Jaribu DRC, RWANDA au SA. Tatizo ni kwamba sirikari wanajua lakini hawatangazi kazi hizo.
Acha uongo , hakuna kampuni ya kukuajiri wewe kizembe hivyo kutokea Tanzania ,Marekani kuna kitu kinaitwa LMIA (Labour market impact assessment ) ,Hilo ni rungu lililoshikiliwa na serikali ya Marekani kupitia department of Labour , Hakuna mwajiri yoyote anayeweza kuajiri foreigner bila kupata hicho kibali LMIA na kinalipiwa hicho kaa ukijua ,yaani mwajiri analipa si chini ya 2000+ USD kukipata ili kukuajiri wewe foreigner ,na sio guarantee na hiyo fee ni nonrefundable ,LMIA anatuma maombi department of Labour na wakikataa hiyo pesa yake hairudi na hawezi kukuajiri , wewe na kazi yako hiyo ya sales ni mwajiri gani wa kugharamika kutoa pesa ili aajiri foreigner ambaye first of all ni liability kwa sababu ni mgeni wa mazingira inabidi apate training upya na wakati kuna wazawa hapo hapo for immediate hire ,Hakuna mwajiri wa kufanya biashara kichaa .K
Kuna chimbo la kazi abroad nimelistukia majuzi linaaitwa Indeed nimeapply kazi nyingi za sales na marketing kazi za kampuni za Arizona hapa Nina interview kama 4 za online ,
kama sijakosea mkuu ubalozi wa USA unatoaga nafasi kila mwaka uwe na degree yoyoteMi Nina degree ya kiswahili.natafuta connection huko ugaibhuni nikafundishe
Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
Na huu ndio ukweli, huyo uliyemtag kwa comment ya kwanza kama hajakuelewa achana nae.Kama kuna mtu hapa anabisha aingie leo Indeed au LinkedIn aaply kazi Marekani halafu atatupa mrejesho hapa , hutapata hata hiyo interview na pia sababu ni moja kubwa pia ,utahitaji World education system assessment result , mfumo wa elimu bongo na USA ni tofauti ,kama ni nafasi ya Proffessional job au trade / kazi za ufundi ni lazima hilo rungu likuhusu ,ni lazima ufanyiwe hiyo assenent ,kama elimu yako ulisomea Marekani hapo sawa ,ila kuna nchi ni exception ,mfano China na India hicho kizuizi hamna ,sasa ni mikataba waliyofanya hizo nchi mpaka mifumo yao ya elimu ukafanyiwa assement na wakapewa go ahead na kuwa categorised kama sawa na huko hizo nchi nyingine ,sasa ni mtu kamalizia India anaweza enda kufanya kazi USA ,UK nk bila kikwazo kama sisi ,
Serikali haikwepi wajibu wake kwenye hili suala
We jamaa IVI ata Indeed upo kweli watu kibao wanapata kazi kupitia umo ata Leo saa 11 jioni EAT nilikuwa nifanyiwe interview kupitia zoom sema nicaicancel ,we Tomaso nini😀😀Indeed kazi kibao za nje aswa US labda ungesema issue ya kuingia US ndo ngumu ila sio kufanyiwa interview mi ninazo interview kalibia 3 zote kutoka makampuni ya Arizona,Kama kuna mtu hapa anabisha aingie leo Indeed au LinkedIn aaply kazi Marekani halafu atatupa mrejesho hapa , hutapata hata hiyo interview na pia sababu ni moja kubwa pia ,utahitaji World education system assessment result , mfumo wa elimu bongo na USA ni tofauti ,kama ni nafasi ya Proffessional job au trade / kazi za ufundi ni lazima hilo rungu likuhusu ,ni lazima ufanyiwe hiyo assenent ,kama elimu yako ulisomea Marekani hapo sawa ,ila kuna nchi ni exception ,mfano China na India hicho kizuizi hamna ,sasa ni mikataba waliyofanya hizo nchi mpaka mifumo yao ya elimu ukafanyiwa assement na wakapewa go ahead na kuwa categorised kama sawa na huko hizo nchi nyingine ,sasa ni mtu kamalizia India anaweza enda kufanya kazi USA ,UK nk bila kikwazo kama sisi ,
Serikali haikwepi wajibu wake kwenye hili suala
Unasahau sirikari ina makubaliano mfano na SA kusupply walimu wa kiswahili.Mwambie anaetaka hiyo michongo sio mimi. Sio kazi ya serikali kukutafutia kila kitu mambo mengine ni kujiongeza wenyewe tu, nawajua watu zaidi ya 10 from TZ na KE waliofundisha lugha vyuo mbalimbali duniani, serikali has nothing to do with it, ni juhudi zako tu.
mm kaka nataka bandua ya mualiko nichek pmMimi nilipambana nikapata passport sababu nilimuomba jamaa Fulani anaishi Congo BC akaniandikia barua ya mwaliko.lkn changamoto inakuja kupata connection na pesa ya kuanzia yani kujilipua.hizo ndo changamoto nilipata Mimi kama kijana Nina miaka now nakimbilia 25 na nilitafuta passport na sijui lini nitatimiza ndoto zangu lkn kuwa na passport pia kunanifailijigi sana hasa napoiona kwamba na Mimi nimejalibu kwa kadili Fulani.kwahyo yeyote ambaye anashida na barua ya mwaliko aseme nimpe yeye atabadilishatu details na kuweka zake.
Passport 150000/= unaweka bando shilingi ngapi na kubet kwa mwezi kuingia inst na betting sites?Naomba kwanza kabla ya kutulaum sisi vijana unijumlishie Jumla ya gharama ya passport na visa na nauli ya safari kutoka Tanzania hadi Kuwait kwa mfano.
Baada ya hapo uje kutulaum sisi vijana
Very sad and exhausting brother. Viongozk wetu kwa makusudi na maslahi yao binafsi wanafanya mambo yanakuwa magumu, pasi na tija.Maoni fall on deaf ears. Sio kwamba hawajui ila hawataki. Nchi inayokataa uraia pacha kwa nguvu kabisa karne ya leo, nchi inayoogopa kutumia PayPal, what does that tell you? Kuna mtu haiamini paypal ukitoa bongo?
NALA ya mbongo kaitoa bongo sasa is headquartered Kenya, that speaks volume. That is a slap in the face. Ila wao wanaona fresh tu. Hakuna international comapny hata moja inataka kuwa na makao makuu bongo, sasa hadi balozi zote zinahamia Kenya miviongozi ya bongo inaona fresh tu. Ile nchi is doomed.
Mwl nyerere na CCM ndo walianzisha upinzani dhidi ya diasporaKwenye nchi zilizoendelea kwasasa kuna uhaba mkubwa wa vijana wa kufanya kazi lakini wakati huohuo kuna janga kubwa la vijana wasikuwa na kazi Tanzania. Pamoja ni jitihada nyingi za serikali za kusaidia vijana kupata kazi na kufanya shughuli za kilimo ni lazima vijana nao wajiongeze walau kuweka mikakati ya muda wakati serikali ikijipanga vizuri hasa kwenye viwanda na mashamba ya mikakati. Badala ya kushinda vijiweni huu ni wakati wa serikali kufikiria zaidi ya Tanzania kwenye mambo ya ajira.
Tatizo tofauti na jamii za nchi jirani kama Kenya na Uganda watu wengi Tanzania wameweka utamaduni wa kuaminisha vijana wakienda nje tu kutafuta maslahi eti sio wazalendo. Ni bora wabaki vijiweni na kupuyanga wakati hawana uwezo wa kuchangia chochote kwa familia zao na wazazi wao. Naomba mlielewe siongelei vijana wote lakini nacho sema hapa tusiweke madongo kwa wale wanaotafuta maslahi nje ya nchi. Je, kuna fursa zipi hasa na nashauri nini. Hii ni kwa wale vijana wasio na kazi wala vipato
1. Serikali msione aibu kuongea na kampuni kubwa za teknologia ambazo zinaajiri watu nchi nyingine. India mfano wanafanya kazi nyingi sana za nchi nyingine kuanzia engineering design, accounting, programming, computer coding, technology training. Sasa je, ni kwanini hakuna jitihada zozote za kuwezesha Watanzania waweze kuajiriwa wakiwa Tanzania. Nasema hivyo kwasababu mimi nipo USA na naona hizi nchi kuna watu wengi sana wanafanya kazi kutoka nchi nyingine. Kuna kampuni ya Houston, Texas ambayo ina wafanyakazi zaidi ya 100 na wanafanyia kazi India!. sasa hawa wametuzidi nini. Mawaziri wetu wa teknologia hata kujiangaisha au kufikiria haya hawafanyi.
2. Serikali iweke uhusiano mzuri na diaspora na kuwawezesha diaspora wenye nafasi za kiungozi kuweza kuajiri Watanzania. Tatizo kwasasa hakuna sheria ambazo ziko wazi mfano kama manager diaspora yupo Canada na anataka kumpa kazi kijana Mtanzania na afanyie kazi kutoka Tanzania je ni sheria gani za kikodi na uwazi zipo kwasasa ili yule mwajiri aweze kuwa na uhakika anafuata sheria? Je tunasheria za hivi au hatuna? mafao na kodi zinalipwa vipi?
3. Watanzania vijana wahangaikie kazi za muda. Nchi nyingi zina kazi za muda kuanzia kwenye kilimo, meli za wageni, hospitali, mahoteli.. na hata ujenzi. Vijana badala ya kushinda mitandaoni na kuendesha bodaboda kwa Tsh 10,000 kwa siku tumia muda wako kutafuta kazi nje. Hizi kazi ni za mikataba mwaka mpaka miaka mitatu halafu unaweza kurudi wakati serikali nayo imejipanga. Mjue tu miaka ya 1995-2000 kuna watanzania wengi tu walienda USA kwenye program ya summer camp. walitafuta wenyewe lakini vijana wa siku hizi ni wepesi kulalama badala ya kutafuta fursa.
4.Vijana tafuteni " mentor" au washauri wenye uzoefu. Kuna Watanzania Dunia nzima wewe ni kijana wa miaka 20's badala ya kulalama tafuta mtu mzima wa kukushauri ambaye anafanya kitu ambacho wewe unapenda. Tatizo leo mnashinda kufikiri na kutaka kuwa kama Diamond au Nandy badala ya kutafuta wataalamu au wafanyabiashara ambao unataka kuwa kama wao. Sio lazima wawe Tanzania. Jioulize Je una account ya linked? ume connect na watanzania gani ambao wewe unataka kuwa kama wao? linked ni bure kwanini hauja connect hasa kwa wasomi? Hata hapa vijana kuna watu wengi wakuwapa mawazo lakini mnakimbilia kupiga madongo!madongo yanakusaidia nini?
5. Vijana msisubiri serikali. Serikali haijawahi kusaidia vijana kama wakati huu lakini vijana wa huko nyuma miaka ya 1990's na 2000's walienda kutafuta vyuo na maslahi huko nje wenyewe na marafiki zao sio kwa msaada wowote wa serikali. Tatizo vijana mnasubiri sana serikali ambayo itachukuwa muda sana kuweka mambo ya ajira sawa. Nawashauri tafuteni kazi popote Duniani ilimradi unasaidia familia yako. Lakini usisahau nyumbani
Kukaa nyumbani vijiweni na kulalama siku hadi siku sio uzalendo. Na usijidanganye kuwa wewe ni mzalendo kuliko yule kijana anayetuma pesa kusaidia familia yake.
Nishatoa ushauri huu
Ubunifu ni muhimu sana kwa nchi. Ushauri wangu huu ni serious sana kuliko watu nwengi wanavyofikiria.
Mimi ni diaspora hapa USA naona jinsi ambavyo kazi nyingi za technolojia zinafanywa kutokea India. Sasa najiuliza kuna ugumu gani ya vijana wetu wanaomaliza shule na kufanya kazi hizi kutokea Tanzania? inawezekana kabisa lakini kunatakiwa kuwa na makubaliano na hizi kampuni.
Nashauri serikali ifanye mwaliko wa hawa maguru na wakubwa wa hizi kampuni ili wafungue data center Tanzania waweze kuajiri wataalamu tofauti hasa kwenye teknolojia. Tusione aibu kuandikia barua na kualika hata kama wakisema hawana muda tunaweza kubahatisha mmoja.
Niongezee tu kwenye soko la hisa za Marekani 50% ni kampuni za teknolojia hizo hapo ni thamani za kampuni mfano Apple hapo ni $T2.3 na Oracle ni $240B
Larry Ellison-Oracle Corporation
bol Company Cap Rank
1-27-23Market Cap
1-27-231d Chg
1-27-231m Chg
1-27-2312m Chg
1-27-23AAPL Apple 1 2,311.0 1.4% 12.2% -8.3% MSFT Microsoft 2 1,848.0 0.1% 4.7% -17.2% GOOGL Alphabet 3 1,294.3 -0.9% -1.1% -34.6% AMZN Amazon 4 1,042.6 -1.6% -10.6% -48.1% BRK-A Berkshire Hathaway 5 682.8 0.0% 1.7% 1.9% TSLA Tesla 6 561.8 11.0% 63.0% -35.6% NVDA Nvidia 7 501.0 2.8% 44.2% -7.2% TSM Taiwan Semiconductor 8 483.9 -0.2% 25.5% -19.8% V Visa 9 477.2 3.0% 12.2% 12.3% XOM ExxonMobil 10 476.1 -1.8% 4.9% 53.9% UNH UnitedHealth 11 454.1 -1.3% -8.6% 5.3% JNJ Johnson & Johnson 12 439.8 -0.4% -5.2% -1.4% JPM JPMorgan Chase 13 411.6 0.2% 6.5% -3.4% META Meta 14 397.9 3.0% 29.8% -48.5% WMT Walmart 15 386.5 0.8% -0.4% 5.5% MA Mastercard 16 359.6 -0.9% 8.1% 6.7% CVX Chevron 17 347.0 -4.4% -0.1% 32.6% PG Procter & Gamble 18 331.6 -0.4% -8.7% -11.7% LLY Eli Lilly 19 325.1 -1.7% -6.2% 44.5% HD Home Depot 20 322.8 0.9% -0.9% -11.1% BABA Nvidia 21 313.4 -1.8% 31.7% 5.9% BAC Bank of America 22 284.4 0.3% 9.0% -22.0% MRK Merck 23 267.2 -1.4% -6.0% 30.8% ASML ASML 24 266.6 -2.4% 24.2% 5.2% KO Coca-Cola 25 261.6 -0.5% -5.8% 1.4% ABBV AbbVie 26 258.7 -0.8% -10.3% 7.6% AVGO Broadcom 27 247.0 -1.3% 6.8% 9.0% PFE Pfizer 28 245.8 -1.0% -14.4% -18.0% ORCL Oracle
Tesla-Elon Musk
Microsoft-Satya Narayana Nadella
Alphabet-Google-Sundar Pichai
SAP CEO Christian Klein
IBM CEO Arvind Krishna's
Nimekusoma mkuu ni kweli hata mimi niliapply kazi sana za electrician indeed na sijawahi kupata kumbe iko ndio kigezo arafu kingine hawa jamaa awaamini elimu za bongoKama kuna mtu hapa anabisha aingie leo Indeed au LinkedIn aaply kazi Marekani halafu atatupa mrejesho hapa , hutapata hata hiyo interview na pia sababu ni moja kubwa pia ,utahitaji World education system assessment result , mfumo wa elimu bongo na USA ni tofauti ,kama ni nafasi ya Proffessional job au trade / kazi za ufundi ni lazima hilo rungu likuhusu ,ni lazima ufanyiwe hiyo assenent ,kama elimu yako ulisomea Marekani hapo sawa ,ila kuna nchi ni exception ,mfano China na India hicho kizuizi hamna ,sasa ni mikataba waliyofanya hizo nchi mpaka mifumo yao ya elimu ukafanyiwa assement na wakapewa go ahead na kuwa categorised kama sawa na huko hizo nchi nyingine ,sasa ni mtu kamalizia India anaweza enda kufanya kazi USA ,UK nk bila kikwazo kama sisi ,
Serikali haikwepi wajibu wake kwenye hili suala
Ina maana ulikuwa hujawahi kufikiria hili before? Tafuta kazi popote kijana ili mradi iwe