Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Polisi aliyepewa amri hashtakiwi.

Anashtakiwa aliyetoa amri. Huyo aliyetoa amri si ajabu na yeye amepewa maelekezo kutoka juu.
 
Mimi naaza kuwa na wasiwasi inawezekana akawa anatumiwa na taifa jirani kuleta umwagaji damu katika Tanzania, Tanzania imekuwa kisiwa cha amani kwa muda mrefu, inawezekana wanatuonea wivu kwa stability yetu, sasa wanamtumia jamaa alete umwagaji damu katika nchi yetu. Urafiki wake na Kagame unatia mashaka makubwa sana. And he simply does not care. we have to be vigilant with this guy, jicho la tatu linatakiwa ikiwezekana apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye.
1.Awam ya Mkapa Mauaji ya mwembe chai na mauaji ya Zanzibar chini ya MAHITA.Pamoja na ile saga ya Bulyanghulu
2.Awam ya JK pia mauaji yametokea ya Mwangosi ambapo POLISI ndio waliua
3.Awam ya JPM mauaji yametokea meengi yenye UTATANISHI.
Je aman gani Unayoipromote?
 
Hii ndio gharama ya demokrasia ambayo Watanzania wanalazimishwa kuilipa ili tuu fulani ashinde!.
Mungu yupo na haya anayaona!.
Kweli inasikitisha sana eti utasikia TUDUMISHE AMANI......Shida sana nchi ikiongozwa na MALIMBUKENI NA WASHAMBA!!!!!
PUMZIKA AMANI.
 
Hapa mwanasheria msomi lazima uangalie kwa kina "DOCTRINE OF CAUSATION" na tuiangalie kwa kina concept ya "BUT FOR TEST"

Ni mawazo yangu kwamba tukichukua kijuu juu tunaweza kusahau ni nini halisi kimesababisha kifo na tukawa tunajadili matokeo ya after impact.

Kwangu najiuliza kile kitendo ambacho kiliwafanya polisi wakusanyike na mpaka kutumia nguvu kilikuwa ni halali au kimefuata matakwa ya kisheria? Nazungumzia yule mtu aliyeamrisha watu baada ya kumaliza mkutano waandamane tena akijinasibu kuwa haogopi kufa kwa nini huyu asiwe ndio '' SINE QUO NON"? (maana nyingine ndio msababishi mkubwa na asingetoa amri ile basi watu wasingeandamana bila kibali na polisi wasingekuja kuwatuliza na lisingetokea lililotoke? (BUT FOR TEST)

Ni maoni yangu kuwa viongozi wa siasa wana wajibu wa kuangalia impact ya matamshi wanayoyatoa kwenye majukwaa kwani yanaweza kuwa ndio primary cause ya matukia kama haya.

Kwenye vurugu,na ukifuatilia kwa makini ile video ya ufungaji wa kampeni utaona maneno makali aliyoyatoa kuhusu vyombo vya usalama na washaabiki wake walikuwa wanaitikia kwa jazba sana sasa kama katika msongamano ule na katika uchochezi ule mzito uliotolewa kwenye kadamnasi ile kwa nini yule aliyetoa maneno na ammri ya wazi ya kuandamana bila kibali wala sababu za msingi asiwe ndio actua cause?
 
NO WAY ASKARI HAWANA MAKOSA NI LAZIMA WAHAKIKISHE AMANI NA UTULIVU VINAPATIKANA!
Tusijiingize katika anga zao jamani!
Rip Aqulina!
Huyu binti hakuwa kwenye siasa alikuewa kwenye daladala sasa anga za askari zimeingiaje labda?Weledi unahitajika kwa hawa askari vinginevyo haya matukio yanatufanya tufikirie vibaya kuhusu uwezo wa kufikiri na kutenda
 
Hakusaidii waandishi wa habari mnanguvu kubwa kuliko Risasi za Watawala lakini mmekuwa waoga kutumia kalamu na karatasi zenu. Mko tayari kusifu na kuabudu.

Unabahati ya kuwa mwandishi na mwanasheria
Jiulize ndani ya nafsi yako umechangia kwa kiasi gani binti huyu kukatishwa masomo yake na ndoto zake.

RIP Aqulina

Mimi naona kwa hili tu tusimhukumu Pascal.kwa kuwa nafikiri kuleta tu huu uzi na kusema kwa uwazi bila ya yeye kujificha,ametimiza wajibu wake, kwa kiasi kikubwa,nami nampongeza.

kwa kweli ni wajibu wa serikali kuchukua hatua sasa.
Pole kwa familia na watanzania wote wenye nia njema kwa matukio mabaya kama haya.
 
Yani Police wa Tz waajabu sana wanaangaika na serikali ambayo aiwajali kwa lolote toka mwaka juzi mishaara yao awajapandishiwa, vyeo awajapandishwa na makazi duni ila wanaona ni bora waue watanzania wenz tu.
Usiseme hivyo kuna wengine na joto LA dar wanalala kwenye vibanda vya mabati.Poor plsi.
 
Kwenye vurugu,na ukifuatilia kwa makini ile video ya ufungaji wa kampeni utaona maneno makali aliyoyatoa kuhusu vyombo vya usalama na washaabiki wake walikuwa wanaitikia kwa jazba sana sasa kama katika msongamano ule na katika uchochezi ule mzito uliotolewa kwenye kadamnasi ile kwa nini yule aliyetoa maneno na ammri ya wazi ya kuandamana bila kibali wala sababu za msingi asiwe ndio actua cause?[/QUOTE]

Kwanini asiwe mkurugenzi aliyeshindwa kutoa barua ya utambulisho kwa mawakala wa chadema?
 
RIP Aquillina.
Waacheni Polisi wafanye kazi yao. Naona lawama zinaelekezwa Polisi lakini Mnajisahaulisha kuwa Walioanzisha Maandamano hayo walikuwa na Vibali Halali au?
Kumbukeni jana ilikuwa ni siku ya kufunga Kampeni na leo ni uchaguzi. Damu iliyomwagika ni KAFARA ya uchaguzi.
 
Huyu binti hakuwa kwenye siasa alikuewa kwenye daladala sasa anga za askari zimeingiaje labda?Weledi unahitajika kwa hawa askari vinginevyo haya matukio yanatufanya tufikirie vibaya kuhusu uwezo wa kufikiri na kutenda
kwani tuna maaskari wadhoefu ,
 
Hapana mkuu wana njia nyingi za kutuliza vurugu siyo lazima risasi za moto, ni upuuzi na ushenzi tu uliozoeleka TANZANIA mauaji kuwa sehemu ya maisha na watu kuona ni kawaida tu wakanyamaza nina uhakika ushenzi huu huwezi fanya kwa watu wanaojitambua kama kenya
Ficha upumbavu wako kwa kunyamaza kimya. Unajua wanachofanywa Raia wa Kenya na Polisi wa huko!? Unajitoa fahamu kama kungwi la unyagoni!
 
1.Awam ya Mkapa Mauaji ya mwembe chai na mauaji ya Zanzibar chini ya MAHITA.Pamoja na ile saga ya Bulyanghulu
2.Awam ya JK pia mauaji yametokea ya Mwangosi ambapo POLISI ndio waliua
3.Awam ya JPM mauaji yametokea meengi yenye UTATANISHI.
Je aman gani Unayoipromote?

Siku hizi hawahubiri amani tena, ni lini umemsikia akitamka neno amani toka aingie madarakani, yeye ni confrontation tu ndo raha yake
 
Back
Top Bottom