Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Uko sahihi kabisa Serikali ishitakiwe na mbowe pia ashitakiwe kwa kuhamasisha maandamano yasiyokuwa na kibali.
Upo sahihi ila umesahau aliyesababisha/ waliosababisha hayo maandamano kuwepo,ukumbuke yalikuwa ni maandamano ya kushinikiza kutolewa hati za viapo ambazo hadi wakati huo zilikuwa hazijatolewa kwa taratibu za kawaida.
 
Chadema walaaniwe kwa Kuwa sehemu ya sababu ya kifo cha binti huyu.....!!Polisi walikuwa katika sehemu yao majukumu yao kulinda amani Baada ya Chadema kuivuruga.
Mkuu jitathimini kwa kina utagundua umekosea sana, kwa hiyo amani iliyo vurugwa na chadema itulizwe kwa dhana za kivita?? Mkuu hao chadema walikua wanataka haki zao. Na ni ccm ndio wamebana haki za wananchi.
 
Dah inasikitisha sana.... Sijui haya yoye yanafanyika ili wanufaike na nini katika hii dunia.... They think wataishi milele? Mungu anawaona
 
Walipewa na nani ruhusa ya kuandamana.....!? Kwendeni zenu msiopenda kuukabili ukweli.eti chadema hawamiliki silaha....
Maandamano na mikusanyiko duniani kote haihitaji ruhusa ya yeyote! Kasome katiba ya jmt kisha urudi hapa! Isitoshe, hii fallacy of generosity yako kuwa cdm wanastahili lawama sio sahihi kwani kuna victim mmoja muhimu sana unamuacha ambaye angetimiza majukumu yake inavyopasa kisheria na kiutaratibu haya yote yasingelitokea. Ni bora huyo victim akajitokeza na kuomba radhi kwa madhila aliyoyasababisha kwa umma.
Igp, rpc, mkurugenzi wa nec na manispaa na waziri wa mambo ya ndani walitakiwa wawe wamejiuzulu nafsi zao ili kupisha uchunguzi huru!
 
Mimi naona serikali ya CCM ifute vyama vya upinzani na ifute kabisa democratic system.Hii itatusaidia kuokoa pesa nyingi zinazotumika kwenye chaguzi na figisu figisu nyingi za kisiasa.Pia itaepusha mauaji ya kipuuzi kama haya .Najua wamejiandaa kushinda kwa gharama yoyote ndio maana hadi risasi za moto zinatumiwa kwa watu wasio hata na kiwembe

Upuuzi gani huu?Damu za watu zinamwagika kwa ajili ya ujinga wa kujionesha kuwa tuna demokrasia,futeni basi.Pesa za uchaguzi mngelipa arrears watumishi wengi tu.Kama hamko tayari na huu mfumo futeni tu .Nimeudhika sana
 
Magufuli hii damu iliyomwagika pamoja na wote wanaopotea ipo mikononi mwake hawezi epuka....
Tumemzoea Magu kama kiongozi aneyeingilia kila sehemu ambayo imeoza..lkn kwa suala la mauaji amekua kimya kasema...hata kusema neno moja la kulaan mauaji haya hamna
 
NO WAY ASKARI HAWANA MAKOSA NI LAZIMA WAHAKIKISHE AMANI NA UTULIVU VINAPATIKANA!
Tusijiingize katika anga zao jamani!
Rip Aqulina!

Hawana makosa? Binti alikua kwenye daladala anaenda kwenye mambo yake. Halafu unasema polisi hawana makosa? Utakua na moyo wa kishetani.
 
R.I.P
Poleni wafiwa

Chadema wanaenda kuwanunua kuwapa chenji ndogo wajaze sehemu wanapita..

Uchunguzi wa polisi ufanyike kwa kifo chake hii ni lazima
Na pia uchunguzi nani anawakusanya wajae kufanya fujo bila kufata sheria na huku wanajitayarisha na mitihani n.k. lazima Chadema wawajibishwe pia.

NA HAWA POLISI NA CCM KWANINI HAWAKUFATA YA JUZI YA NAIROBI, KUWAACHIA TU. WANAJUA CHADEMA WANAPENDA YA KUUANA KUTAFUTA HURUMA.

Huyo ni mwanafunzi alikuwa amepakia kwenye daladala aka public transport anarudi nyumbani, Polisi kama kawaida yao wakarusha risasi hovyohovyo na nyingine ndio hio imemuua huyo Binti, Kifupi huyo binti hakuwepo kwenye hayo maandamo bali alikuwa mpita njia kama wengine..
 
Boss Pascal Mayalla So sad aisee, Usitegemee hatua zozote kuchukuliwa. Rejea baadhi ya matukio. Ishafika Polisi kulindwa wafanyapo kazi zao kinyume na maadili ya kazi. RIP Malaika. Poleni Familia na Wazazi na wote tulioguzwa na kifo hichi.
 
Yani Police wa Tz waajabu sana wanaangaika na serikali ambayo aiwajali kwa lolote toka mwaka juzi mishaara yao awajapandishiwa, vyeo awajapandishwa na makazi duni ila wanaona ni bora waue watanzania wenz tu.
Ile ni kazi ya laana na ndo maaana wakistaafu huwa wanamaisha ya ajabu sana kuliko watumishi wote,wanatia huruma sana,N.B kuwa polisi hakukuondoi wewe kuwa ni binadamu,polisi tuwe na utu hata jwtz katika medani adui akitupa silaha na kunyoosha mikono juu ukimuua adhabu yako mbele za haki inakusubili kwakuwa umeua asiye na hatia
 
Wewe bila shaka ni chadema...na mimi ni CCM na kinachotufanya tunavutana ni utofauti wetu wa kile ninachoamini na wewe unachoamini....Naomba nikuone haupo sahihi na wewe unione vivyo hivyo.
Labda niseme tu kiufupi sina chama, ila kwa yanayotendeka, ni wazi ccm na viongozi wenu wana force mambo. How useme chadema wamevuruga amani ndio chanzo cha polisi kumuua binti asie na hatia kweli?!!!! Mkuu tafakari.
 
Ina umiza sana kwa kweli, mwenyezi MUNGU awape faraja familiar yake pamoja na wanafunzi wenzake katika kipindi hichi kigumu wanacho pitia, RIP Aqulina.
 
huyo denti alikua anatafuta nin huko kwenye mikutano ya siasa wakati wenzie wako kwenye maandalizi ya mitihani?
Tatizo Mungu kakunyima vyote elimu na akili +hata haki zako huzijui,kila mtu anahaki ya kujumuika,anahaki ya kuhudhuria mikutano ya kampeni.Baba yako kazi yake ilikuwa ni kumdandia mama yako usiku na mchana badala kutafuta pesa ya kukupeleka shule
 
NO WAY ASKARI HAWANA MAKOSA NI LAZIMA WAHAKIKISHE AMANI NA UTULIVU VINAPATIKANA!
Tusijiingize katika anga zao jamani!
Rip Aqulina!
Huwa najiuliza sana maana ya Ku "LIKE" bandiko la mtu nini ? Je ni kwa unakubaliana naye ktk hilo bandiko au unapenda mwandiko wake ? au ni personality yake ndani au nje ya JF.
Bandiko hili la ISIS limepata like kutoka kwa mtoa post Pascal Mayalla na wengineo je ni kuwa anasapoti haya mawazo au ni lazima kila anaye reply ktk post yake ana like
 
Kwangu mimi hili lisiachwe lipite hivihivi bali hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote waliohusika na kifo cha mtanzania huyu asiyekuwa na hatia!
Naomba wanasheria wote wa serikali na wakujitegemea itumieni taaluma yenu ya sheria kwa kuishtaki serikali, ccm, nec, igp, rpcs wa kanda na mkoa wa kipolisi wa kinondoni, mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni, mkuu wa mkoa na wa wilaya, waziri wa mambo ya ndani na askari aliyerusha risasi ile ndani ya basi la abiria ili angalau marehemu aipate haki yake kwanza hapa duniani!
Mkishindwa kulifanya hili nafsi na damu ya binti huyu iwaandame ninyi na vizazi vyenu!
 
Back
Top Bottom