Je, ni wakati wa vijana kufikiria kutafuta kazi nje ya nchi?

Je, ni wakati wa vijana kufikiria kutafuta kazi nje ya nchi?

Nchi wa wapumbavu hii hawataki vijana wapige hatua passport tu Kupata changamoto kubwa fursa hazioenekani
Changamoto una itolea wapi?

Kuna group la wanafunzi kwenda china wana fundisha mpaka namna ya kupata passport na kwa sababu ni mandatory...

Wewe una shindwaje? Au utafutiwe pesa upewe uletewe na passport!

Mimi pass nimeipata mwaka wa pili chuo na sina safari ya wapi kwa kwenda

Nikachukua 50,000/- kipindi hicho nikapeleka, barua ya mwaliko nika tafuta mitandaoni huko, dean wa wanafunzi akanipa barua ya utambulisho nikapeleka uhamiaji nakupata huduma

Wewe una taka je?

Naona watu wana lalama passport ngumu kupata ngumu kupata...

Sasa kama pass ina kushinda si utarejeshwa kwenu kwa kukosa kadi ya Homa ya inni?

Visa utapata kweli na benki a/c yako ina zero?

Mna fikirisha ndio maana zina onekana ni ngumu kupata ila sio ngumu ni nyepesi mnooooo...

Hiko kipengele cha barua ya mwaliko ni chepesi sana sana...

Zipo vyuo vina toa admission letter una weza tumia, na kwa kuanza wana kubari ujaze National ID yako! Uki pewa una enda ombea Visa

Kuna conferences kibao zina toa barua za mialiko

Kuna training kibao nje zina toa barua za mialiko nk

Tafuta taarifa upate maarifa!

Wenye uhitaji wameshapa pass, wasio na uhitaji wana lalamika mitandaoni... mpambanaji hawezi kosa

Tuna fahamu mpaka watu mitaani wanao watafutia vijana passport na kuwa saidia kupata visa wana enda ulaya na marekani kufanya kazi wapo darasa la saba kibao ata kingereza hawa jui

Wewe umesoma mpaka PhD bado upo jalalani una subiri mtu aje akutoe jalalani kama Prof.

Passport yetu kuipata ni rahisi sanaaaaa
 
Sio lazima barua ya mwaliko unaweza ambatisha hata tangazo la scholarship zilizotangazwa sehemu yeyote wanakupa chap....tena siku hizi hamna vishoka Kila kitu ni online ukimaliza application unapeleka hard copy.....yaani hawana shida hata.
Yeah ndio maana nasema anaye shindwa kupata pass kwa sababu ya barua basi huyo hana nia ya Safari bali ni malalamiko FC

Watu wana zipata mtaani kama njugu wanazo wame weka ndani

Wengine mpaka chanjo wanaenda chomea zenji wapate vikadi kamavya ATM vya uviko

Leo watu wana kaa mtandaoni wame kariri kama insha za kidato cha nne mfekane war, maji maji war...!
 
Naongelea kupata hati ya kusafiria kwanini tunawekeana vikwazo wakati ni haki ya kiła raia anayehitaji na ukiangalia kwa jicho la umakini ni chanzo kikubwa cha mapato kwa serikali kwanini tunashindwa kuiga jirani zetu tunabaki na akili za kijima Miaka nenda rudi? Kwanini uombe barua ya mwaliko kwa muombaji kama anataka apate hati kwanza ndipo apange safari yake?
Barua ya mwaliko Au sababu ya Safari

Ile ni hati ya kusafiria... na moja ya vigezo vya kuipata ni kuwa na barua ya mwaliko Au sababu ya Safari ili upewe

Mbona hauulizi kuhusu viambatanisho vingine kama

-cheti chako cha kuzaliwa
-cheti cha Mazazi cha kuzaliwa
-nk

Kwanini barua? Ndio iwe kikwazo kwako?

Huwezi kupata basi tafuta na consults wapo wata kusaidia na utaipata safi kabisa

Ukiwa na nia huwezi kosa hii kitu boss
 
Pasport tu wanataka barua ya mwaliko. Sas aunajiuliza Mwaliko naupata wapi hata passport sina?
Yana wanafanya mambo kijima kabisa dunia inakimbia wao bado wanaota ndoto katika usingizi wa pono vikwazo kama hivi ni changamoto juu ya kuharakisha kuchangamkia fursa mbalimbali zilizoko nchi mbalimbali sasa ukianza kufikiria barua ya mwaliko eti ndo kigezo cha kupata hati ya kusafiria kama sio uzwazwa ni nini hii? Haishangazi kijana wa Kitanzania aliamua kuhamishia makao makuu ya kampuni yake Nairobi (Kenya) baada ya kukumbana na urasimu usio na faida kutoka mamlaka mbalimbali za serikali wamekuja kushtuka kijana ashapewa ruhusa ya kuanza shughuli zake kutokea Kenya eti nao wanampatia kibali yani ni uzwazwa kwenda mbele
 
Yeah ndio maana nasema anaye shindwa kupata pass kwa sababu ya barua basi huyo hana nia ya Safari bali ni malalamiko FC

Watu wana zipata mtaani kama njugu wanazo wame weka ndani

Wengine mpaka chanjo wanaenda chomea zenji wapate vikadi kamavya ATM vya uviko

Leo watu wana kaa mtandaoni wame kariri kama insha za kidato cha nne mfekane war, maji maji war...!
Kwanini kuwe na mazingira magumu mwanzo tu kwanza inachochea mianya ya rushwa hakuna aliyesema inashindikana kupatikana mtaani ni rahisi wengi tunaelewa swali, je kuna umuhimu gani wa sharti kama hilo kuwepo kwenye form za maombi kama kiambata kwanini tuendelee kuchochea mazingira ya kugushi nyaraka kusiko na afya yoyote kwa nchi yetu maana nia ya kubadilisha mfumo wa kutoa hati za kusafiria umetumia gharama kubwa sana sasa badala uwe na tija kwa nchi kwa kusaidia kuingiza mapato zaidi tunaona sawa tu idadi ndogo ya maombi na wachache wakipata hati.
 
Barua ya mwaliko Au sababu ya Safari

Ile ni hati ya kusafiria... na moja ya vigezo vya kuipata ni kuwa na barua ya mwaliko Au sababu ya Safari ili upewe

Mbona hauulizi kuhusu viambatanisho vingine kama

-cheti chako cha kuzaliwa
-cheti cha Mazazi cha kuzaliwa
-nk

Kwanini barua? Ndio iwe kikwazo kwako?

Huwezi kupata basi tafuta na consults wapo wata kusaidia na utaipata safi kabisa

Ukiwa na nia huwezi kosa hii kitu boss
Miongoni mwa vingi nimetaja hiyo barua kama mtu yuko na kitambulisho cha taifa chenye taarifa zote za mtu inakuaje tena unamuomba cheti chake cha kuzaliwa ina maana mifumo ya serikali haisomani ni mwendelezo ule ule wa mawazo ya kijima ambao hauna tija kwenye ustawi na taifa letu.
 
Kazi nje zipo nyingi lakini ili upate kazi kirahisi lazima uwe na passport, lakini mtu akitaka passport hawezi kukosa maana wapo watu wanaanda izo barua za mwaliko za mchongo.
Mfano south korea wana program maalumu ya kuajiri wageni kipindi cha msimu wa kilimo zinakuwa ajira za muda miezi 3 mpaka 6.
Mimi Binafsi nimeshajaribu kuwashawishi Lakini nikichogundua wengi wanataka umwambie sehemu fulani kuna kazi inalipa vizuri nenda. Kuhusu passport atakwambia sina hela ya kufatilia passport lakini kila siku unamuona na nguo mpya . Vijana kujipambania kutafuta fursa nje ya nchi hawataki kabisa wanaona bora waendelee kuomba omba buku aweke mkeka 😅, labda serikali ijaribu kuwapambania kuwatafutia hizo fursa kama burundi inavyofanya
 
Kwanini mtu atake hati ya kusafiria aanze kufikiria barua ya mwaliko ya mchongo sikatai wengi wanafanya hivyo (kuandaliwa barua za mchongo)hatuoni kama ni wakati sahihi kwa mamlaka husika kupunguza viambata kwenye form za maombi ikiwemo na hili na vyeti vya kuzaliwa maana taarifa zote zimo kwenye kitambulisho cha taifa
 
Na utajiri wa chief godlove [emoji23]
Ukienda Botswana huko kuna walimu,madokta kitambo sana walichomoka
Miaka ya 97 huko mama zetu manesi wlkadhaa waliondoka huko ma UK,USA
Kizazi cha sahv cha singeli,kufatilia mambo ya kina mondi konde kubishana umbea wataweza wapi

Ova
 
Mtu kastaafu Jeshini anateuliwa kuwa Balozi ili akalete jipya gani ughaibuni![emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Yaani hii ni ajabu sana ubalozi inakuwa kama sehemu ya mtu kupumzika wakati inapaswa kuwa kinyume chake balozi hapaswi kulala yeye ndio jicho la nchi yetu katika nchi husika lazima achangamke kung'amua fursa mbalimbali na kuziweka wazi kwa watu wa taifa lake waweze kuzichangamkia na kuchochea ustawi wa taifa letu. Tazama jiriani zetu hasa Kenya wanavyochangamkia fursa ughaibuni katika nchi mbalimbali tofauti na sisi tumelala lakini hili halinishangazi sana ikiwa kupata tu hati ya kusafiri kizungumkuti.
 
Ukienda Botswana huko kuna walimu,madokta kitambo sana walichomoka
Miaka ya 97 huko mama zetu manesi wlkadhaa waliondoka huko ma UK,USA
Kizazi cha sahv cha singeli,kufatilia mambo ya kina mondi konde kubishana umbea wataweza wapi

Ova
Uko sahihi lakini zama zimebadilika na mambo mengi pia yamebadilika sera nyingi za mahusiano za nchi mbalimbali pia zimebadilika nafikiri sio sahihi sana kulinganisha nyakati
 
Picha linaanza kwenye kupata passport tuu, utaambiwa nenda ukalete cheti cha kuzaliwa cha babu mzaa baba sasa unajiuliza hivi nini maana ya kuwa na kitambulisho cha taifa (NIDA) kwa maana hiyo tuu inatosha kupata taarifa zote. Urasimu upo karibu kwenye kila sekta.
 
Kwanini kuwe na mazingira magumu mwanzo tu kwanza inachochea mianya ya rushwa hakuna aliyesema inashindikana kupatikana mtaani ni rahisi wengi tunaelewa swali, je kuna umuhimu gani wa sharti kama hilo kuwepo kwenye form za maombi kama kiambata kwanini tuendelee kuchochea mazingira ya kugushi nyaraka kusiko na afya yoyote kwa nchi yetu maana nia ya kubadilisha mfumo wa kutoa hati za kusafiria umetumia gharama kubwa sana sasa badala uwe na tija kwa nchi kwa kusaidia kuingiza mapato zaidi tunaona sawa tu idadi ndogo ya maombi na wachache wakipata hati.
 
Yaani nchi kama Kenya ni wiki iliyopita imesaini mkataba na USA, Germany na Qatar/ Saudi Arabia,kuexport human resource zao , kwenye kazi mbalimbali, zinazohitaji watu kwenye nchi hizo....Nyie Bongo endeleeni tu na siasa za kutelekeza nguvu kazi ya vijana wakibakia kuendelea kubakia kushabikia , bongofleva, Yanga/Simba na promotion za vijana kuendelea kubet tu Kwa bidii....... Kwa kweli safari yetu, bado ni ndefu na tutafika tumechooka.....
Agency za Kenya ni proactive sana.
Watoto wa kibongo waoga sana kwenda Uarabuni. Wanaogopa sana..
Lakini huko ndiyo pakupata mitaji na gateway ya kupata mitaji ya kuingia West. Tatizo wabishi na waoga sana!
 
Miongoni mwa vingi nimetaja hiyo barua kama mtu yuko na kitambulisho cha taifa chenye taarifa zote za mtu inakuaje tena unamuomba cheti chake cha kuzaliwa ina maana mifumo ya serikali haisomani ni mwendelezo ule ule wa mawazo ya kijima ambao hauna tija kwenye ustawi na taifa letu.
Ni kuweka kumbukumbu sahihi!

Kisa una Nida hivyo hutakiwi kupeleka cheti cha kuzaliwa?

Kuna watu wana Nida lakini taarifa zina chengana

Mfano
Majina hayafanani
Tarehe hazifanani

Hivyo pia ni taasisi mbili tofauti na majukumu tofauti pamoja na sheria na kanuni zinazo muongoza mtendaji ofisini kwake

Na sio kila Nida ina taarifa zote zinazo hitajika
 
Kazi nje zipo nyingi lakini ili upate kazi kirahisi lazima uwe na passport, lakini mtu akitaka passport hawezi kukosa maana wapo watu wanaanda izo barua za mwaliko za mchongo.
Mfano south korea wana program maalumu ya kuajiri wageni kipindi cha msimu wa kilimo zinakuwa ajira za muda miezi 3 mpaka 6.
Mimi Binafsi nimeshajaribu kuwashawishi Lakini nikichogundua wengi wanataka umwambie sehemu fulani kuna kazi inalipa vizuri nenda. Kuhusu passport atakwambia sina hela ya kufatilia passport lakini kila siku unamuona na nguo mpya . Vijana kujipambania kutafuta fursa nje ya nchi hawataki kabisa wanaona bora waendelee kuomba omba buku aweke mkeka 😅, labda serikali ijaribu kuwapambania kuwatafutia hizo fursa kama burundi inavyofanya
Jitahidi kuweka taarifa zake hapa ili watu waweze kupambana kwa walio tayari

Kama kuna site ya kutuma maombi na kama mwezi fulani ni mzuri kufanya maombi

Wewe fanya yako na wenye kufanya watafanya pia
 
Sahihi kabsa hati ya kusafiria tu kizungumkuti eti unaambiwa fomu za maombi uambatanishe na barua ya mwaliko mambo ya kijima kabsa haya mwaliko inawahusu nini vikwazo lukuki wakati kila raia mwenye uhitaji anapaswa kuwa na hati ya kusafiri pia ni chanzo kikubwa cha mapato hebu fikiria wizara ya mambo ya ndani idara ya uhamiaji ingetengeneza kiasi gani cha mapato kama kamishina na wasaidizi wake wakija na mkakati wa kutoa hati za kusafiria 2,000,000 kwa kila mwaka. Lakini unashangaa watu wako maofisini wanashindwa kuja na mipango kazi inayoeleweka kazi zinafanyika kwa mazoea bora liende rushwa ndo inazidi nchi inakosa mapato na fursa zinachangamkiwa na vijana wa nchi nyingine.
Wewe kama unataka paspoti na una wenzako wengi wengi unawajua nitafute. Hapa hakuna mambo ya kutoa laki 3. Unatoa pesa ileile ya serikali na ahsante utayojisikia kunipa.
 
Back
Top Bottom