Je, ninunue aina ipi na nizitunze vipi cadet na jeans zikae walau mwaka?

Je, ninunue aina ipi na nizitunze vipi cadet na jeans zikae walau mwaka?

Siri ya jeans na cadet ni kufuliwa mara chache ,mimi nguo zangu zote midosho sina jeans wala cadet ya elfu 30 lakini hiyo midosho mingine ya tangia ,2018 mpaka leo navaa na ipo poa tu , nguo hasa za dukani hutakiwi kuifua mara kwa mara ,vaa fua atleast mara moja kwa wiki mbili ,inatakiwa unakuwa na midosho mingi inaivaa Kwa kualternate ila kama ndio unanunua halafu unakaa na kazi za kuchafuka sana halafu unatakiwa uwe unafua kila siku ,hiyo nguo haikai
 
Sure nilinunua Cadet 2 shs 55,000 kila moja. Eti hazi chuji. Kumbe ni za hovyo tu.
Harafu cha ajabu kama mimi nanunua kawaida tuu hapo Bree Street kwa Wa Ethiopian Jean zao ni Rand 200 kama 28,000 na kadet wanauza bei hiyo hiyo mazee ni ngumu na Kadet kweli haifubai mpaka unaweza kugawa mtu akadhani umempa nguo mpya kumbe ina siku kadhaa mwilini Bongo tunauziana vitu having ubora harafu bei ghari na tunaona Ujanja huo ..nguo haina hata level wahuni wanakwambia 60,000 hiyo hela unapata Levis 350 mbili mpya au Wrangler...
 
Kuna kale karaha mtu upo huko katika shughuli zako umevaa nguo bado zipo fresh, Sio unapita sehemu nguo imepauka/rangi zimefifia yani hata mtu akikuangalia mara mbili unajua tu hapa kipengele ni nguo.

Nilinunua jeans 2 na cadet 2, kwa ufinyu wa bajeti yangu nilinunua jeans elf 25 kwa pair na cadet zilikuwa elf 28 kwa pair.

Nilitegemea walau zinivushe huu mwaka lakini hali imekuwa ndivyo sivyo, kwa sasa naanza kuona hata soo kuzivaa.

Nawaza hapa nikanunue cadet na jeans aina ipi ambazo zitaweza kunivusha salama huu mwaka na pia nizitunze vipi.

Jamani nguo zinanipasulia bajeti, naombeni ushauri please.
Kadeti au nguo yoyote ukitaka isichoke ununue nyingi ili uwe unabadilisha na kuzipumzisha. Jeans 2 na kadeti mbili huwezi kutoboa mwaka labda kibishi miezi minne tu

Kadeti nenda Kariakoo ununue kadeti za elfu 18 sio za 15 (bei ya jumla) ukichukua kadeti za laki moja unatoboa miezi hata 9 na kabla hazijachoka unachukua nyingine ili kuzisitiri zile za mwanzo

Naishi na kanuni hiyo
 
Ushasema mtumba!
Hapo unataka masharti gani kutunza mtumba...!?

Huo mtumba bei yake ukiwa mpya ulaya inaweza zidi hata laki 5 za kibongo!
Ambapo utunzaji wake lazima ufuate masharti!
Tatizo wabongo tunavaa nguo kimazoea kwa kuwa nyingi ni bei rahisi hivyo tunaona vyovyote tutakavyozifanya ni sawa tu!
Cardet Og ya Boss ulaya ni zaidi ya laki 7 za kibongo, inunue uone utapewa masharti gani ya kuitunza ili iendelee kubaki na ubora wake!
Mtumba namaanisha quality, nimekupa mfano hapo juu miaka ya late 90 kuna duka lilikuwa linaleta nguo quality, zilikua ni gharama lakini worth it,
Halafu hata huko ulaya kuna classes za nguo si kila cadet ni ta laki 7 kama unavosema zipo affordable na ubora wa kutosha ,
 
Tafuta wahuni smart wakuelekeze chimbo lenye mitumba Grade A....
nguo unakaa nayo mwaka ipo vile vile
 
But sasa si miaka ya 90!
Vitu vya kale kwanza kulikuwa hamna copy na fake! Miaka hii ya sasa idadi ya watu imeongezeka, viwanda ni vingi na watu wanataka vitu cheap!

Nilichozungumzia ni resrictions za matunzo!

Hiyo mitumba kama waliokuwa wakitumia wangekuwa hawafuati kanuni za matunzo, zisingefika huku Africa!
Tatizo wabongo mna ubishi mwingi usio na faida!

Kwa kuwa watu mna mazoea ya kununua na kuvaa tu, zaidi ikichafuka ufue na kuanika ikauke na kupiga pasi inyooke basi!
 
Mkuu hata miaka hii bado kuna vitu vizuri sana na kwa bei nafuu ,shida ni kuwa wafanyabiashara wameingiwa na tamaa na kutuletea vitu low quality.
Juzi kati tu hapa nimeagiza heat gear t shirts, zilikuwa zinauzwa kwa mafungu ebay , tano kwa dola 90 plus shipping, under amour ,nike na addidas , very high quality na naamini nitavaa kwa miaka kadhaa zikiwa na ubora wake .
Nguo nzuri zipo ila wafanyabiashara wanasababu zao za kuleta midosho
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]jeans zetu hizo za 13k, 14k etc. Namimi ninayo moja saiv imekuwa bwanga hata suruali za kitambaa zinasubiri wakati kipindi naichukua kkoo ilikuwa modo safi kabisa.
Hatari yani
Nilibana mara ya kwanza, nimevaa siku ngapi sijui, sijaamini....imekuwa bwanga la hatari.....sijui wanatumia material gani hawa jamaa kutengeneza hizo jeans 🤣
 
Tafuta wahuni smart wakuelekeze chimbo lenye mitumba Grade A....
nguo unakaa nayo mwaka ipo vile vile
Mitumba ni option nzuri sana, na kuna nguo imara sana , kuna shati nililiotea nlikaa nalo hadi likachanika , halikupoteza ubora .
Shida ya mtumba inabidi upoteze muda kutafuta nguo na hazinaga uhakika wa kupata aina moja ya nguo.
 
Hatari yani
Nilibana mara ya kwanza, nimevaa siku ngapi sijui, sijaamini....imekuwa bwanga la hatari.....sijui wanatumia material gani hawa jamaa kutengeneza hizo jeans 🤣
Hili ndio tatizo mtoa mada anaongelea , nguo hazina ubora kwa thamani ya pesa zinazonunuliwa .
Ni afadhali uniuzie shati hata laki moja lakini nikawa na uhakika kuwa nitalivaa kwa mwaka , kuliko kununua shati kwa 20,000 , halafu ukifua mara moja linapauka .
 
Shida bongo uaminifu ndo chenga shati la 20 atakuuzia 80 na kukwambia og
 
Hatari yani
Nilibana mara ya kwanza, nimevaa siku ngapi sijui, sijaamini....imekuwa bwanga la hatari.....sijui wanatumia material gani hawa jamaa kutengeneza hizo jeans [emoji1787]
Halafu unakuta ni nyepesii. Siku ya kwanza kuifua ilitoa rangi nyingi maji yakawa meusi tiii mpaka nikaogopa. Aisee serikali iingilie kati hili suala[emoji16][emoji16]
 
Nani kakudanganya nguo kali hazina masharti?

Wewe nguo huzijui wewe!
Umezoea kuvaa matambara ya Tandika unafulia maji ya chumvi na kutumia sabuni za magadi!

Hivi unaijua suti Og za brand kama Giorgio Armani ama Brunello Cuccinello(ambapo naamini ndio kwanza unaona hizi brand leo) ni za kufua kwa maji ya chumvi na kuanika kwenye mawe ama majani...?

Wewe nguo kali huzijui ndio maana unasema hazina masharti!
Wee endelea kuvaa matambara ya tandika huko ndio hayana masharti!
Sawa , ila kufokeana fokeana sio issue
 
Back
Top Bottom