Je ni sahihi kijana mwenye miaka 23 kuendelea kuishi kwa wazazi wake?

Je ni sahihi kijana mwenye miaka 23 kuendelea kuishi kwa wazazi wake?

Yesu mwenyewe mpaka saizi anaishi kwa baba yake. Sisi ni

Kawaida , mbona mimi ninaitafuta Fote bado nipo kwa mshuwa na wala hawalalamiki kwa lolote.

Kila siku mzee ananisihi kama bado sijajipanga vizuri nisiharakie kukimbia nyumbani kwenda kupanga wakati nyumbani kuna nyumba ya bure hakuna mtu wa kukaa wanaishi panya tu.

Chakula anachopika mama mara nyingi kinabakia wanamwaga kwa sababu ya upweke wa kuishi peke yao ninapokuwa nimetoka.

Wadogo zangu wote wameshaondoka nyumbani kwenda kujitegemea na kuanzisha miji yao , mimi ndiyo bado nimebakia nyumbani
Sio hawalalamiki, na wewe unaona nisawa kukaa home. Je mzee akitoka hutaweza kuondoka na kujitegemea au utabaki kumsaidia mama??
 
Kwa mawazo haya umaskini utakuandama Sana.
Kufikiri wazazi wafe urithi Mali ni mawazo ya kimasikini Sana.
Wazee wanadunda Hadi 90 halafu wewe Hadi 65 unasubiri urithi.

Watu wenye pesa hawasubiri uzee uliokithiri ili watoe viwanja, nyumba na mitaji kwa watoto wao.

Ukiona hiyo kitu bhasi ujue hao ni kipato cha kati ambapo unakuta baba ana nyumba mbili ama moja anayoishi na shamba kijijini. Kwa hiyo watoto macho yote hapo
 
Kwa vijana wa sasa hilo ni sahihi kabisa kwao .Ila enzi zetu huo umri ulisha oa zamani na una mji wako.Kuna moja nililikuta limevaa taulo kwa baba yake halijaoa lina 33 wala halina hata aibu aisee ?
Mm nna 35 na naishi kwa shangazi, siku akiwa nyumbani na mm nataka kuoga fresh kabisa napita mbele yake na Taulo langu jeusi
 
Kwa vijana wa sasa hilo ni sahihi kabisa kwao .Ila enzi zetu huo umri ulisha oa zamani na una mji wako.Kuna moja nililikuta limevaa taulo kwa baba yake halijaoa lina 33 wala halina hata aibu aisee ?
Wala sio shida home boy mimi nimeondoka Mabatini nikiwa na 25 na hata leo mpira ukiwa mgumu naweka kwapani naurudisha vizuri tu
 
Sema nn wakuu, Kibongobongo miaka 23 huyu bado ni mwanafunzi/mwanachuo labda mpaka 25-6 ndo unakuta ameshamaliza chuo.

Hapo weka miaka 2 ya kujitafuta, ongeza miaka miwili ya kujipanga kwenda kupanga, hapo jumla ni kama miaka 29-30

So atleast nikiona mtu ana 30 afu bado yupo home ndo naweza kushangaa na sio miaka 23.
 
🤣🤣🤣unarudisha mpira kwa kipa.Je na mzee nae angekua na mawazo kama yako sizani km ungekua na sehem ya kuita nyumbani
Alisharudisha mara nyingi sana hadi yeye na mke wake walilelewa.

Haya maisha yana kanuni nyingi mno alafu za kushangaza leo si unaona unafuraha unacheka kesho kuna kilio tena kichungu mno ndivyo maisha yalivyo.
 
Kwa vijana wa sasa hilo ni sahihi kabisa kwao .Ila enzi zetu huo umri ulisha oa zamani na una mji wako.Kuna moja nililikuta limevaa taulo kwa baba yake halijaoa lina 33 wala halina hata aibu aisee ?
Acha kujipakulia minyama mkuu wasukuma zamani walikua wanakaa kwa wazazi mpaka miaka 45 iweje utuambie ety miaka 23 upo kwako
 
Back
Top Bottom