Je, ni mfuko gani wa UTT AMIS uko vizuri zaidi?

Nashukuru sana wadau wote mliochangia hapa. Nimepata Elimu niliyokuwa naitafuta kwa muda mrefu. Jamii forum ni jukwaa muhimu sana. Maxce mello uliyepata wazo la kuanzisha jamii forums barikiwa sana.

Soon naenda kuwa mwekezaji wa uttt baada ya biashara kadhaa nilizojaribu kwa kupata abcs humu humu kugundua haziendani na Mim.

Nadhani jamii forums inabidi ianze kupata ruzuku serikalini (just kidding) maana ni msaada mkubwa kwa wanaoitumia vizuri
 
Kuwekeza hela ndogo kwa return ya 13 kwa mwaka haifai.
Mimi kwa uelewa wangu watu wanafanya diversification kuminimize risks, si vema ukawa na biashara moja unatakiwa kuwa na biashara kuanzia nne nakuendelea nyingi zikiwa na indirect involvement. Sasa hapo unainvest kwenye financial sector Kama vile UTT , bonds, stocks etc, unawekeza kwenye real estate kidogo, ukiweza transpot kidogo nk Ukifuatilia mijadala ya wenzetu huko QUORA nilichokuja kugundua wenzetu wametuacha mbali sana, si kwamba sisi hatuna mitaji hapana, hatujeza kutumia akili sawasawa ili kuweza kutoka kimaisha.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ndugu wapendwa nina swal
Kwa mfano ukaweka 100k kwa mwez kuptia UMOJA fund...it means mwez unaofata unapata 1% ya hyo pesa

Sas ukaweka tena 100k mwez wa 2 jumla ikawa 200k na ile ya nyuma
So utapata tena 1% ya hyo lak2 c ndio ??

Au utaendelea pata 1% ya ile lak100 ya ulio anzia kuweka???
 
Mwezi unaofata Utapata ya 200k, na ukiongeza nayo inakuwa ya total uliyowekeza
 
Mkuu elezea kuhusu faida inavyokuwa.. Mfano nimenuanua kipate kwa sh 817.. nikanunua viaonde vya million 40, inamana nitanunua vipande 49,000. sasa kwa mwaka wamemsema unapata faida ya sh 12 kw kipande.. Nikajiuliza inamaana faida ya kuwekeza kwa mwaka ni sh 12 kwa kipande X 49000= inamaan nitapata gawio la sh 588,000 Tsh. Jamani si nihasara kubwa sana au sijaelewa. nakama sijaelewa naomba mtu afafanue jinsi mtu aaye nununa vipande anavyopata faida?
Asante
 
Hata Kutoka Umoja kwenda bond au Liquid pia inawezekana
 
Sidhani kama mahesabu yako sawa.
 
Mkuu hiyo bond , gawio la mwezi linaingia kwenye simu au Hadi muanze kupanga folen
 
Share basi kitu ulichochambuliwa
 
MFANO WEWE ULIONA NI MFUKO GNAI BORA KAMA UNA 40 mILLION?
 
Basi huu Ni ujinga kwanini Wasiseti kama nataka malipo Kwa mwezi iwe inaingia automatically.

Yani hela ni hela yangu Hadi kila mwez niwe narequest tena hela itoke Kwa Siku 10 tena za kazi !
 
Basi huu Ni ujinga kwanini Wasiseti kama nataka malipo Kwa mwezi iwe inaingia automatically.

Yani hela ni hela yangu Hadi kila mwez niwe narequest tena hela itoke Kwa Siku 10 tena za kazi !

Kuna taasisi nyingine za kifedha, mfano bank ya Crdb ukiweka pesa wao malipo yanaingia kwenye account yako automatic kulingana na time scale utakayokuwa umechagua mwenyewe.

Wameanzisha mfuko unaitwa Mzigo Flex ambao wanatoa riba ya 9% kwa mwaka na pesa lazima iwe fixed kwa mda wa miaka 3.

Kama hutaki usumbufu huu wa utt-amis unaweza kuwekeza CRDB kwa riba hiyo ya 9% (binafsi sioni shida kwani kama pesa nataka iwe inaingia kwenye account kila tr1 basi kila tr 20 unafanya request)
 
Nina swali fikirishi wakuu,mfano nina milioni 10,nikaenda bank kukopa milioni 30,jumla nikawa na millioni 40......hii hela nikienda kuiweka UTT je faida ntakayopata si itakuwa sawa na makato nayokatwa bank? Ninachowaza gawio la UTT linilipie mkopo bank.
 

Rafiki yangu clinician hilo wazo linaonekana zurj hata hivyo kwa bahati mbaya sana “mathematics” haitakubali.
Kwanza kabla ya kufanya hivyo ni lazima ujiridhishe na haya machache;
a) Bank utatakiwa kulipa pesa hiyo kwa riba kiasi gani- kumbuka UTT wanatoa riba ya 1% ya pesa yako kwa mwezi.
b) Lazima ujue mkopo huo utatakiwa kuulipa kwa mda gani.
Sina uhakika kama Tanzania bara kuna bank ambayo riba ya mkopo ni chini ya 1%- kama inawezekana basi unaweza kuchukua mkopo bank na kuweka utt ili wao wakulipie, sina uhakika na hilo hata kidogo otherwise, kila mtu angekuwa anafanya hivyo.
 
Nashukuru kaka kwa shauri lako,nilitegemea faida ya UTT isitoshe kurejesha makato ya mkopo,ndio maana nikaona niongezee niongezee hela yangu cash ili kuziba hilo gap..Lakini nadhan bila details za mkopo ni ngumu kujadili kwa kina.Nitarejea ndugu yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…