Je, ni mfuko gani wa UTT AMIS uko vizuri zaidi?

Thamani ya hisa inaongezeka pia
 
Nikiweka kwenye umoja ama bond nitavuna laki laki hiyo hiyo? Na maana kwamba kati ya mifuko yao upi unaasilimia kubwa zaidi?
 
Nawashuku sana wakuu mbarikiwe sana nyote mliojitoa kuchangia kwenye huu uzi ni madini madini tupu, mfuko huu ni mzuri kwa vijana Kwa mfano ukifanya uwekezaji sasa miaka 10 ijayo na kuendelea unajikuta umri umeenda na unaukwasi wako km walivyosema wahenga fainali uzeeni. Muda ni sasa tuwekeze huko uzuri mfuko wenyewe huko chini ya serikali ni sehemu sahihi.
 
Yan nmesoma mwanzo mwisho txt kalbia 250+...
Sas n muda wangu [emoji1320]

Mwanzo niliona kwa Mh Kigwangala alizungumzka hii issue ya UTT kupitia Twitter na nikaifatilia na baadae mpaka nikaenda CRDB...ingawa bado sikuelewa km nilivyo elewa leo hii

Yan uzi umechambliwa vzr sanaa ukiwa Na experience ndan yakeee

Yan kila kitu kimechambuliwa kutoka kweny nn maana aya UTT.

Jinc ya kununua vipande na mpapa sas namna ya
Faida na ongezeko la faida kwa sku aiseee [emoji120][emoji120]


Na kaka ulie kama kiongoz ubalikiwe sanaaaa
 
Je unaweza kuweka kila mwezi au ukiweka mara moja basi
Unaweka hela muda wowote siku yoyote kiasi chochote kuanzia sh. 10,000. Tumia simu airtel money, tigo pesa, mpesa au nenda tawi lolote la crdb. Crdb ni mawakala wa utt. Sio lazima uende ofisi za utt. Maliza kila kitu kidigitali. Tumechelewa mno. Wahindi wabazijua saba hizi mavitu ya mutual fund, forex etc.
 
Mkuu, Mimi naomba nisaidie kujua namna ya kujiunga hasa nikiwa mbali na ofisi zao.
Nenda tawi lolote crdb karibu yako. Jaza form. Pia tumia simu LIPA BILL. chagua UTT. endelea na steps zinazifuata. Tunechelewa mno....wahindi wanazijua hizi issue za Forex, mutual fund long time!! Umejua sasa wajulishe na ndugu, jamaa na marafiki!!!
 
Weka Bond Fund. UTAKULA HELA ACHA KABISA. SAFETY/SECURITY 100%
 
Mimi nimewekeza Umoja, nikifikisha kiasi fulani cha pesa nitawekeza kwenye Bond.Nakumbuka kuna mdau alisema unaweza kubadilisha mfuko.
Kubadilisha inaruhusiwa lakini huwezi toka umoja kwenda bond fund. Kwa nini? Kwa sababu UTT hela zilizochangwa kwenye mifuko hiyo wanaiwekeza katika sehemu tofauti.
Unaweza kuhama toka liquid kwenda bond. Au bond kwenda liquid.
Watoto(umri ukizingatiwa) kwenda umoja.
 
Naona kama kikundi cha watu flani wanachati
Mmoja anauliza,mmoja anajibu..anyway
I hope this isn’t a scam !

Guy’s be careful with your money!
Only Place i can trust is a bank only.
Hakuna faida rahisi rahisi duniani hapa
UTT AMIS ni taasisi ya Serikali ya Jamuhuri ya Tanzania chini ya wizara ya Fedha. Ofisi zao zipo. Mawakala wao wapo(CRDB). Pia wakati wa maonesho ya sabasaba ukipata muda tembelea banda lacwizara ya fedha humo ndani utakutana na taasisi zote za hiyo wizara ikiwemo UTT. Ni kweli ni vizuri kuwa muangalifu.
 
Kiuhalisia unaweza kuswitch kutoka mfuko wowote kwenda mwingine. Kinachofanyika ni utt kununua vipande vyako vote vya mfuko unaouacha, ila fedha hizo badala ya kukupatia wanakununulia mfuko unaotaka kuhamia. Haya yanafanywa automatic na utt mara baada ya mteja kutaka switching.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…