Je, ni mfuko gani wa UTT AMIS uko vizuri zaidi?

Je, ni mfuko gani wa UTT AMIS uko vizuri zaidi?

Na ukishajaza hyo fomu ya kuuza vipande ni mpk wafanikiwe kuuza ndo upate pesa zako?? Nauliza hvi coz nina hisa za voda nilinunuaga nikaweka sokoni mpk leo mwaka wa pili hawajafanikiwa kupata wateja.
Sasa kama umeshindwa kuuza hizo hisa za VODA utapataje hizo fedha za Voda kuwekeza Huko UTT?
 
Mkuu rudia kusoma niliyoandika pengine unaweza ukaelewa kinachozungumzwa.

Umeandika ulikuwa na hisa za VODA umeziweka sokono lakini ni miaka miwili sasa hawajapata mteja wa kuzinunua!!! Sasa kama hawajapata mtu wa kuzinunua maana yake huwezi kupata cash kutokana na hizo hisa za VODA!!! Nadhani utaelewa sasa.
 
Ulikuwa ni mfano tu kwamba kuna baadhi ya secta ukiwekeza kuja kupata hela yako ni mpk hisa zako ziuzwe, bt sio utt. Mfano wake ndo ukawa voda, bt sikusema kuwa nilikuwa nategemea kuuza hizo hisa ndo niingie utt, umeelewa sasa.
 
Nauona uzi mzuri huu baada ya kumaliza kuspend 5M kwa matumizi yasiyo ya maana.
Wacha nijipange tena nijiunge japo kwa kianzio kidogo kwanza
 
Ni 10M mie nataka tu iongezeke haraka, mfuko gan unanifaa?
 
Ni 10M mie nataka tu iongezeke haraka, mfuko gan unanifaa?
Kwa maelezo ya wahusika hapa, huu mfuko wa UTT sio uwekezaji wa kuvuna haraka haraka na kwa wingi, bali uwekezaji salama usio na stress, hivyo faida huwa kidogo kidogo na pole pole.
Kwa mfano, hiyo 10ml ikiweza kuiwekeza kwenye Liquid fund, utakuwa na uhakika wa kuvuna wastani wa shilingi laki moja kila mwezi, huku pesa yako ikiwa iko salama.

Binafsi nimeanza kuuelewa fresh huu mfuko, muda sio mrefu nitajiunga, unanifaa.
 
Back
Top Bottom