Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Hivi kulikuwa na ulazima wa kufanya maandamano hayo?yalifanyika muda gani?wakati wa saa za kazi au baada ya ofisi kufungwa?kwa nini wanasiasa hawaleti watoto wao kwenye maandamano?nionavyomimi wote wanapaswa kulaumiwa!
Kwa maoni yako CDM wangepataje hivyo viapo vyao?
 
NO WAY ASKARI HAWANA MAKOSA NI LAZIMA WAHAKIKISHE AMANI NA UTULIVU VINAPATIKANA!
Tusijiingize katika anga zao jamani!
Rip Aqulina!
Wewe kama hao wanaotumia risasi za moto kutawanya maandamano! What if ikithibitika kuwa marehemu alikuwa mpita njia? Waweza kutetea upuuzi huu akiuawa mwanao asiye na hatia yoyote kisa unamuunga mkono na kumfurahisha mtu mmoja tu? Nenda kwenye maombi!
 
Ww jamaa nazan una matatizo sasa huyo mwanafunzi alikuwa kwenye dala dala anarudi zake home hajui chochote ile risasi imepiga dala dala na kwa akuwa alikuwa amekaa ndiyo hiyo risasi imempata ( kumbuka vurugu za polis na chadema zimetokea pale mkwajuni yaani pembeni ya rami tu kwahiyo daladala nyingi zilikuwa zinapita hapo) au siku hizi maandamano hufanyika kwenye gari
Utapigaje Risasi ovyo ovyo hii nchi haikumbolewa kwa mitutu ya bunduki. Kwa hii mbegu inayopanda inazidi kumea kila uchao mwisho mazoea.
 
Mimi kama mzazi ambaye nina binti wa kike na kiume hii ishu imeniuma sana.

Mungu halali yupo macho muda wote na haya anayaona.

R.I.P kid..
 
namsikia Adam kambaya akisema kuwa mawakala wao wamezuiwa kuingia kuwa wasimamizi hawajapata barua, na kura zimepigwa bila mawakala wa chama chake, huyo ded huyu kuna kitu anakitafuta
 
huyo denti alikua anatafuta nin huko kwenye mikutano ya siasa wakati wenzie wako kwenye maandalizi ya mitihani?
Hivi ni wanachuo wote hukaa hostel? Acha kuhukumu kwani yawezekana alikuwa anarudi kwenye makazi yake mtaani au alikuwa anatafuta mahitaji yake na hata kama alikuwa anaandamana, kwanini apigwe risasi ya moto badala ya plastic? Fikiri tena na kisha uwaze kama kuna polisi aliyeshambuliwa na waandamanaji wale!
 
Hi ilipangwa. Iweje tayari mmepata picha yake, kwani aliwaaga wakati akienda kufanya fujo? Ni mtoto gani wa shule anajihusisha na siasa badala ya kusoma? Hilo la Mahakamani unamwuliza nani, si ulipita shule? Hawakukusomesha kuwa hiyo ndiyo kazi ya Mahakama, unatuuliza kututania au kutujaribu? Mbona Mbowe humuulizi, kwa nini hakuenda mahakamani?
Unaishi Kremia au Luthinia? Unajigeuza kenge mchana kweupe. Unaulizia picha? Unaijua mitandao ya kijamii? Kama hujui nenda kamuulize nyanya yako.
 
Ila wakumbuke dunia tunapita haya unayoyafanya hapa utaenda kuyajibu mbele ya haki tena peke yako kwenye uzima wa milele
RIP
 
Siku hizi naona mauaji yamekuwa ni sehemu ya maisha ya watz hii ni hatari kwa kweli.

Ina maana wananchi hawana mtu wa kwasemea kuhusu haya mauaji ama!!

Watz wenzetu wanapigwa risasi na hata wengine kuuawa hakuna anaejali!!

Hakika ipo siku.
 
Narudia kauli yangu na sitaacha kuisema kauli hiyo *ipo siku watanzania watachoka na watadai haki kwa nguvu bila woga wa kupigwa risasi* ngoja serikali ijifanye kipofu saivi ndo siku ikifika watajua
 
point of correction ! [HASHTAG]#pascal mayalla[/HASHTAG] huyu mwanafunzi ni wa Chuo cha Taifa cha usafirishaji (NIT) kwa taarifa zilizopo alikuwa anasoma Procurement $ Logistics mwaka wa kwanza
 
It's real sad, sidhani kama watapelekwa popote maana Tanzania ya sasa ipo on behalf of minority, polisi wanapokea order kutoka juu.. Pain
 
NO WAY ASKARI HAWANA MAKOSA NI LAZIMA WAHAKIKISHE AMANI NA UTULIVU VINAPATIKANA!
Tusijiingize katika anga zao jamani!
Rip Aqulina!
Are serious??? Polisi hawana makosa?? Ni Sheria gani inawaruhusu kuwashambulia na kuua watu wasio na hatia?? Jitafakari mkuu hapa lazima Polisi walaumiwe hakuna kukwepa lawama hapo
 
Back
Top Bottom