Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Kuna wakati kukaa kimya huwa ni hekima. Lakini kukaa kimya huku mkiangalia kichaa akiwa ameshika panga, anawafyeka mmoja baada ya mwingine ni upumb.avu.

Wameua watu, miili wanatupa kwenye mito na kwenye fukwe za bahari, tupo kimya. Eti tunasema Mungu anajua.

Mungu anachojua ni kuwa ametupatia akili na nguvu za kupambana na vichaa. Yeye alifanya kazi kutuonesha kuwa mafanikio ni kwa kufanya kazi.

Wametaka kumwua TL, tupo kimya. Wameteka watu, tupo kimya. Wanakamata watu na kuwaweka korokoroni kama watakavyo, tupo kimya.

Hakika hata huku mbele ya Mungu, sote tutahukumiwa sawa na wauaji na watesaji. Wakati wao watahukumiwa kwa mauaji na utesaji, sisi tutahukumiwa kwa kushindwa kutekeleza wajibu wetu wa kujilinda na kuwalinda wenzetu. Hakuna ahera wala mbingu ya mtu mwoga na mzembe.
Waafrica hasa vyama tawala wanapenda sana vurugu!! Hawavumilii wananchi kuwakataa kwao ni bora kuua kuliko kukataliwa ndani ya box la kura. Huyu buana anajinasibu kupendwa kwa nini isiwe chaguzi huru?! Na leo najuwa kinondoni itatekwa kama walivyofanya Mwz
 
NO WAY ASKARI HAWANA MAKOSA NI LAZIMA WAHAKIKISHE AMANI NA UTULIVU VINAPATIKANA!
Tusijiingize katika anga zao jamani!
Rip Aqulina!
Pumbavu, askari hawana makosa kivipi? Binti anatia gani mpaka apigwe risasi? Na kwanini iwe risasi kwa raia wasio na silaa yoyote?? Huu upuuzi ukome Mara moja.
 
Kwanini nihitaji kibali kutoka kwa aliyegandamiza haki yangu ili niipate haki hiyo?
Ndiyo maana mlistahili risasi za moto...wauaji wakubwa nyie!!Hata lissu ana Mungu wake tu kwa mipango yenu haramu hiyo. siku si nyingi mtaumbuka na kuwajua viongozi wenu vizuri ni watu wa aina gani....shubaaaaaamit!Kupiga mpige nyie vilio mlete upande wa pili Hatukubali!CCM Oyeee×8
 
Ndiyo maana mlistahili risasi za moto...wauaji wakubwa nyie!!Hata lissu ana Mungu wake tu kwa mipango yenu haramu hiyo. siku si nyingi mtaumbuka na kuwajua viongozi wenu vizuri ni watu wa aina gani....shubaaaaaamit!Kupiga mpige nyie vilio mlete upande wa pili Hatukubali!CCM Oyeee×8
Tulistahili risasi za moto?

Ni vema na haki.
 
Kuuwa ni kosa la jinai hasa pale unapo uwa kwa makusudi sio kwa kujihami. Sidhani kuwa Aquilline alishambulia polisi. Kama raia inaniuma sana binti huyu kupigwa risasi. Tumetoka kwenye wimbi la watu kupotea sasa tunaingia kupigwa mapanga au risasi mchana kweupe tena hadharani. Ninani anaye dhamini haya maovu?
R.I.P Aquilline
 
huyo denti alikua anatafuta nin huko kwenye mikutano ya siasa wakati wenzie wako kwenye maandalizi ya mitihani?
Alikwambia alikuwa kwenye mkutano wa siasa? Binti alikuwa kwenye usafiri/ daladala, risasi ilimpatia kwenye chombo cha usafiri kwa uzembe wa polisccm.
 
huyo denti alikua anatafuta nin huko kwenye mikutano ya siasa wakati wenzie wako kwenye maandalizi ya mitihani?
Kwahiyo kwenye mikutano ya siasa watu wapigwe risasi tu? Haya maswali yanweza kuulizwa na mjinga tu na sio mtu mwenye akili timamu.
 
Tatizo tunawachekea mno.
Polisi tunaishi nao,tunakokaa sisi ndiko wanakokaa wao.
Hukumu zao zimefukiwa na ujinga wetu.
Wakishaacha hizo bunduki zao vituoni wanarudishwa na bodaboda zetu na sisi ndio tunawarudisha .
Wakija baa tunakaa nao na sisi ndio tunawachomea nyama baada ya kupokea rushwa zetu toka kwa bodaboda.
Wanapambana kutafuta mademu mitaani na sisi ndio tunawafanikishia.
Wanauguliwa na watoto zao,mama,baba na ndugu wengine na sisi tunawatibu hao ndugu zao, jamii inashirikiana nao katika kila jambo,furaha na huzuni .
Polisi wakifika siku wakafahamu kuwa mtaani wakiamua kuanzisha operation ngumu dhidi yao,dhidi ya familia zao hapatakalika.
Tutauana bure wote sisi Watanzania.
Pumbavu kabisa
 
Watanzani bhana hivi mnadhani Congo,burundi,sudani hakuna mahakaa!?,ts tie for pay back hivi nyie amchoki!?mahakani ni kujipotzea muda,Kesi ya ngendere awezi kupelekewa nyani!!
 
Wanabodi,
Kwanza nitoe pole kwa kifo hiki cha malaika huyu
454a637916def479540d0fc946e0cc85.jpg


Jee mnajua Jeshi la Polisi Linaweza kushitakiwa kwa kifo hiki cha uzembe na wahusika kuhukumiwa kama kifo cha Mwangosi, lakini pia serikali ikashitakiwa kwa kesi ya madai na kuhukumiwa kulipa fidia kwa familia ya marehemu?.

Kuna mazingira ambayo polisi wanaweza kumuua raia wa kawaida katika polisi shootout na polisi wasiwe na criminal liability kama tukio hilo linahusisha matumizi halali ya risasi za moto kwa mujibu wa miongozo yao, lakini tukio lile ni kuthibiti riots, hivyo tangu lini jeshi la polisi linatumia risasi za moto kuthibiti riots za watu wasio na silaha zozote badala ya kutumia rubber bullets?!.

Tena kuna ushahidi wa kutosha na usiotia shaka, mara nyingi uvunjifu wa amani unasababishwa na polisi wanaodhibiti maandamano hayo!. Kama polisi wangesimamia na kuwapa ulinzi Chadema katika kufuata viapo vyao ili wakiona vurugu ndipo waungilie, what did they stand to loose?. Kilichotokea ni uzembe tuu wa polisi wetu na hakuna excuse yoyote itakayo weza kutolewa ku justify uzembe huu wa jeshi letu la polisi kupoteza maisha ya an innocent civilian just like that!.

Poleni sana, wazazi, wanafunzi wenzake, ndugu, jamaa, marafiki, wana Kinondoni wote na wote walioguswa na kifo hiki.

Hii ndio gharama ya demokrasia ambayo Watanzania wanalazimishwa kuilipa ili tuu fulani ashinde!.
Mungu yupo na haya anayaona!.

Rip, mwanafunzi wa Mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM),Aqulina Akwilini Baftaha
Nisahihishe, pale hakukuwa na riots ila ni matembezi ya amani
 
Tena kama yule alokuwa anasema wamedhibiti sijui fujo, nilitamani niwe mchawi nimuue hapo kwenye TZ washangae tu kafa.
 
POLISI WA TZ MI NILISHASEMA, HAWATUMII UBONGO WAO, WANAENDESHWA KAMA NA REMOTE NA NGUVU NDYO KIPAUMBELE. HUYO BINTI HATA INGEKUWA YUPO KWENYE RIOTS, KWA ULAIN HUO UNAMDHBITIJE KWA RISAS YA MOTO KAMA SYO UNGESE
 
Wa kulaumiwa ni Chadema....kwani viapo vinapatikana kwa kuleta fujo na maandamano haramu....Chadema ndiyo Chanzo cha kifo cha huyo binti na Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi
Jiulize kama NEC wangetoa vile viapo kwa wakati haya yote yasingetokea..

Alafu nguvu kubwa ya nini kwa raia ambao hawakuwa na chochote cha kutishia amani..
 
I shall continue to serve until my last breath and when I die, I can say, that every drop of my blood will invigorate India and strengthen it. In:Selected Speeches of Indira Gandhi: January 1, 1982-October 30, 1984.
Hiyo speech ni mfano tosha kwa Binti huyu aliyeuwawa wakati wa harakati zake za kidemokrasia
 
Back
Top Bottom