Je ni sahihi kumuacha huyu mwanaume, au ni mvumilie huku naumia ?

Je ni sahihi kumuacha huyu mwanaume, au ni mvumilie huku naumia ?

Utoe ka million ka mtaji then ulale ndani usubiri kulelewa

Hakikisha nikirudi nikute vyombo visafi umepika na umefua nyumba safi na unipokee matunda niliyobeba

Mwanaume anaweza kua special
Au akawa speshoo 😅
Dada asante kwa kunijibia
 
Wanawake na ubinafsi hamjambo, eti namlisha yeye, anakuja kula ukweni anaondoka bila kuacha hata mia hizo ni dharau aisee, wewe ulishaachana naye hapa unataka upate sapoti tu, tayari ushaingia kiburi, yaani yeye akafanya starehe na wenzake wewe akakupa milion moja ukafanya mataji na biashara akaja kuiua mwenyewe, una uhakika katika zile milioni mbili hukugusa hata sent? Muachage dharau maisha ni mlima kuna kupanda na kushuka
 
Kawaida ya mwanaume timamu ambae anaijua future yake hua anapambana, na kama ikitokea kama ilivyotokea kwako haina budi kukaa nae chini na kuzungumza nae kwa kina na hata muda mwengine wewe kama wewe muombee dua abadilike mana anatuzalilisha vijana wenzake.
Asante lakin naona hawezi kubadilika kwa maneno yangu ni vyema nimuache
 
Acha mara moja kumpa pesa yoyote , unapofanya hivyo unampa sababu ya kuendelea kuwa mvivu.

Kama bado mnaishi pamoja tafuta njia ya kuondoka au yeye aondoke, kuendelea kuwa karibu yake ndiyo kunakufanya uendelee kufanya hayo yote unayoyafanya.

Wewe ni mama, nguvu unazotumia kumpambania mtu mzima ambaye haoni umuhimu wa kujipambania yeye mwenyewe zielekeze kwa mwanao na biashara yako, zingatia mwanao anahitaji kulelewa na mama mwenye afya ya akili.

Huyo mwanaume siyo rahisi kubadilika kwa sababu umekubali kuvumilia ujinga wake, atazidi kuharibika kwa sababu unamlea, ondoka, jenga maisha yako, na mwanao atakuja kukushukuru siku zijazo kwa ujasiri utakaouonyesha leo.
 
Sijui nakushauri vibaya au lah

Lakini huyo mwanaume hakufai
Usitishwe na maneno ya watu ya kuitwa single mother kheri uwe single mother kuliko kua single married

Ondoka hapo acha aendelee kulala akiona haupo na wa kumuhudumia hamna atachagua yeye sasa afe njaa au atoke njee akatafute

Binti wanaume ni wabinafsi sana kama hujui thamani yako utayumbishwa mpaka useme hiki ni nini?

Hivi umewahi kuona mwanaume akiacha ndoto zake au mipango yake kisa mwanamke

Sisi ndio deileee tunajitilisha huruma
Na kuishia kutumika na kunyanyaswa kihisia na muda mwingine tunaacha ndoto zetu na mipango yatu kisa wanaume

Wao hata huku jukwaani kila siku wanapandishiana nyuzi kushauriana
Utasiki man to man fanya hivi

Sisi huku nyuma ya keyboard kudanganyana
Shoga angu vumilia wanaume ndivyo walivyo upuuzi tu

Usivumilie upumbavu ondoka mapema angali una nguvu za kujitafutia na kujilea mwenyewe sio unavumilia unakuja kukumbuka kuondoka umekua ajuza

Jifunze kumsoma mwanaume muongo mbinafsi na mlagai kimbia upesi usimpe hata sekunde ya kuendelea kunyonya energy yako 🙏

Narudia jifunze kusoma mtu una em date macho yako usiyatoe kwenye macho yake muangalie kama anachozongumza kinatoka ndani

Ukiwa makini na timamu Mwanaume tapeli hachukui round una mdaka
Mhhhhhh jmn sio kwa kuwashambulia huko wanaume mboana tupo simple 2 lakini kwa hizo changamoto za mwenzetu huyo mdada nikwamba aongeze kamda kidogo na dua,umakini atajuwa linalompasa kufanya asant ila umetuponda sana sis wanaume
 
Wanawake na ubinafsi hamjambo, eti namlisha yeye, anakuja kula ukweni anaondoka bila kuacha hata mia hizo ni dharau aisee, wewe ulishaachana naye hapa unataka upate sapoti tu, tayari ushaingia kiburi, yaani yeye akafanya starehe na wenzake wewe akakupa milion moja ukafanya mataji na biashara akaja kuiua mwenyewe, una uhakika katika zile milioni mbili hukugusa hata sent? Muachage dharau maisha ni mlima kuna kupanda na kushuka
Asante ni ngumu kuwa upande wa mwanaume mwenzio lakini ili uepuke dharau na kiburi cha wanawake wanaume chenille kujibwwteka pambaneni
 
Brother huna
Una matatizo makubwa we mbibi , japo eti unajiita msichana wa miaka 26 mwenye mtoto Mmoja,my friend usichana unaishia miaka 17, 18 wewe ni mama ukisha ingia kwenye familia,na miaka 26 wewe ni jibibi.

Mumeo alikupa milioni 1 uanzishe biashara,umeona mwenzio kaishiwa,sasa wewe umejiona huwezi hudumia familia,kwani familia ni ya nani hasa!? Ni yako na mumeo,na yeyote anawajibika nayo,wewe hudumia, kama huwezi Rudi kwenu tukuone na huo usichana wako wa mchongo utafika wapi!!


Wanawake ni viumbe wapumbavu sana, hamuwezi vumilia wanaume wenu wanapokuwa na changamoto,lakini sisi tunawavumilia in any condition. Mimi nakushauri uachane na huyo mwanamume kwakuwa umejiona wewe ni mpambanaji,umeingiwa na kiburi cha kutoweza tambua umuhimu na fadhira ulizofanyiwa na mumeo
Brother huna akili usiniulize kwanini
 
kujiona yeye hakosei kila wakati yupo sahihi

Huyu mwanaume kutoa 1M sio sababu ya yeye kujifungia ndani na asitake kazi tena yaan anafanya makusudi kisa ana uhakika atakula na atalala unaona ni sahihi wewe?

Sisi tunajadili hoja iliyo mezani
Kaka nikuambie sio huyu tu wa mleta mada wanaume kutohudumia familia na kutaka kulelewa limekua janga
Sababu ya kutohudumia familia hataki kufanya kazi ngumu anataka udalali ambao haumpi ela
 
Wanawake na ubinafsi hamjambo, eti namlisha yeye, anakuja kula ukweni anaondoka bila kuacha hata mia hizo ni dharau aisee, wewe ulishaachana naye hapa unataka upate sapoti tu, tayari ushaingia kiburi, yaani yeye akafanya starehe na wenzake wewe akakupa milion moja ukafanya mataji na biashara akaja kuiua mwenyewe, una uhakika katika zile milioni mbili hukugusa hata sent? Muachage dharau maisha ni mlima kuna kupanda na kushuka
Hio milioni moja sio tiketi ya kutohudumia famila je milioni moja wewe unaweza itumia ndani ya miaka 5 na ikawepo mpaka leo
 
Piga goti omba roho ya mabadiliko na uwajibikaji

Hakika atabadirika na hakuna linaloshindikana kwa MUNGU
 
Sisi kwenye Baraza letu la usuluhishi wa ndoa, tunasikiliza Kila upande. Hapo umeeleza ya mwenzio, naye angeeleza Yako. Maana Hadi wazazi wako wanamkaribisha Kuna kitu hatukijui hapa
 
kujiona yeye hakosei kila wakati yupo sahihi

Huyu mwanaume kutoa 1M sio sababu ya yeye kujifungia ndani na asitake kazi tena yaan anafanya makusudi kisa ana uhakika atakula na atalala unaona ni sahihi wewe?

Sisi tunajadili hoja iliyo mezani
Kaka nikuambie sio huyu tu wa mleta mada wanaume kutohudumia familia na kutaka kulelewa limekua janga
Hivi ni kwanini
 
Back
Top Bottom