Huu uzi nimeupitia page ya kwanza hadi ya mwisho.
Niseme kwamba JF kwa TZ ndo sehemu sahihi ya kupata taarifa sahihi kwa Kiswahili. Nilianza kusoma km mgeni enzi ikiwa jambo forum hasa jukwaa la vichekesho, badae nikahamia jukwaa la siasa na habari mchanganyiko.
Umri ulivyozidi na kughafilishwa na siasa nikahamia jukwaa na IT badae jukwaa la magari.
Kila Jukwaa nimejifunza na kunipatia vitu sahihihi.
Sasa hivi nimehamia jukwaa hili rasmi. Nawashukru sana wadau.
Baada ya kusoma page zote nimeshawishika na mimi kuingia UTT, nina matumizi mabaya sana ya hela na sijui kuweka akiba.
Umri unakimbia na majukumu yanazidi je inawezaekana nikiwa naweza kila mwezi 1M na sina mpango wa kutoa? Baada ya miaka 2 nitakua na shilingi ngapi hasa kwa account ya Liquid?
Asanteni sana