Je, ni sahihi kwa mwanamke kunyonyesha hadharani?

Je, ni sahihi kwa mwanamke kunyonyesha hadharani?

View attachment 3077317

Katika mwili wa mwananke kifua ni sehemu nyeti na haipaswi kuonwa na watu wengine zaidi ya mwenye mamlaka tu, yaani Mume.

Lakini tunaona baadhi ya wanawake wakinyonyesha watoto wao hadharani bila kuficha au kusitiri vifua vyao, mfano katika vyombo vya usafiri au sehemu zenye mikusanyiko ya watu.

Ni haki ya mtoto kupatiwa maziwa pale atakapo hitaji, lakini sidhani kama sababu hii ndyo inahalalisha mwanamke kutoa ziwa mahali popote.

Kwa walio na dini au wasio na dini wote wanafahamu kifua cha mwanamke ni sehemu nyeti na haipaswi kuonekana hovyo.

Je, ni sahihi kunyonyesha mahali popote kwa kisingizio cha kumpa mtoto haki yake?
Hakuna jambo hilo.Kwani ukifumba macho na kutafakari,anakua hana matiti au vidole?Kila kiungo ni tafsiri yako tu.Watoto wanyonyeshwe muda wote watakapo.Afutaroo,there is no fixed time and specific place for breastfeeding!
 
Kwaio mtoto aendelee kulia njaa Na kuumwa njaa Kisa unaogopa watu😅😅😅😅mama atabaki kuwa mama being a mother unasacrifice a lot ....mwenye kosa Ni mtazamaji ukiona Ivo usiangalie kwepesha macho
 
Kwaio mtoto aendelee kulia njaa Na kuumwa njaa Kisa unaogopa watu😅😅😅😅mama atabaki kuwa mama being a mother unasacrifice a lot ....mwenye kosa Ni mtazamaji ukiona Ivo usiangalie kwepesha macho
Mtoto ni lazima apewe Chakula chake, ila ni busara kama Mama atafunika na kuficha kifua chake pasipo kuruhusu watu wengine kuona
 
Sio sahihi na wanao fanya hivyo hawana hekima wala busara, mwanamke anaye jua thamani ya kifua chake hawezi ruhusu kionekane kwa sababu ya kumpa mtoto.
Vyema sana Mkuu, wale ambao hawaelewi hili ni dhahiri hawana heshima na nidhamu, hawajui umuhimu wa kujistiri na kutunza heshima ya maumbile.
 
View attachment 3077317

Katika mwili wa mwananke kifua ni sehemu nyeti na haipaswi kuonwa na watu wengine zaidi ya mwenye mamlaka tu, yaani Mume.

Lakini tunaona baadhi ya wanawake wakinyonyesha watoto wao hadharani bila kuficha au kusitiri vifua vyao, mfano katika vyombo vya usafiri au sehemu zenye mikusanyiko ya watu.

Ni haki ya mtoto kupatiwa maziwa pale atakapo hitaji, lakini sidhani kama sababu hii ndyo inahalalisha mwanamke kutoa ziwa mahali popote.

Kwa walio na dini au wasio na dini wote wanafahamu kifua cha mwanamke ni sehemu nyeti na haipaswi kuonekana hovyo.

Je, ni sahihi kunyonyesha mahali popote kwa kisingizio cha kumpa mtoto haki yake?
Matiti hayatakiwi kuchukuliwa viungo vya faragha. Hata wanaume wana matiti japo huwa ni madogo. Lakini hata wanawake wengine wanamatiti madogo.

KInachotakiwa kufichwa ni UKE na UUME
 
Shida inaanzia kwenye kauli yako "ni sahihi kunyonyesha hadharani"ukisema hivyo means mtoto akilia mbele za watu aachwe tu kisa kuna watu! kunyonyesha ni wajibu wa mama na haki ya mtoto anapohitaji haijalishi ni kwenye mazingira gani. ila suala ni ustaarabu tu wa mama mwenyewe je atafunika maziwa yake wakati ananyonyesha au ataacha wazi.
 
Matiti hayatakiwi kuchukuliwa viungo vya faragha. Hata wanaume wana matiti japo huwa ni madogo. Lakini hata wanawake wengine wanamatiti madogo.

KInachotakiwa kufichwa ni UKE na UUME
Wewe unaweza kukaa mbele ya wazazi wako kifua wazi?
 
Kwahiyo akiamua kuacha wazi ni sawa?
Ni sawa tu mkuu hakuna sheria kwamba ni kosa, ni kama vile kuna mtu anaweza kula mbele za watu na kuna mwingine hawezi na hakuna mwenye kosa kati yao kila mmoja ni ustaarabu wake tu aliojiwekea
 
Ni sawa tu mkuu hakuna sheria kwamba ni kosa, ni kama vile kuna mtu anaweza kula mbele za watu na kuna mwingine hawezi na hakuna mwenye kosa kati yao kila mmoja ni ustaarabu wake tu aliojiwekea
Wewe unaweza kuruhusu mke wako akae kifua wazi mbele ya wazazi wako au marafiki zako?
 
Kwanza sijao na sina mpango wa kuoa hivyo sina experience ya mwanamke anaenyonyesha. ila Kwa kujibu swali lako tu mtu mzima hapangwi, anaweza akaficha ukiwepo na usipokuwepo akaachia. Mimi napenda mtu anaejiheshimu yeye yaani yeye ndo aone hili jambo si sawa sio mimi nimfundishe kujiheshimu.
 
Back
Top Bottom