Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Umefika wakati sasa watanzania tunaochukizwa na matendo ya serikali ya CCM kwa msaada wa Polisi Tanzania, tuanze kuwatenga hawa watu.

Tuwatenge kwenye maisha yetu ya kila siku. Hivi ndivyo Magufuli anataka.

Mimi nilishaanza siku nyingi sana. I don’t roll with any CCM associate or PT associate. Kuna siku lizee limoja la CCM na manguo yake liliomba lift, nikaliambia lift hupati kwa sababu ya manguo yako ya kinyesi.

Tuyatenge haya mauaji na makatili.
 
Huyu Rais tuliye naye hakika laana ya mauaji ya yule mwanafunzi asiye na hatia wa UDSM itamuandama katika maisha yake yote

Tumapopata mkuu wa nchi ambaye anashehrekea umwagikaji wa damu wa wananchi wake hakika kama Taifa tunakwenda kubaya sana.

Misingi ya Umoja ambayo Taifa hiki liliachiwa na muasisi wa Taifa hili Mwalimu Nyerere, inaporomoka kwa kasi ya kutisha

Mimi naaza kuwa na wasiwasi inawezekana akawa anatumiwa na taifa jirani kuleta umwagaji damu katika Tanzania, Tanzania imekuwa kisiwa cha amani kwa muda mrefu, inawezekana wanatuonea wivu kwa stability yetu, sasa wanamtumia jamaa alete umwagaji damu katika nchi yetu. Urafiki wake na Kagame unatia mashaka makubwa sana. And he simply does not care. we have to be vigilant with this guy, jicho la tatu linatakiwa ikiwezekana apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye.
 
huyo denti alikua anatafuta nin huko kwenye mikutano ya siasa wakati wenzie wako kwenye maandalizi ya mitihani?
wewe ulimuona kwenye mkutano ata angekuwa kwenye mandamano alipaswa kuuliwa !?
kabisa ww angekuwa mdogo wako ungesema hayo jinga kabisa ww au angeuliwa mama yako ungejisikiaje ww huna mtoto unajuwa mzazi anatumia nguvu kiasi gani kulea na kufundisha kabisa ww !!
 
Nimeguswa sana na kifo cha huyo binti. Mkurugenzi ndio chanzo cha hicho kifo kwa kusababisha fujo usiyo ya lazima kwa kutofuata sheria ,imagine angefuata sheria na kuwaapisha mawakala hizo vurugu zisingetokea. Alitumia sheria ipi kukataa kuwaapisha na baada ya vurugu na mauaji alitumia sheria ipi pia kufanya kazi ya kuwaapisha. Alaaniwe huyo shetani kwa jina la Yesu kwa kusababisha vurugu na kifo. Tena alaainiwe yeye na familia yake. Mungu alimpa dhamana lakini amelewa madaraka na sifa kama yuda iskarioti kwa kupenda fedha . Wote tulioguswa na msiba huo tuseme ameni.
 
Kaka izo unazo ziita risasi za mpira nazo zinaua. Kinachotakiwa Jeshi la polisi lijitaidi kwenye mafunzo namna ya kutumia hizo risai ili kuepusha vifo visivyo kusudiwa. Kwa ujumla sehemu yenye vurugu na ikatokea matumizi ya risasi jitahidi kwa kadri utakavyoweza uwe mbalisana na eneo hilo. Uwezi jua uyo anaye tumia iyo silaha akili na weledi wake upo vizuri kiasi gani.
 
Kama chadema wangegomea chaguzi haya yaaingetokea,lakini kwa kuwa walidhamirimia kuharibu nchi wakaona liwalo na liwe
Wenye akili wanajua huu uchaguzi chadema hawashindi hata waandamane uchi
Kumbe lengo lenu cdm waugomee lakini wakagoma sio pamoja na vijibarua vyenu vya uzushi mitandaoni sio? Baada ya option moja kufail mkaona mje na la kuua kwa risasi lakini bado mnashindwa sio? Lililobaki ni kumtangaza mshindwa kuwa mshindi sio? Sioni kama maoptions yote haya kushinda bali kujiaaibisha na kujidhalilisha mbele za umma mnaojidai kuuongoza ilihali mnakataliwa kila upande! Msijidanganye bali kubalianeni na uhalisia kuwa hampendwi na hamuungwi mkono na wenye kujitambua! Na safari hii wabomoleeni nyumba zao zote kuonyesha hasira zenu! Wauaji ninyi.
 
Kuna wakati unaweza ukawa na akili lakini aina ya watu unaokaa nao wakakufanya ukatokwa na akili.eti mtu analaumu chama cha upinzani kwa tukio la mtu kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala,anyway Rip Sis.
 
Ndio mkome sasa
Nani aliwaambia mchague Rais muongo

Tatizo unadhani tulimchagua basi, ni udhaifu wa kitaasisi unaozikumba nchi nyingi za kiafrika, tume inatangaza wanayemtaka au aliyepangwa kabla. Tunaposema udhaifu wa kitaasisi hatusemi polisi peke yake ni pamoja na tume ya uchaguzi, TAKUKURU na vyombo vingine
 
huyo denti alikua anatafuta nin huko kwenye mikutano ya siasa wakati wenzie wako kwenye maandalizi ya mitihani?

Maswali ya kizembe kama haya ndio yanaendelea kufuga upimbi wa hawa polisi. Kwanza, mwanafunzi alikuwa kwenye daladala katika mizunguko yake binafsi. Pili, hata kama alikuwa eneo la tukio kwasababu ya kufuatilia lala salama ya kampeni halali za vyama, bado polisi hawakustahili kurusha kiholela risasi za moto. Tunatakiwa tupinge uzembe na uonevu kama huu, na sio kuuliza maswali yanayoonyesha dhahiri kwamba yana tetea polisi wasio fanya kazi yao kwa weledi.
 
Back
Top Bottom