Wanajamii,
Nitaendelea kuyakubali maneno ya rais wa zamani wa Marekani Barack Obama aliyesema Africa does not need strong people but rather strong institutions. Haya maneno watu wanayachukulia poa lakini ni maneno yenye mantiki kubwa.
Moja ya sifa ya madikteta wanapopata upenyo wa kuingia kwenye madaraka huwa ni kuzidhoofisha taasisi, Huyu Magufuli alipoingia madarakani moja ya kazi aliyofanya ni kulidhoofisha jeshi la polisi, cha kwanza ilikuwa ni kumtoa Ernest Mangu na Kumweka Simon Sirro, inasemekana Mangu alikuwa hakubaliani na maagizo ambayo yanaenda kinyume na taaluma yake.
Alichofanya mheshimiwa ni kummweka puppet ambaye atampeleka kama gari bovu. Matokeo yake tunayaona jeshi la polisi linafanya kazi ya ukandamizaji na ukatili.
Kila kukicha jeshi ili limfurahishe rais lazima watende ukatili kwa raia especially wafuasi wa vyama shindani kama jana kumuua binti wa chuo kikuu. Kwa sasa jeshi halifanyi kazi kitaaluma wamepoteza nguvu ya kuwa taasisi inayojitegemea ili raia watendeane haki. Pia limeingia mtego wa siasa kuwa msaidizi wa ccm wakati katiba na sheria haziwataki kufanya hivyo.
Kama wakuu wa polisi watasoma post hii naomba wampelekee Sirro ajitathmini upya ni namna gani inaweza kurudisha nguvu yake ya kitaasisi ambayo imeporomoka kwa kasi ya kutisha. Nchi imejaa hasira kwa utendaji usio wa haki na ukatili.