Je, ni wakati wa vijana kufikiria kutafuta kazi nje ya nchi?

Vijana gani hao?hawa wa dot.com?,kijana ana first degree ualimu, unakuja lalama humu wakati kuna ajira far east za kwenda kufundisha kiingereza, Rwanda ameenda Zimbabwe kutafuta English teachers!,vijana wa kwanza kujilipua kwa kazi za ubaharia ukanda huu wa Afrika walikua ni watanzania, Gerezani, ilala &magomeni (hawa walikua vijana ngangari wenye ku take risks)
 
Mheshimiwa rais wetu mpendwa sana mama yetu kipenzi dokta Samia suluhu Hasan anaupiga mwingi. Ameboresha huduma za afya, elimu, ajira kama njugu maslahi bora kwa wafanyakazi hasa waalimu na sekta nyingine. Nani kama mama? Mama mpaka 2030. Achana na Kenya watu wa shida hao.
 
Wewe kama barua ya mwaliko ni tatizo, visa utapata kweli? Au utabakia na passport kama pambo?
 
Kumbe ulienda kwa nauli ya Baba yako. Basi sawa.

Asante kwa elimu lakini.
 
Pasport tu wanataka barua ya mwaliko. Sas aunajiuliza Mwaliko naupata wapi hata passport sina?
 
Kasome namba 5 ! Usifikiri kusaidiwa na serikali jitume kwanza . Yaani umeshaingiza serikali bila hata ya kujua hakuna mtu anaye kuzuia bali ni wewe mwenyewe
Maneno kama haya yapo sana mtaani hasa kwa nyie mliofanikiwa huwa mnaona ambao hawajafanikiwa kama wajinga, wavivu wasiojituma wala kuona mbele😅😅😅
 
Yaani ndugu yangu Tz bado mambo mengi Wana 'hangover' za kuwa na mifumo ya enzi za siasa za kikomunisti za siku zote kuwa na mawazo ya kudhibiti ' movement za raia wake, wasitoke nje hata kama fursa mazingira ya kujipatia riziki ndani hazipo......kaazi kwelikweli.
 
Naomba kwanza kabla ya kutulaum sisi vijana unijumlishie Jumla ya gharama ya passport na visa na nauli ya safari kutoka Tanzania hadi Kuwait kwa mfano.

Baada ya hapo uje kutulaum sisi vijana
Wenzetu wa nchi nyingine wanaziwezaje hizo gharama? Watu mpaka wanachanga ukoo mzima mtu mmoja avuke boda.
 
Sio lazima barua ya mwaliko unaweza ambatisha hata tangazo la scholarship zilizotangazwa sehemu yeyote wanakupa chap....tena siku hizi hamna vishoka Kila kitu ni online ukimaliza application unapeleka hard copy.....yaani hawana shida hata.
 
Andiko bora la mwaka, vijana wamestuck...... hakuna progress hawana future na wengi wanashindwa hata kuwa na familia sasa tutakuja kuwa na wazee wa hovyo hapo baadae
Wanatengeneza tabaka kubwa sana la wasomi masikini.
 
Kuhusi kwenda kufundisha kiingereza unawaonea tu nani atakupa kazi ya kufundisha lugha ambayo si lugha yako ya kwanza? Jiulize kwa nini Rwanda walikwenda Zimbabwe na si kwingineko. Wangeenda kutafuta walimu wa kiswahili huko ndio tungepaswa kujiuliza.
 
You speak upuuzi hivi unajua Maisha ya watz we Jamaa idiotism.
Leta suluhisho Wacha kulalama bila kutoa suluhu unafikiri watu wakijichanga ukoo mzima hawapati hela za mtoto wao kufanya michakato akatoka hapa? Maisha ya watanzania ni ya kuchangia sherehe si ndio.
 
Leta suluhisho Wacha kulalama bila kutoa suluhu unafikiri watu wakijichanga ukoo mzima hawapati hela za mtoto wao kufanya michakato akatoka hapa? Maisha ya watanzania ni ya kuchangia sherehe si ndio.
Natania tu mkuu usipanic upo sahihi
Je ni nchi gani Kuna fursa kijana anaweza kwenda kujitaftia Ugali wake?
 
Mkuu tuongee facts, Rwanda ameenda kutafuta waalimu wa kiingereza Zimbabwe, why aturuke sisi?,Zimbabwe wapo super!!,kiswahili mmmmm SA alitafuta waalimu Kenya na sio Tanzania, hii nayo ni fact, tusiogope kuongea mapungufu yetu ili tujijenge,mabaharia wa mwanzo pale Gerezani qts hawakujua kiingereza au kigiriki BUT walikua ni risk takers, wengi walifankiwa na wengi pia walikufa,elewa wengine hata passport hawakua nazo,na walisafiri pori kwa pori hadi Egypt!,wakikumbana na vita vya Mr Garang pale Sudan!!,dot.com ni lalama tu ndani ya JF
 
Kuna mambo ambayo kama nchi hatutakiwi kuyapata kwa shida.dunia iko kila mahali sasa hivi,na viongozi wamesoma sasa kwanini vitu kama kwenda kutafuta maisha nje ya nchi kuwe na milolongo mingi isiyo na sababu.kwahiyo serikali haikwepi kwenye hili.kulitakiwa kuwe na mifumo rahisi na rafiki kwa kila mtu ili mtu yoyote akihitaji anapata huduma.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Wewe kama barua ya mwaliko ni tatizo, visa utapata kweli? Au utabakia na passport kama pambo?
Naongelea kupata hati ya kusafiria kwanini tunawekeana vikwazo wakati ni haki ya kiła raia anayehitaji na ukiangalia kwa jicho la umakini ni chanzo kikubwa cha mapato kwa serikali kwanini tunashindwa kuiga jirani zetu tunabaki na akili za kijima Miaka nenda rudi? Kwanini uombe barua ya mwaliko kwa muombaji kama anataka apate hati kwanza ndipo apange safari yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…