Je ni sahihi kijana mwenye miaka 23 kuendelea kuishi kwa wazazi wake?

Je ni sahihi kijana mwenye miaka 23 kuendelea kuishi kwa wazazi wake?

Kwa vijana wa sasa hilo ni sahihi kabisa kwao .Ila enzi zetu huo umri ulisha oa zamani na una mji wako.Kuna moja nililikuta limevaa taulo kwa baba yake halijaoa lina 33 wala halina hata aibu aisee ?
Muonyeshe Kwao Sasa,,Tofauti Na Hapo Ulipomkuta Kwa Wazazi Wake Halali,,Ili Aweze Kwenda Kuziondoa Hizo Aibu...​
 
Inategemea hususani kwa wale ambao wanasoma(Wengi katika umri huo bado unakuta wanakaa kwao ) Note:Elimu huwa inachelewesha sana vijana wengi kuanza kujitegemea permanently. Achana na yale mambo ya vijana kujirundika ghetto wakiwa masomoni(Hii mara nyingi huwa temporary).
 
Je ni sahihi kijana mwenye miaka 23 kuendelea kuishi kwa wazazi wake? Je kijana uyo atakuwa alelewa kujitegemea au kutegemea maisha yake yote??
Kijana amemaliza elimu, hana ajira, hana kipato cha uhakika, hana mtaji wa biashara, elimu aliyopata imejaa utata mtupu, hana ujuzi wala mafunzo ya kazi, n.k.!?

Sasa unategemea kijana kama huyu atakaa wapi kama siyo kwa wazazi wake mpaka ajitaffute na kupata uhakika wa maisha ya kujitegemea. Wewe unafikiri anguko la kimaadili kwa vijana waliokuwa wengi linatoka wapi!?
 
Back
Top Bottom