Wanabodi,
Kwanza nitoe pole kwa kifo hiki cha malaika huu
Jee mnajua Jeshi la Polisi Linaweza kushitakiwa kwa kifo hiki cha uzembe na wahusika kuhukumiwa kama kifo cha Mwangosi, lakini pia serikali ikashitakiwa kwa kesi ya madai na kuhukumiwa kulipa fidia kwa familia ya marehemu?'
Poleni sana, wazazi, wanafunzi wenzake, ndugu, jamaa, marafiki, wana Kinondoni wote na wote walioguswa na kifo hiki.
Hii ndio gharama ya demokrasia ambayo Watanzania wanalazimishwa kuilipa ili tuu fulani ashinde!.
Mungu yupo na haya anayaona!.
Rip, mwanafunzi wa Mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM),Aqulina Akwilini Baftaha