Je, ni wakati wa kuwatambua Mbowe na Lissu kama maadui wa taifa?

Je, ni wakati wa kuwatambua Mbowe na Lissu kama maadui wa taifa?

Bavicha hawaamini wanachokiona uturn iliyopigwa na maadui wapya wa taifa ni ya hatari 😂😂

Mbowe na Lissu hawakushiriki kupitisha tozo bungeni, waliopitisha tozo ni wabunge wa CCM na Covid 19. Kama ni lawama wapelekee hao na sio kina Mbowe na Lissu ambao wataishia kupinga kwenye press conference basi hakuna badiliko litakalo tokea.

Adui wa taifa ni yule aliye kubali kupitisha tozo hizi zote na kushindwa kupunguza ugumu wa Maisha.
 
Lissu kapata ulemavu akitetea tumbo lake mtetezi wa nchi asingeweza kukaa upande wa acacia wakati tunapambania madini yetu.

Kumbe Lissu alipigwa Risasi kiss kutetea acacia?. Unaiaibisha serikali yako. Kwanza unasema imempa pesa Lissu halafu unasema ilimpiga risasi Lissu kiss anatetea acacia.
 
Hapo nyuma walikuwa wanatudanganya kuwa wao ni wapambanaji na wapo kwa ajili ya maslahi ya taifa.
Pamoja na ugumu wa kufanya siasa zao za ujanja ujanja kwenye awamu ya tano lakini walikuwa wanapiga sana kelele na kuwaaminisha wafuasi wao wanapambania nchi.

Kelele zilikuwa nyingi baada ya kupoteza mali zao zenye makando kando na kuingia kwenye usaliti wa nchi kwenye sakata la madini.

Tumeona awamu ya sita imewaita ikulu na kuwapa wanachotaka. Lissu kapewa kila alichokuwa anadai.

Mbowe inasemekana pamoja na kufunguliwa gazeti lake ila kavuta mzigo wa maana.

Sasa hivi lugha yao imekuwa tofauti wanasema hawawezi kuongoza mapambano ya watu wasiojitambua.

Yani wafuasi wenu wamekuwa hawajitambui baada ya nyinyi kuingia makubaliano na Mama??

Mliitisha maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi alafu viongozi hamkuonekana watu wakaja kuona Lissu anasindikizwa kupanda ndege na mabeberu huku Lema akitokomea kupitia njia za panya.

Kwa siasa hizi za uongo uongo na kujali matumbo yao. Je, ni wakati wa kuwatangaza watu hawa kama maadui wapya wa taifa letu??

NB: Zitto hatumuoni tena akija na analysis za kiuchumi wakati huu wa tozo kila eneo tofauti na huko nyuma.
Akili yako kama ya mwendazake
 
Hujui unachokibishia unafikiri mbowe ni mwanamziki? mbowe ni mwanasiasa na kiongozi wa upinzani ilitakiwa yeye ndo awe wa kwanza kupinga haya yanayoendelea sasa kuliko hata kipindi cha nyuma na hiyo ndo nafasi alioichagua au unafikili siasa ni mpaka uchaguzi tu
Unataka apinge kukusanya kodi?
Huna akili kabisa kuna nchi inaendelea bila kodi.
Fyatu kabisa wewe
 
Kwako mtoa mada Lissu kawa mlemavu wewe umepoteza hata ukucha kwa sababu ya kutetea Nchi,Mbowe amesota mahabusu karibu mwaka wewe ushawahi kukaa hata usiku mmoja,binasfi naona kukaa kwao kimya ni vizuri maana walikuwa wanaumia peke yao kwa kutetea kundi la watu wengi.
Mkuu mbona kuna watanzania kibao jela wamefungwa kionevu na wako hadi hawana watu wa kuwaaombea kutoka kama ilivyokuwa kwa Mbowe.
 
Mbowe ana kusanya kodi? Au Lisu anakusanya kodi? Mbona mnakuwa wajinga sana, post za kijinga sana kutwa nzima Mbowe Mbowe, ana kusanya kodi?

Mbowe ana husiana vipi na ayanayo endelea kwa sasa? Hujui wa kuwapelekea lawama?

Alivyo kuwa Jela wewe na Familia yako mliandamana hata Sebuleni kwenu kupinga Mbowe kukamatwa?
Mbowe alivyokamatwa watu walipigia kelele kutaka aachiwe hawakukaa tu kimya na kweli akaachiwa, na Mbowe huyo huyo kabla ya kukamatwa alishapoteza mali zake kwa sababu ya kukosoa serikali ila hakukaa kimya ndio alizidi kuongea sasa ajabu sasa hivi kukaa kimya na kuhusu kwenda Jela wala hata sio mara ya kwanza kukaa jela.
 
Mkuu mbona kuna watanzania kibao jela wamefungwa kionevu na wako hadi hawana watu wa kuwaaombea kutoka kama ilivyokuwa kwa Mbowe.

Inalaumu serikali ya CCM na sio upinzani. Tofautisha mwenye mamlaka na asiye na mamlaka. Pia Mbowe alitoka kwa kelele za watu naye alikiwa afungwe Maisha.
 
Huu ni uchochezi. Na unajenga Uhasama wa visa na hila .
Umakini unahitajika.
 
Mbowe alivyokamatwa watu walipigia kelele kutaka aachiwe hawakukaa tu kimya na kweli akaachiwa, na Mbowe huyo huyo kabla ya kukamatwa alishapoteza mali zake kwa sababu ya kukosoa serikali ila hakukaa kimya ndio alizidi kuongea sasa ajabu sasa hivi kukaa kimya na kuhusu kwenda Jela wala hata sio mara ya kwanza kukaa jela.

Acha kuzunguka mbuyu. Nani anastahili lawama wabunge wa CCM waliopitisha tozo au Mbowe aliyeko nje ya bunge.
 
Hapo nyuma walikuwa wanatudanganya kuwa wao ni wapambanaji na wapo kwa ajili ya maslahi ya taifa.
Pamoja na ugumu wa kufanya siasa zao za ujanja ujanja kwenye awamu ya tano lakini walikuwa wanapiga sana kelele na kuwaaminisha wafuasi wao wanapambania nchi.

Kelele zilikuwa nyingi baada ya kupoteza mali zao zenye makando kando na kuingia kwenye usaliti wa nchi kwenye sakata la madini.

Tumeona awamu ya sita imewaita ikulu na kuwapa wanachotaka. Lissu kapewa kila alichokuwa anadai.

Mbowe inasemekana pamoja na kufunguliwa gazeti lake ila kavuta mzigo wa maana.

Sasa hivi lugha yao imekuwa tofauti wanasema hawawezi kuongoza mapambano ya watu wasiojitambua.

Yani wafuasi wenu wamekuwa hawajitambui baada ya nyinyi kuingia makubaliano na Mama??

Mliitisha maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi alafu viongozi hamkuonekana watu wakaja kuona Lissu anasindikizwa kupanda ndege na mabeberu huku Lema akitokomea kupitia njia za panya.

Kwa siasa hizi za uongo uongo na kujali matumbo yao. Je, ni wakati wa kuwatangaza watu hawa kama maadui wapya wa taifa letu??

NB: Zitto hatumuoni tena akija na analysis za kiuchumi wakati huu wa tozo kila eneo tofauti na huko nyuma.
WaTanzania wa leo hamna tofsuti na WaIsrael wa kipindi cha Yezebel na Ahabu. Kuna watu waliwasemea mkawaona ni watumwa wa Mabeberu. Leo wamekaa kimya mpo mnawananga. Hivi wewe unaskkia raha mke na watoto wa Mbowe na Lissu wakilia kila siku kuhusu hali za baba yao? Hata Eliya baada ya kuwaona WaIsrael hawaeleweki alienda kujilaza penye kijito ili afe. Hakuhangaika na WaIsrael tena. Now our fate is in our hands. Lets show we are feeling the pinch or we are busy with Simba and Yanga. If we cant stand with our self then we got no right to open our mouth. Those families have had enough already. Jail, hospital bills and others like that. Now we anoint you to take their place. Please forward move the Tanzanian agenda of second liberation!!
 
Inalaumu serikali ya CCM na sio upinzani. Tofautisha mwenye mamlaka na asiye na mamlaka. Pia Mbowe alitoka kwa kelele za watu naye alikiwa afungwe Maisha.
Sijalaumu bali nawaambia mnaosema hatukufanya kitu Mbowe alipofungwa kana kwamba ndio mtanzania pekee kufungwa kionevu wakati yeye alipofungwa watu walipiga kelele hadi akaachiwa ila wapo watanzania wengine huko jela kabla ya Mbowe na hakuna wa kuwapigia kelele kama ilivyokuwa kwa Mbowe, sasa ajabu kaachiwa anakuja kukaa kimya.
 
Acha kuzunguka mbuyu. Nani anastahili lawama wabunge wa CCM waliopitisha tozo au Mbowe aliyeko nje ya bunge.
Kwani hata Mbowe angekuwepo huko bungeni na hizo tozo zikapita ndio ina maana na yeye kapitisha hizo tozo au kwamba Mbowe ndio alikuwa anaweza kuzuia wabunge wa ccm wasipitimishe mambo yao?
Watu wanachokisema ni kutokuona Mbowe akikosoa tena serikali kitu ambacho hakiitaji yeye hadi awe mbunge.
 
Back
Top Bottom