Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Unajua kulikuwa na vibaka wangapi,unajua ni nani alikuwa anaandamana kwa dhati,unajua ni yupi alikuwa chadema na yupi hakuwa chadema......!? Haya mambo lazima uangalie kwa kubalance
Kaka una poor reasoning. Huyo kibaka alikuwa kwenye daladala lililokuwa likipita barabaran?
Kama polis wamefunzwa vizur, kulikuwa kuna haja gani ya kufyatua live round kwenye daladala ?
 
Kwanza natoa pole kwa familia ya Aqulina Akwilini Baftaha na kitendo hicho kilaaniwe.. Tanzania ni nchi ilyokuwa ikisifiwa kwa Amani na utulivu lakini kwa mambo yanapoelekea na serikali isipochukua tahadhari ya haraka hiyo amani na utulivu itakuwa historia. Vyombo vya usalama vichukue mfano wa Kenya wakati Raila Odinga alipojiapisha kuwa Rais wa wananchi, vyombo vya usalama hawakuingilia wala kuzuia yale maandamano matokeo yake hakuna mkenya hata mmoja aliuwawa. Serikali itafakari kwa makini sasa ni miaka 20 ya mfumo wa vyama vingi na demokrasi ni vigumu kuifuta dhana ya watanzania katika kutimiza haki zao kikatiba kufanya mikutano ama maandamano ni vizuri sana kama serikali kutotumia nguvu katika kuzuia haki hizo. Uchaguzi wa Kinondoni ufanyike kufuata taratibu zote na mshindi halali atangazwe
 
Kwa hiyo unataka kuniambia huyo binti aliwekwa target kabisa kama unaanza kuniambia niangalie na sura....!!?Chadema ni chanzo cha uvunjifu wa amani
 
Kumbe ndio huyu, aisee nilidhani ni mwanaume.
R.I.P.
 
Washitakiwe wapi mkuu. Ndio kwanza walipandishwa vyeo na kuhamishiwa makao makuu ya polisi dar. Pumzika kwa amani Msomi wetu.

..RPC Kamuhanda alipandishwa cheo na kuhamishiwa makao makuu.

..ukiangalia video ya tukio lile utaona kwamba Kamuhanda alikuwa na mshawasha wa kuwapiga chadema.

..Askari polisi aliyemlipua Mwangosi alishtakiwa na kuhukumiwa kifungo.

..Mpaka hapo utaona kuna sababu za msingi kabisa kwa mjane wa Mwangosi kulishtaki jeshi la Polisi kwa kusababisha kifo cha mume wake.
 
Ni kweli,lakini inasaidia nini?Kwa mfano Mimi hata nikipewa mabilioni ya pesa uchungu na hasira juu ya wote waliohusika na kifo cha mdogo wangu kwa namna moja au nyingine hazitaisha milele.Nawachukia sana,tulikuwa wengi sasa idadi imepunguzwa kwaajili ya ulevi tu wa madaraka!Sawa,Mungu yupo na atatuimarisha na kutuonyesha njia sahihi ya kukabiliana na waabudu miungu.pumzika kwa amani mdogo wangu,hukuwa na kosa lolote lakini wameamua kukatisha ndoto zako.Aah inatosha sasa!Tanzania gani hii?
 
Vipi kama hiyo risasi haikupigwa na polisi!??maana inabidi tuanze kuwaambia ukweli wenu na Umafia wa viongozi wenu.....!!
Nani mwingine alikuwa na assault rifle eneo lile?
Vip uchunguz ukitoka na risas iliyopatikana mwilini imetoka kwenye bunduki za polis? Una la kusema hapo
 
Usinieleze mambo ya chadema na hao vibaka unaowasema. Mm nakuambia haikuwa sahihi kutumia silaha za moto mpaka binti atolewe uhai wewe unaniambia chadema wamefurahi. Polisi wasitumie silaha za moto kama waandamanaji hawajabeba silaha za moto. Wapita njia wasiojua kuna maandamano ni wengi hawana haki ya kuuwawa.
 
signature yako inamaanisha tofauti na shairi lako. Any way wazazi ndo wamepoteza wengine tutasahau leo.
 
Kuna vijana wa propaganda watajitokeza na kusea Chadema wamejipiga risasi ili iwe karata yao ya uchaguzi alafu unakutana nao kwenye nyumba za ibada wanasali
 
Chadema walaaniwe kwa Kuwa sehemu ya sababu ya kifo cha binti huyu.....!!Polisi walikuwa katika sehemu yao majukumu yao kulinda amani Baada ya Chadema kuivuruga.
Je sehemu nyingine ya mkurugenzi aliyesababisha ifanyweje?
 
Na wewe Utoe habari ya Mtulia ndiyo chanzo....thn ndiyo tujadili.!!!Hatuwezi kujadili tu kile unachopenda ukisikie wewe.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…