Amani iwe nanyi, nawaonya CCM na Police wenu acheni kuona watanzania wote ni mbumbumbu. Tangu nizaliwe sijapata kuona mtuhumiwa anajichunguza mwenyewe na kujihukumu.
Imefika wakati Police kuua Raia ni kitu cha kawaida mpaka leo nakumbuka mlivyomuua kikatili marehemu Daudi Mwangosi, juzi mmemuua binti mdogo asie na hatia kisha mnaitisha press conference mnasema eti mnafanya upelelezi; yaani mnajichunguza na kwamba mnawahoji police na mnawashikilia wafuasi 40 wa CHADEMA pia mnamtafuta Mbowe, hii cjaielewa ni nani hasa alifyatua risasi ni Mbowe, Polisi au CHADEMA?
Walioua wanajulikana mnawalinda na wale police sio wajinga inamaana walitumwa je nani alowatuma? Nilitegemea mumwajibishe alowatuma police kufyatua risasi sio kumtafuta Mbowe. Mbowe ndo alowatuma kufanya mlilofanya, je msimamizi wa uchaguzi angewapa CHADEMA viapo vyao mapema kama alivyowapa CCM haya yote yasingetokea.
Kwa hili la mauji lawama zote nawalaumu CCM, time ya uchaguzi na police mbegu mnayopanda ipo siku itamea na kutoa matunda ambayo itabidi muyavune maana apandacho mtu ndicho atakachovuna.
Police na CCM acheni sarakasi damu za wanyonge zinawalilia kutoka ardhini mjitasimini mkatubu.
Mungu tunusuru Tanzania ni yetu zote sio Mali ya CCM