Je ni sahihi kijana mwenye miaka 23 kuendelea kuishi kwa wazazi wake?

Je ni sahihi kijana mwenye miaka 23 kuendelea kuishi kwa wazazi wake?

Wewe unafikiri hao wazazi wako walijizaa? Au waliomba kuzaliwa?
Wamekutunza Hadi umri unaweza kujitunza. Si jukumu lao tena kukutunza.
Hakuna aliyeomba kuzaliwa huo ndo mpangilio wa dunia.
Uyo kijana sidhani kama akili iko sawa aswaa . Unakula kwa wazazi auibu huna kweli ata kidogo tu...? Unaoga kwaiyo sabuni ikiisha anaulizia au chakula wanampakulia ikiwa si zamu yake kupika ?mmm kamwe hawezi kupata family akalea iliwajitegemee ila wawe tegemezi
 
Kwani huyo kijana si ndio mrithi wa mali zilizochumwa na wazazi wake? Kwa hiyo atoke nyumbani aende wapi kama wazazi walipanga kuwa na mtoto? 🤔
Kwa mawazo haya umaskini utakuandama Sana.
Kufikiri wazazi wafe urithi Mali ni mawazo ya kimasikini Sana.
Wazee wanadunda Hadi 90 halafu wewe Hadi 65 unasubiri urithi.
 
Kuna umri ukifika unatakiwa kujitunza mwenyewe.
Wazazi wako hawakujizaa au kwamba waliomba kuzaliwa.
Jukumu lao kukutunza Hadi 18 halafu ukatafute familia yako nawe uzae utunze watoto wako.
Basi atoke kwao aanze kukomaa na mtaa, mimi nilikuwa namsapoti tu asiteseke jua nalo ni kali mno huku nje asijeungua ngozi bure!
 
Swali halina jibu moja.

Waha hawafikishi hata 15yrs washapotea makwao hasa zile familia masikini,

Kule usukumani vijijini mtu anaoa na kupata watoto hata watatu yupo kwao kwa wazazi na akijitegemea anaoa mke wa pili anampeleka kuishi kwa wazazi wake.
 
Basi atoke kwao aanze kukomaa na mtaa, mimi nilikuwa namsopoti tu asiteseke jua nalo ni kali mno huku nje asijeungua ngozi bure!
Wewe unafikiri hao wazazi wako wasingetoka kwa wazazi wako wangeoana halafu waishi vipi na wazazi wa Nani? Wa mke au wa mumeo?
Leo hii mgekuwa mnaishi kwa bibi au babu?
 
Kawaida , mbona mimi ninaitafuta Fote bado nipo kwa mshuwa na wala hawalalamiki kwa lolote.

Kila siku mzee ananisihi kama bado sijajipanga vizuri nisiharakie kukimbia nyumbani kwenda kupanga wakati nyumbani kuna nyumba ya bure hakuna mtu wa kukaa wanaishi panya tu.

Chakula anachopika mama mara nyingi kinabakia wanamwaga kwa sababu ya upweke wa kuishi peke yao ninapokuwa nimetoka.

Wadogo zangu wote wameshaondoka nyumbani kwenda kujitegemea na kuanzisha miji yao , mimi ndiyo bado nimebakia nyumbani
 
Back
Top Bottom