Je ni sahihi kumuacha huyu mwanaume, au ni mvumilie huku naumia ?

Uhalisi wa maisha yake anajua muhusika wanaume tafuteni ela muhudumie familia zenu muepuke dharau
 
Ni kweli nilijipachika mimba na nikaingia kwenye maisha yake pengine hakua tayari kuwa na familia ni kosa ambalo najutia mno ila siwez kubadilisha makosa japo naumia na kujutia
Hilo ndio ulitakiwa uanze kulisema kwanza kuliko kumsimanga mtoto wa watu kwa makosa yako, umesema alikataa baadaye akakubali, kwa hiyo usimtwishe mzigo na kumpaka maneno
 
Utoe ka million ka mtaji then ulale ndani usubiri kulelewa

Hakikisha nikirudi nikute vyombo visafi umepika na umefua nyumba safi na unipokee matunda niliyobeba

Mwanaume anaweza kua special
Au akawa speshoo 😅
Wewe ni mbabe
 
Hilo ndio ulitakiwa uanze kulisema kwanza kuliko kumsimanga mtoto wa watu kwa makosa yako, umesema alikataa baadaye akakubali, kwa hiyo usimtwishe mzigo na kumpaka maneno
So point yako ni ipi
 
Hata kama una hasira kaanaye chini mweleze ili ajue tatizo lake na kama hakusikii tafuta rafiki yake mkubwa sana mweleze ili ampange jamaa. Plz hata kama una hasira kiasi gani usimtamkie mwanaume neno tuachane kumbuka hasira inaisha ila maneno yanaishi lichukulie hilo jambo kama jalibu lako kwahiyo pambana sababu ukisema umuache je unaachana na wangapi? Je unataka uwe single mother ili ubaruzwe vizuri? Unaweza kumwambia jamaa muachane alfu akafanya mabadiliko mambo yakaisha na mkaishi vizuri ila hilo neno tuachane litakuwa likizunguka akilini kwa huyo jamaa hivyo kuna siku atakuacha ww alfu maisha yamenyoka .NoTe kumwambia mwanaume tuachane ni sawa na kumwambia wewe siyo mwanaume
 
Dah huyo sio mwanaume ni kiumbe cha kiume .
Kimbia sister huyo sharobaro hakufikishi popote na wa hivyo najua kitandani masha'Allah ndiyo maana unatatizika kumbwaga sema nini ,tududu tupo twingi temana na huyo mlamba midomo
 
Nitumie namba yako nikupe ushauri ujue namna nzuri ya kujitunjika kwenye kamba bila kuumia wala kuumiza mtu au kumuacha bila kumuumiza ulie muacha..
 
Nilichojifunza maumivu ya maisha yako unayajua mwenyewe ni kuchuja chuya na mchele uko wapi alafu nyie wanaume why ni wabinafsi yani koment nyingi humu achana nae uwe single maza hivi mnaisi waliolewa wote walikutwa na bikira zako au hawana watoto ebu chenille kumdhoofisha mwanamke kwa kigezo cha usingle maza hao single maza ndio hao nyinyi mliowazalisha na kuwaacha acheni ubinafs tafuteni ela mleee familia zenu
 
Ulitaka nisemeje nimkingie kifua kwa kumtetea
Kwani ni lazima kusema? Kama umeona hakufai kwanini umseme vibaya mtu aliyekuwa anakuhudumia kabla hajaacha kazi, na unakiri kabisa na ya mtaji alikupa? Kwani hujui kuna wengine hata mtaji hawajaw pewa? Wamezalishwa tu na kuachwa?
 
Hata hivyo ugolikipa haufai. Mwanaume hakikisha umeoa mwanamke aliye enda shule na anayejua kufanya kazi. Hii itasaidia kufunza hata watoto wako wakike jinsi ya kujitegemea
Ni mwanamke gani anataka kua goalkeeper saiv bro ?

Nyie si ndio hamtaki wanawake wafanye kazi kwa kuhofia wakujipata mtashindwa kuwa nyanyasa?
 

Kwani ni lazima kusema? Kama umeona hakufai kwanini umseme vibaya mtu aliyekuwa anakuhudumia kabla hajaacha kazi, na unakiri kabisa na ya mtaji alikupa? Kwani hujui kuna wengine hata mtaji hawajaw pewa? Wamezalishwa tu na kuachwa?
Kaka nikuulize kitu mfano shida yako ww ilikua milioni mbili ili ufanye biashara ukamuomba mshikaji wako akusaidie akakupa ww ukafanikiwa kwenye biashara kias chake ukaenda kukaa kwa rafiki yako ambae alikusaidia ile ela lakini rafiki yako badaa ya kuona ww umefanikiwa akawa afanyi kazi anakutegemea ww umlishe ,umvishe ,kila kitu ww kisa alikusaidie milioni mbili na ukimwambia tafuta kazi rafiki yangu anakujibu kazi hamna ww ndo ujue maisha yake nijibu utafanyaje ikiwa upo na rafiki kama uyo unaishi nae ndani
 
Simtetei mume wa mtoa mada, sababu kiuhalisia mumewe anakosea kujilemaza bila kuhudumia chochote kwa familia yake.
Twende sawa hapa
Mke akiwa hana kazi kwa misingi ipi anajilemaza ?
Au anapambana kutafuta kazi
Ila bado hajapata?

hivi huoni huyo mwanaume hataki kutoa mguu ndani anataka alale aangalie movie kwenye flash

Huyo mwanaume angekua anafanya juhudu za kutafuta kazi asingelalamikiwa hata kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…