Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

hapa ndiyo tuongee sasa....kama umetambua kuna mapungufu sehemu basi tujadili nini kifanyike ili haya mambo yasipate nafasi tena
Kutoa haki. Wananchi wakipata haki yao hutawaona wakiandamana.

Ili uweze kubadilisha sheria lazima uwe na wabunge. Bila kuhakikisha wabunge wanaingia bungeni dhidi ya hila za CCM hatukaa tufike popote.
 
ISIS. usijifanye hamnazo, kabla ya kutoa hoja soma chanzo na ukielewe; Marehamu alikuwa abiria ndani ya daladala wala hakuwa dereva wa hiyo daladala, sijui aliingilia vipi anga za polisi.
 
Polisi aliyetekeleza mauaji haya tayari ameshaingia kwenye msongo wa Mawazo mkubwa kila akiiona picha ya huyu binti ikiwa INA circulate kwenye media, so slow death is awaiting him or her, kwakuwa nafsi zetu zimeumbwa kuregret for anything wrongdoing when we are alone, so rip in advance.
 
Dah aisee nimajonzi nauhuzuni kubwa imetawala kwenye familia ya aqulina na ndiomana watu hupenda kusema kuwa 'popote penye amani ujue kuna watu waliilipia hiyo amani' aqulina nimiongoni mwawatu watakaokuwa wameipigania amani yakifikra itayotokea siku zijazo rip
 
Paaco kuongea ni rahisi sana
Mbona na wewe hukutuma wanao wakaandamane?
Huyo mtoto ametumwa kufuata elimu sio maandamano,chadema waache kutumia wanafunzi ili kupata wingi wa watu,hiyo risasi ilitakiwa impate Mbowe ingependeza zaidi.
Rip mwanafunzi
mzee alikuwa kwenye dala dala kuna mtu kafafanua vizuri tu pitia comment #18


R.I.P AQU
 
Wanabodi,
Kwanza nitoe pole kwa kifo hiki cha malaika huyu
454a637916def479540d0fc946e0cc85.jpg


Kuna mazingira ambayo polisi wanaweza kumuua raia wa kawaida katika polisi shootout na polisi wasiwe na criminal liability kama tukio hilo linahusisha matumizi halali ya risasi za moto kwa mujibu wa miongozo yao, lakini tukio lile ni kuthibiti riots, hivyo tangu lini jeshi la polisi linatumia risasi za moto kuthibiti riots za watu wasio na silaha zozote badala ya kutumia rubber bullets?!.

...
Poleni sana, wazazi, wanafunzi wenzake, ndugu, jamaa, marafiki, wana Kinondoni wote na wote walioguswa na kifo hiki.

Hii ndio gharama ya demokrasia ambayo Watanzania wanalazimishwa kuilipa ili tuu fulani ashinde!.
Mungu yupo na haya anayaona!.

Rip, mwanafunzi wa Mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM),Aqulina Akwilini Baftaha
Watanzania wote tunamwombea marehemu roho yake iwekwe pema peponi.

Bila kumng'unya maneno, na kuingiza siasa katika uhalifu, Paskali nakubaliana na wewe kwa mengi uliyoyandika (maandishi mekundu). Ila, kama mwandishi wa habari nguri, unajua visababishi vya matukio amabayo uleta mapambano kati ya Polisi na Raia.

Unaelezaje pale swala linalopaswa kufikishwa mahakamani, viongozi wa kisiasa wanahamsisha wanachama wao, raia wasio na hatia, kuingia barabarani kuandamana, wakati kuna ushahidi kuwa siyo wote huandamana kwa amani, wapo wahalifu hutumia nafasi hiyo kufanya uhalifu au vurugu tu!

Hivi wewe Paskali uliwahi au unaweza kushiriki maandamano yasiyo na kibali, kwa sababu yoyote ile?
 
Masikini anauawa wakati sio jambazi wala hana silaha mkononi ni nani wa kutetea umwagaji huu wa damu zisizo na hatia kwanini kuilaani nchi kwa kumwagilia damu za binadamu, hii mbegu mnayoipanda mtaivuna ee Mungu ujuaye yaliyo jificha sirini tunakulilia wa Tanzania tusaidie, damu za hawa watu ziwe juu yao na familia zao kisasi kina wewe Mungu mtetezi wetu, rest in eternal peace akwilini baftah[emoji120]
 
Back
Top Bottom