Unafungua account kwenye simu na Account inakua tayari kuweka pesa hapo hapo. Hauwezi kutoa pesa kabla ya kukamilisha usajili. Kukamilisha usajili download form ya usajili, print, jaza, wasilisha tawi lolote la CRDB (CRDB ni wakala wa UTT). Kujiridhisha zaidi unaweza piga simu UTT na kuwauliza kama wamepokea form zako za kuomba usajili ulizokabidhi kwenye tawi la CRDB.
Mimi saivi nna mifuko mitatu, Wekeza Maisha, Umoja Fund na Watoto Fund ambazo zote nimefungua bila kufika ofisi za UTT, kasoro Watoto Fund ambayo yenyewe ni lazima kufika ofisini...