongezwa kukionekana kuna picha ya mtu mwenye ndevu nyingi akiwa na pua kama ya nguruwe.
Baada ya picha ile kusambaa maimamu walikuwa wakisema gazeti lile linaendeshwa na serikali ya denmark, hivyo wajitokeze kuomba msamaha. Serikali iligoma na kukanusha sababu Hawakuona kosa.
Kilochofata baada ya hapo, chuki ile ikasambaa makanisa yakanza kuchomwa, waandamanaji kutoka pakistan na indonesia wakachoma moto bendera ya Denmark wakaharibu makazi ya wakristo na makanisa.
Lakini baadae ikaja fahamika picha ile yenye mfanano na nguruwe ilikuwa ni kwa ajili ya mashidano yaliyokuwa yakiadaliwa.
Huko Nigeria wakristo walichomwa moto pamoja na jumbe zilizosema “Butcher those who mock islam” “behead those who say Islam is violent religion”
Haya ndio yaliyotokea lakini mwaka 2013 imam ahmed akkari alikuja kuomba msamaha akitambua umuhimu wa free speech.
Ndio maana nikasema hoja yako inaweza kuwa sahihi, lakini hatujawahi kusikia kupingwa kwa nguvu kwa hawa wanaojihusisha na ugaidi kwa mgongo wa uislamu.