Je, Protase Rugambwa ndiye Kardinali ajaye Tanzania?

Kutoa Maaskofu wa3 ndio kuwa Blessed mkuu au unamaana nyingine
Kagera imetoa maaskofu wazawa zaidi ya 20...wakiwemo maaskofu wakuu na Kardinali mmoja...

Kagera imetoa mapadre wa kwanza Tanzania
Kagera imetoa Askofu wa kwanza mtanzania
Kagera imetoa kardinali wa kwanza mweusi
Kagera imetoa askofu balozi wa kwanza mtanzania...

Bila kusahau rundo kubwa la mapadre toka mwaka 1917...
Bila kusahau majimbo makubwa matatu ya kiaskofu...


Kwa nini kagera isiwe blessed Kiimani...
 
Huu mtazamo wako siuamini hata kidogo. Maana kabla ya Muadhama Kardinali Polycarp Pengo, tayari alikuwepo Muadhama Kardinali Laurean Rugambwa. Na sidhani kama alitokea kwenye hayo Majimbo uliyoyataja.

All in all, namuombea heri Askofu Mwandamizi Protase Rugambwa, katika safari yake ya kumtumikia Mwenyezi Mungu, na pia Kanisa lake Takatifu Katoliki la Mitume.
 
Kwanini?
  • Hawezi kuwa kadinali? Kwani hawezi kuhamishwa kwenye majimbo yenye ushawishi?
  • Kwanini tusipate tena kiti cha ukadinali?
Kupata kiti cha ukadnali sio nyepesi sana kwa nchi zetu hizi kwa sababu kuna limit fulani hivi ya ukadnali, ijulikane kadinali yoyote huwa na kanisa lake pale Roma ajali hudumu kama paroko, kwa hiyo hayo makanisa au parokia za roma ziki jaa nafasi mpya za ukadnali ni nadra sana
 
Hivi kila nchi inakuwaga na Kadinali wake? Au ni kwa ukanda yaani regions say EAC region, Kadinali moja?
Hapana sio kila nchi inakua na kardinali kwasababu cheo cha kardinali sio chauongozi wa nchi katika kanisa.
Kardinali ni mshauri wa papa na anaingia kwenye Conclave ya kumchagua papa ikiwa hajawa na umri unaofika miaka 80.
Kuna nchi hazina makardinali na kuna nchi zinao zaidi ya mmoja
 

Ushawishi nao una nafasi yake , htsks kule kenya nairobi ndio yenye askofu ambayo na kadinali japo nae ni mstaafu
 
Huyu jamaa,kavuma sana.Nimelisikia jina la Rugambwa miaka mingi,kumbe ndiyo huyu,mbona anaonekana ni badobado sana?
Anyway,hawa ndiyo majasusi wabobezi,wanaijua dunia nje ndani.
Huyu ni RUGAMBWA wa tatu kuwa ASKOFU.

huyo unayemuongelea alikuwa Kardinali RUGAMBWA mtangulizi wa Kardinali Pengo.
 
Hivi kumbe Askofu Rugambwa yupo! Mimi nimekua nikisikia jina tu nikidhani alishafariki zamani, kumbe mwamba alikuwa zake mambele.

Halafu Askofu Paul Ruzoka kahamia wapi?
Sio Huyu yule aliefariki ni KARDINALI RUGAMBWA mtangulizi wa Kardinali Pengo.

Aliefariki miaka mingi ya 90 huko.

Huyu ni another RUGAMBWA.

Kama sikosei kuna ASKOFU mwingine nae alikuwa anaitwa RUGAMBWA Ukimtoa Kardinali Na huyu.

So yawezekana akawa rugambwa watatu kuwa ASKOFU.

Ila Sina uhakika kama wako blood related.
 
Nimekuelewa vizuri sana. Ahsante sana
 
Bala shaka huyu ni mtoto wa rugambwa alimpataje nawao hawaoi?au ni mtoto wa nduguye
 
Rugambwa alikuwa na mke?
 
Huyu jamaa,kavuma sana.Nimelisikia jina la Rugambwa miaka mingi,kumbe ndiyo huyu,mbona anaonekana ni badobado sana?
Anyway,hawa ndiyo majasusi wabobezi,wanaijua dunia nje ndani.
Inawezekana ulimsikia Rugambwa mwingine yaani kardinari Laurian Rugambwa aliyekuwa kardinari kabla ya Pengo.
 
Hapo nimeelewa sasa.

Asante.
 
Na masikini kuliko zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…