Je, Rais Magufuli alikuwa na Pacemaker au Defibrillator? Ilidukuliwa?
Nimejiuliza na kufikiria sana sana kuhusu kifo cha Rais Magufuli kilichosababishwa na mfumo wa umeme wa moyo uliokuwa unaratibiwa na pacemaker/defibrillator.

Kujiuliza na kufikilia kwangu kumetokana onyo la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Marekani (Department of Homeland Security-DHS) lililotolewa mwaka 2019 linaloonya makampuni yanayotengeneza pacemaker/defibrillator kuhusu hatari ya kifaa hicho kudukuliwa na wataalam wa udukuzi na kupelekea hata kifo kwa watu waliopandikizwa kifaa hicho.

Ukitaka kusoma onyo hilo unaweza kugonga hapa;
Link>>> Pacemakers and Hacker Dangers

Wizara hiyo ilibainisha kuwa wadukuzi wanaweza kuingilia mifumo ya pacemaker/defibrillator na kuweza kubadilisha mawasiliano yake ambapo inaweza kupelekea mtu aliyewekewa kifaa kufariki.

Wizara hiyo ilienda mbali zaidi na kusema hata wadukuzi ''mwenye uwezo mdogo'' wanaweza kudukua pacemaker/defibrillator na kufanikiwa kuleta madhara makubwa kwa watu waliopandikizwa vifaa hivyo kwa sababu vifaa hivyo havina mfumo wa uhakiki au idhini (authentication or authorization) ambao ni kinga ya mwanzo dhidi ya udukuzi.

Onyo hili lilipelekea watoa huduma ya afya nchini Marekani kuwaita wananchi wa Marekani zaidi ya nusu milioni waliopandikizwa vifaa hivyo na kuwaeleza ukweli wake.

Kama kifaa hiki kinaweza kudukuliwa hata na wadukuzi wenye uwezo mdogo na kuleta madhara au kifo, inafikirisha sana kusikia kifo cha Rais Magufuli kimesababishwa na mfumo wa umeme wa moyo uliokuwa unaratibiwa na pacemaker/defibrillator.

Inafikirisha zaidi baada ya kusoma makala iliyoandikwa na Tundu Lissu kupitia gazeti la Afrika ya Kusini liitwalo Maverick akidai alidokezwa kuhusu hali ya Rais Magufuli na chanzo cha ''uhakika'' kutoka Marekani tarehe 6 Machi.

Ukitaka kusoma makala hiyo gonga hapa;
Link>>> OP-ED: Tanzania’s five years of devastation under the presidency of John Pombe Magufuli

Ukiyachanganua maelezo ya Tundu Lissu utagundua kuwa chanzo cha ''uhakika'' walijua wamefanikiwa ''mission'' ya kudukua hasa baada ya Rais Magufuli kwenda katika hospitali ya Muhimbili tarehe 6 Machi kutibiwa ambapo inaonekana daktari/madaktari walitoa siri hiyo nje lakini baada ya kutoka Muhimbili siku ya pili hawakujua yuko wapi kutokana na usiri wa hali ya juu wa ulinzi wa Rais Magufuli.

Hata gazeti ya Kijasusi liitwalo Africaintelligence halikuweza kujua aliko na likadai habari zinazosema yuko Kenya au India sio za kweli kwa sababu limefanya uchunguzi na kugundua sio kweli.

Kama chanzo cha kifo cha Rais Magufuli kitakuwa ni kudukuliwa kwa pacemaker/defibrillator, hii itakuwa ni aibu na udhaifu mkubwa kwa vyombo vilivyopewa mamlaka ya ulinzi na usalama wa taasisi ya Urais nchini Tanzania. Taasisi ya Ulinzi na Usalama inawezekana ilikuwa imejikita katika ulinzi wa mwili(Physical security ) pekee bila kujiandaa kwenye ulinzi wa saibenetiki(cybersecurity).

Kuna baadhi ya watu watajiuliza, kwa nini pacemaker/defibrillator ya Rais Magufuli idukuliwa kwa sasa?

Mtu mwenye upeo mkubwa atajua muda huu ndio ulikuwa ni muda mwafaka kiujasusi baada ya uchaguzi mkuu 2020 kwa sababu nguvu zilizokuwa zimewekezwa katika Uchaguzi Mkuu 2020 ili kumuondoa Rais Magufuli madarakani kwa njia ya sanduku la kura au maandamano kupitia kwa Tundu Lissu kutofanikiwa.

Ukisikiliza sauti ya tatu utagundua kuwa Tundu Lissu aliwaaminisha ''majasusi'' ana uwezo wa kumtoa Rais Magufuli madarakani kwa kura au maandamano.

Ieleweke kuwa, katika baadhi ya misheni hasa za kijasusi zenye changamano na tata huwa kuna mpango(plan) zaidi ya mmoja. Baada ya mpango wa kwanza kushindwa, mpango wa pili ulichukua nafasi yake na kufanikiwa!

Nadhani hoja za kinadharia kutoka kwa baadhi ya wanasiasa hasa wabunge za kutaka kubadilisha katiba ya Tanzania ili kumuongezea Rais Magufuli muda wa Urais pia zimeharakisha sana ''mission'' hii kabla hawajaanza kuandika ''miswaada binafsi'' na kupeleka bungeni kwa sababu ungepitishwa bila kikwazo chochote!

Mission accomplished, the rest is history!

NOTA BENE.
Kwa wasiojua, pacemaker/defibrillatorni ni kifaa kidogo cha umeme chenye ukubwa kama kiberiti ambacho hufuatilia na kudhibiti wimbo wa moyo ambacho huingizwa kwenye kifua ili kufuatilia na kudhibiti sauti ya moyo isiyo ya kawaida ili kusukuma damu kwa kiwango kinachotakiwa.
URL]
Unaeleza kitu ambacho watanzania kwa mamilioni wanajua...walitaka ionekane kuwa ni Corona...lakini hakuna Mtanzania anayetaja kuwa kifo hicho kimetokana na Corona...hata media za Kenya nadhani zimeacha ujinga na upumbavu huu..wameshindwa kabisa kuwaaminisha watanzania kuwa our beloved leader amekufa kwa Corona...watanzania sisi tunajua why Magufuli died...Lissu anajua kiluchomuua Magu...right now Lissu is trembling with fear...
 
Kweli kabisa msomi anakaa na kuandaa bandiko Kama Hili? Ukiitwa uthibitishe hizo shutma utaweza?

Lissu alisema chanzo Cha kuaminika kutoka ndani ya Serikali ya Tanzania,
Lissu anahusikaje na haya? Anajeshi? Anamiliki BOT? Anamiliki nchi ya Tz?

Ule ulikuwa uchaguzi au uchafuzi?
Kiukweli km Wasomi wetu wanafikiri kiujinga ujinga kiasi hiki Basi Tena inahaki tuwe watumwa tu wa wazungu
 
Ona mjinga mwingine hapa. Watu walikufa tangu corona iingia Tanzania ni wachache? Viongozi na watu muhimu waliokufa ni wachache? Huoni imepiga mpka ikulu na kumuua rais? Nyie mlisomea shule gani zinatoa watu wajinga na wapumbavu namna hii? Ona unavyosema ujinga ule ule wa Marehemu eti kifi kilikuwepo na kitakuwepo! Sasa kama kifo kipo ndiyo tuwe wazembe na watu wafe tu kwa coroina? Ujinga mwingine bwana!
Wajinga Sana hao.
Hivi unaona treni inakuja halafu unalala kwenye reli halafu useme siku ilikuwa imefika! Kama ni hivyo huwa tunachukua tahadhari za nini sasa? Watu si tungekuwa tunapika hata mimea yenye sumu tu kwa kuamini kama imefika imefika, kwa nini kwenye boti kuna life jackets? Kwa nini kuna alama za batabarani? Kwa nini waendesha pikipiki wanatakiwa kuvaa helmet?
Msipende kuongea ujinga ili ku justify mambo ya kipuuzi. As long as uko hai, ni lazima uchukue tahadhari.
 
Unachekesha na kuhuzunisha sana kwa wakati mmoja
 
Nakumbuka Sir Seretse Khama Rais wa kwanza wa Botswana alikuwa na pacemaker kwa miaka mingi tu na alikuwa anafanya upgrading ya mara kwa mara.
Pacemaker wanatumia watu wengi. Magufuli kilichomuua ni corona ikichanganya na huo ugonjwa aliokuwa nao. Mimi nashangaa watu wanakuja na nadharia za kusadika hapa wakati inajukana kabisa ni nini kilikuwa tatizo. Karne hii siyo ya kuangalia tena mchawi ni nani watoto wetu wanapokufa kwa utapia mlo.
 
Umeandika vyema sasa jana nilishangaa sana nilipoana makala ya Lisu eti sources zake ni USA na Africa kusini.
Anaweza kuwa anapoteza maboya mwanangu, kwani huoni unaambiwa kigogo ni Didier Mlawa? Ni kupoteza tu ili mjue kigogo yuko nje kumbe tunaye
 
Hizi pacemaker huwa zahitaji kubadilishwa kila baada ya miaka 6 au 7 hivi.

Kuna risks za kutumia hivi vifaa bila kuchukua tahadhari.

1. Mgando wa damu kwenye sehemu ya kifaa hadi kwenye mkono ulio upande wa moyo. Kuna siku (hivi karibuni) akiwa kwenye ziara zake utamwona akiwa na bandage mkono wake wa kushoto.

2. Infection au au wadudu kushambulia sehemu iliyo na kifaa. hali hii hutokea miezi 12 tangu kifaa kipya kipandikizwe. Hivyo inawezekana kifaa kilipandikizwa miezi 12 ilopita. Moja ya dalili za infections ni joto kali na ndo ukaona feni yatumika kila mara.

Hii infection isiposhughulikiwa hupelekea mgonjwa kupata homa ya mapafu (Pneumonia) kuzunguka sehemu ya moyo na njia za damu kwenda kwenye moyo.

3. Kifaa hiki kikipandikizwa vibaya na kukawepo nguvu kubwa basi husababisha kuweo njia za wazi (air leak) ambapo hewa hujipenyeza kwenda kwenye mapafu. Hapo ndipo huitajika upasuaji kuondoa hewa ya ziada.
Hivyo hupenyezwa kiwaya kidogo kutoa hewa na mgonjwa hutakiwa kukaa hospitali kama siku mbili hivi.

Moja ya hatari ya pacemaker kushindwa kufanya kazi yake sawasawa ni kukutana na miali mikali ya mvuto au magnetic fields.

Mgonjwa alieathirika na kushindwa kwa pacemaker kufanya kazi yake sawasawa ni pamoja na mapigo ya moyo kuwa ya taratibu sana, kizunguzungu, kupiga kwikwi mfululizo na kupoteza fahamu na kuanguka ghafla.

Marehemu alikuwa akitumia kipoza hewa, na gari maalum kwa ajili ya kutoa huduma ya kwanza, na pia mmoja wa walinzi alianza kubeba kisanduku kidogo pengine kwa ajili ya kuichaji pacemaker.

Hivyo Pacemaker ni kifaa muhimu sana na kinahitaji watu ambao wanaelewa matumizi yake na utunzaji wake.

Naamini watu hao wapo na waliaminiwa kukitunza kifaa hicho.

Pia hospitali ya MOI huenda ina vifaa muhimu vya kushughulikia watu wenye pacemaker na kuhakikisha hawavurugi utaratibu mzima wa mstakabali wa kifaa hicho na hali ya mgonjwa.

Hata hospitali ya Mzena sidhani kama ina wataalam wa kushughulikia pacemaker.

Lakini pia siwelewi kwanini marehemu hakupata nafasi ya kubadilishiwa kifaa ambapo sasa hivi hukohuko walikoweka vifaa vya mwanzo, sasa hivi wanatengeneza kifaa hicho chenye umbo la dawa ya kidonge.

Kifaa hicho kipya hupandikizwa moja kwa moja kwenye moyo na hutumia wireless technology ambapo kukiprogram inakuwa rahisi na pia kunazuia infections ambazo husababishwa na kupandikizwa kifaa cha zamani ambacho hutumia nyaya.

Tukija kwenye suali lako lina possibilities mbili:

1. Ugonjwa wa UVIKO-19

2. Mwingiliano wenye vurugu ambao unaathiri utendaji kazi wa kifaa.

RIP John Pombe Joseph Magufuli.
Kirefu cha UVIKO ni nini mkuu
 
Unaeleza kitu ambacho watanzania kwa mamilioni wanajua...walitaka ionekane kuwa ni Corona...lakini hakuna Mtanzania anayetaja kuwa kifo hicho kimetokana na Corona...hata media za Kenya nadhani zimeacha ujinga na upumbavu huu..wameshindwa kabisa kuwaaminisha watanzania kuwa our beloved leader amekufa kwa Corona...watanzania sisi tunajua why Magufuli died...Lissu anajua kiluchomuua Magu...right now Lissu is trembling with fear...
Magufuli aliacha kuchukuwa tahadhari za corona wakati alijua yuko kwenye risk group. Matokea yake corona ilipompata ikaleta kifo. Mengine ni ngonjera za kuwadanganya watu wasio na upeo.

Badala ya serikali kukubali ukweli ifanye overhaul kwenye system nzima inayohusika na afya na ulinzi wa rais tunaposha ukweli. Matokeao yake yanaweza kuwa mabaya kwani kosa litarudiwa tena.

Ni wakati wa kujiuliza ilikuwaje dr wa rais anayejua kuwa Magufuli alikuwa kwenye risk group anamwachia aendelee na maisha bila tahadhari. Na PSU ya rais pia ifumuliwe kwani imeshindwa kufanya kazi yake.
 
Korona ilianza na Kijazi kwanza. Ikasema ngoja nisogee hapa kiti cha pili - ikapiga hapo napo!!
Ambacho huwa najiuliza hii corona inachagua?

Msingi wa swali langu ni kwa sababu huku mtaani tunajichanganya sana vijana na hata wazee, na wenye presha, visukari tena wazee lakini mbona hawafi iwe hao vigogo tu?
 
Magufuli aliacha kuchukuwa tahadhari za corona wakati alijua yuko kwenye risk group. Matokea yake corona ilipompata ikaleta kifo. Mengine ni ngonjera za kuwadanganya watu wasio na upeo. Badala ya serikali kukubali ukweli ifanye overhaul kwenye system nzima inayohusika na afya na ulinzi wa rais tunaposha ukweli. Matokeao yake yanaweza kuwa mabaya kwani kosa litarudiwa tena. Ni wakati wa kujiuliza ilikuwaje dr wa rais anayejua kuwa Magufuli alikuwa kwenye risk group anamwachia aendelee na maisha bila tahadhari. Na PSU ya rais pia ifumuliwe kwani imeshindwa kufanya kazi yake.
Corona inachagua?
 
CORONA ni ugonjwa wa kufikirika. Nina uhakika na hilo kwa sababu nimeshamhudumia mgonjwa aliyesadikika ana CORONA na alikuwa anapumulia mashine kwa miezi miwili. Sikuvaa barakoa wala kutumia sanitizer hata siku 1. Kutakana na jinsi mnavyoupa uzito hata mtu akifa kwa kugangwa na gari mtasema CORONA.
Kumhudumia mgonjwa wa corona na usipate ndiyo ukahitimisha kuwa hakuna corona? Unatania? Tangu corona iingie hujasoma kuwa kuna watu wengi tu wanapata corona na hawaugui hata kidogo? Na hii ndiyo inafanya huu ugonjwa uwe hatari kwa sababu mtu wa aina yako anakwenda kuwaambukiza watu wengine bila kujulikana.
 
Watu waliwekeza sana kwenye uchaguzi wa 2020 na walipoteza fedha zao nyingi.

Pia wapo walopoteza fedha zao baada ya 2015 ambapo "hearts and minds" zilikuwa ni kwenye mirija yao ya kuihujumu Tanzania.

Alipokuwa akisisitza kuwa Tanzania ipo kwenye vita ya kiuchumi alipaswa kuungwa mkono na kila mtanzania na hivyo ndivyo wenzetu wazungu wanavyofanya.
Mkuu unaweza kutusaidia ni kwa namna gani pesa hizo zilizowekezwa zilisaidia kufinance uchaguzi wa 2020? Kama nimekuelewa vizuri ni kuwa unataka kusema kuna kundi lilikuwa financed na hao waliopoteza pesa, hasa kwa 2020.

Halafu ni wazungu gani wanafanya hivyo, sababu ya wazungu kuziunga mkono serikali zao ni transparency iliyopo kwenye serikali, Huku kiongozi anaongea kwa mafumbo kuwa tuko kwenye vita ya kiuchumi au tunamaadui halafu anategemea kuungwa mkono na watu wote! tutajuaje kama hao maadui sio maadui binafsi tusijekujiingiza katika vita binafsi. Wangesema maadui zetu ni hawa, wamefanya hivi na hivi na ushahidi huu hapa ili tuone na tupime kama tunaweza kuwaunga mkono kama "nchi".
 
Back
Top Bottom