Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout? RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!

Chadema walaaniwe kwa Kuwa sehemu ya sababu ya kifo cha binti huyu.....!!Polisi walikuwa katika sehemu yao majukumu yao kulinda amani Baada ya Chadema kuivuruga.
Well hiyo laana haitafika mahali zaidi ya kuishia kwenye mdomo wako.
Sawa hata kama polis alikuwa kazin, kulikuwa kuna ulazima wa kufyetua risasi kwenye daladala lilikuwa limebeba wananchi ambao hawaandamani?
 
Hili jambo usiliangalie kwa macho mawili...!!Ni wangapi walikuwa wanaandamana kwa amani?ni wahalifu wangapi walikuwemo katka hayo maandamano?!...Bila hivyo uhalifu ambao ungetokea leo tungekuwa tunaongea mambo mengine zaidi ya haya...
Walikosa obtion kabisa mpaka kutumia risasi za moto? Embu Weka siasa pembeni halafu rudi juu angalia hiyo picha halafu useme kama ilikuwa sahihi kutumia silaha za moto. Hili si jambo jepesi kama unavyoliangalia wewe, ukitaka kuamini karibu kwenye msiba wa huyu binti.
 
..Mjane wa Daudi Mwangosi anaweza kufungua kesi ya madai dhidi ya jeshi la Polisi.

..Wazazi wa Aqulina wanaweza kulishtaki jeshi la Polisi.

..Lt.Gen.Imran Kombe aliuawa na askari polisi kwa makosa. Familia yake ilifungua kesi ya madai na mahakama akaamuru walipwe fidia.
Hakuna fidia inayolingana na thamani ya uhai wa mwanadamu
 
Ipo siku ccm mtatoka hamtaweza kuua watanzania wote ,ccm mtatoka tu kama Mugabe,Jacob Zuma wametoka ccm mtatoka,mnatumia nguvu sana kwanini msiache watu wakachagua wanapotaka,mnaminya democracy kwa nguvu ,mmeona wananchi wameichoka ccm mpaka wanaimba mtawaua ,raia mnawabomolea makazinya kuishi eti wawapende ccm Hakuna,,,Ccm mwisho wenu mbaya na mna laana kubwa mkiongozwa na mwenyekiti wenu
Kama mmeona uchaguzi wa kinondoni kama tupo Iraq jamani,ccm tumewachoka
Na nyinyi police ipo siku yenu nawaambieni tunyanyaseni raia badala ya kutulinda mnapiga risasi hovyo hivi jeshi lipo wapi
 
..hivi Polisi walishashtakiwa kwa mauaji ya Daudi Mwangosi?

..naunga mkono Polisi kushtakiwa kwa uzembe na matumizi ya nguvu iliyopitiliza na kusababisha kifo cha Aqulina Akwilini Baftaha.

..R.I.P Aqulina.
Washitakiwe wapi mkuu. Ndio kwanza walipandishwa vyeo na kuhamishiwa makao makuu ya polisi dar. Pumzika kwa amani Msomi wetu.
 
Mkuu chanzo ni Mtulia...CCM na police kutumia live ammunition ni kosa kwa raia wao Mimi imeniumiza sana kuwa na matukio yanayosababisha vifo kuwa ya kijinga sijapenda kabisa iwe kifo kitokee kwa MTU yeyote wa chama chochote ni ujinga huo na kushabikia uvyama katika ishu ya kifo ni ujinga plus...
Kiongozi kwa hilo Unaeleweka...tatizo humu watu wana attack direct bila kuangalia hayo mavyama yao ndiyo kimekua chanzo cha kuzima ndoto za binti huyu.....Kiongozi hapo chadema wasingeingia barabarani kungetokea hii balaa?!na Mambosasa alisema toka mapema zaidi ya mara moja lkn hawasikii.
 
Polisi wata pata wapi IQ wakati ajira hiyo ni kwa watu walio feli elimu ndo waje kutulinda.povu ruska
 
Unajua kulikuwa na vibaka wangapi,unajua ni nani alikuwa anaandamana kwa dhati,unajua ni yupi alikuwa chadema na yupi hakuwa chadema......!? Haya mambo lazima uangalie kwa kubalance
Sioni balance yoyote hapo unayotaka niione. Hao chadema kama walikuwa wanavunja sheria na hao vibaka wao bila kuwa na silaha za moto then hakukuwa na sababu ya kutumia silaha za moto. Jeshi letu Lina njia nyingi sana za kuzuia uhalifu. Uende kwe msiba wa huyo binti kama utaweza afu wakati wakimfukia huku wakiimba zile nyimbo za kumuaga utafakari upya hiyo balance yako unayotaka niione.
 
Well hiyo laana haitafika mahali zaidi ya kuishia kwenye mdomo wako.
Sawa hata kama polis alikuwa kazin, kulikuwa kuna ulazima wa kufyetua risasi kwenye daladala lilikuwa limebeba wananchi ambao hawaandamani?
Vipi kama hiyo risasi haikupigwa na polisi!??maana inabidi tuanze kuwaambia ukweli wenu na Umafia wa viongozi wenu.....!!
 
Wa kulaumiwa ni Chadema....kwani viapo vinapatikana kwa kuleta fujo na maandamano haramu....Chadema ndiyo Chanzo cha kifo cha huyo binti na Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi
Hivi unadhani kwa Mkurugenzi kuzuia kwa makusudi viapo vya mawakala wa Chadema unategemea ni njia ipi waitumie hao Chadema zaidi ya kufanya maandamano ya amani kwenda kwa Mkurugenzi kwenda kuvidai viapo hivyo??

Hao waliosababisha kifo cha mwanafunzi huyo asiye na hatia, hakika laana zitawakuta
 
Wanabodi,
Kwanza nitoe pole kwa kifo hiki cha malaika huyu
454a637916def479540d0fc946e0cc85.jpg


Jee mnajua Jeshi la Polisi Linaweza kushitakiwa kwa kifo hiki cha uzembe na wahusika kuhukumiwa kama kifo cha Mwangosi, lakini pia serikali ikashitakiwa kwa kesi ya madai na kuhukumiwa kulipa fidia kwa familia ya marehemu?.

Kuna mazingira ambayo polisi wanaweza kumuua raia wa kawaida katika polisi shootout na polisi wasiwe na criminal liability kama tukio hilo linahusisha matumizi halali ya risasi za moto kwa mujibu wa miongozo yao, lakini tukio lile ni kuthibiti riots, hivyo tangu lini jeshi la polisi linatumia risasi za moto kuthibiti riots za watu wasio na silaha zozote badala ya kutumia rubber bullets?!.

Tena kuna ushahidi wa kutosha na usiotia shaka, mara nyingi uvunjifu wa amani unasababishwa na polisi wanaodhibiti maandamano hayo!. Kama polisi wangesimamia na kuwapa ulinzi Chadema katika kufuata viapo vyao ili wakiona vurugu ndipo waungilie, what did they stand to loose?. Kilichotokea ni uzembe tuu wa polisi wetu na hakuna excuse yoyote itakayo weza kutolewa ku justify uzembe huu wa jeshi letu la polisi kupoteza maisha ya an innocent civilian just like that!.

Poleni sana, wazazi, wanafunzi wenzake, ndugu, jamaa, marafiki, wana Kinondoni wote na wote walioguswa na kifo hiki.

Hii ndio gharama ya demokrasia ambayo Watanzania wanalazimishwa kuilipa ili tuu fulani ashinde!.
Mungu yupo na haya anayaona!.

Rip, mwanafunzi wa Mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM),Aqulina Akwilini Baftaha
Hujafafanua ilikuwaje akapigwa risasi....umetuacha na maswali mengi!je alikuwa kwenye maandamano kama mshiriki? alikuwa mpita njia ?risasi zilimpata akiwa ameketi nyumbani kwao?nk. ...fafanua vizuri
 
Back
Top Bottom