Je ni sahihi kumuacha huyu mwanaume, au ni mvumilie huku naumia ?

Utoe ka million ka mtaji then ulale ndani usubiri kulelewa

Hakikisha nikirudi nikute vyombo visafi umepika na umefua nyumba safi na unipokee matunda niliyobeba

Mwanaume anaweza kua special
Au akawa speshoo 😅
Dada asante kwa kunijibia
 
Wanawake na ubinafsi hamjambo, eti namlisha yeye, anakuja kula ukweni anaondoka bila kuacha hata mia hizo ni dharau aisee, wewe ulishaachana naye hapa unataka upate sapoti tu, tayari ushaingia kiburi, yaani yeye akafanya starehe na wenzake wewe akakupa milion moja ukafanya mataji na biashara akaja kuiua mwenyewe, una uhakika katika zile milioni mbili hukugusa hata sent? Muachage dharau maisha ni mlima kuna kupanda na kushuka
 
Asante lakin naona hawezi kubadilika kwa maneno yangu ni vyema nimuache
 
 
Mhhhhhh jmn sio kwa kuwashambulia huko wanaume mboana tupo simple 2 lakini kwa hizo changamoto za mwenzetu huyo mdada nikwamba aongeze kamda kidogo na dua,umakini atajuwa linalompasa kufanya asant ila umetuponda sana sis wanaume
 
Asante ni ngumu kuwa upande wa mwanaume mwenzio lakini ili uepuke dharau na kiburi cha wanawake wanaume chenille kujibwwteka pambaneni
 
Brother huna
Brother huna akili usiniulize kwanini
 
Umetoa ushauri mzuri sana kwake ila akiachana nae tu ajue nje vijana hawaoi single mother wa kizazi kipya
Jidanganyeni eti wanaume hawaoi single maza chunguza vzr
 
Sababu ya kutohudumia familia hataki kufanya kazi ngumu anataka udalali ambao haumpi ela
 
Hio milioni moja sio tiketi ya kutohudumia famila je milioni moja wewe unaweza itumia ndani ya miaka 5 na ikawepo mpaka leo
 
Piga goti omba roho ya mabadiliko na uwajibikaji

Hakika atabadirika na hakuna linaloshindikana kwa MUNGU
 
Sisi kwenye Baraza letu la usuluhishi wa ndoa, tunasikiliza Kila upande. Hapo umeeleza ya mwenzio, naye angeeleza Yako. Maana Hadi wazazi wako wanamkaribisha Kuna kitu hatukijui hapa
 
Hivi ni kwanini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…